BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 422
- 1,049
Wakazi wa Tegeta A (maarufu kwa Bedui) tuna kero ya Barabara, huu ni mwezi wa tano sasa unaelekea wa sita, barabara ni mbovu na inatuumiza Watumiaji.
Barabara ninayoizungumzia hapa ni ile ya vumbi kutoka kwenye lamı ya kwenda Madale mpaka Centre maarufu kwa jina la Bedui.
Barabara imechimbika, mashimo kila siku yana maji, imemeguka pembeni yaani hata kupishana na Bodaboda ni shida, kila siku magari tunayapeleka services kutokana na kuharibika, ikinyesha mvua ndio kabisa hali inazidi kuwa mbaya.
TARURA wapo; Mbunge yupo, Diwani yupo lakini hakuna kinachofanyika.
Yaani kuna muda unatamani hata Wananchi tuchangishwe ili itengenezwe kwa nguvu zetu kama barabara haiwezi kuchongwa walau kuziba mashimo yaliyopo.
Mamlaka husika waangalie hili linatuumiza kwa kiwango kikubwa sana.