DC Alberto Msando akopa milioni106 benki ili kuwajengea wamachinga sehemu ya kufanyia biashara

Pozzers

JF-Expert Member
Sep 14, 2013
336
560
DC wa Morogoro Albert Msando amesema anakatwa Tsh.Milioni 2.8 kila mwezi kutoka kwenye mshahara wake wa Tsh. Milioni 3.1 kama rejesho baada ya kukopa Benki kiasi cha Tsh. Milion 106 ili kujenga vibanda zaidi ya 700 kwa ajili ya Wamachinga kufanyia biashara.

Kinachonisikitisha Mbunge na baadhi ya Madiwani tuliowachagua wanajipanga kumkwamisha.
Wanadai maamuzi ya kukopa ni yake binafsi hivyo wao hawatahidhinisha ili hilo Deni lilipwe na Halmashauri hivyo itabidi alilipe yeye binafsi
 
View attachment 1939573

Hivi akifukuzwa kazi nani atalipa ? Msando unaleta utapeli huku una kashfa ya Giggy Money unatutakia nini lakini ?
 
View attachment 1939573

Kinachonisikitisha Mbunge na baadhi ya Madiwani tuliowachagua wanajipanga kumkwamisha.
Wanadai maamuzi ya kukopa ni yake binafsi hivyo wao hawatahidhinisha ili hilo Deni lilipwe na Halmashauri hivyo itabidi alilipe yeye binafsi
Kama anakatwa Tsh. 2.8 kati ya 3.1 anajikimu vipi huyu mtu? Tungekuwa na Mamlaka za Uteuzi zenye akili huyu Bwana alipaswa akamatwe ajieleze huu utopolo alioongea.. Ila hapa kwetu tusishangae akapewa u-RC kabisa.
 
Mimi sio mtaalam wa political science au mambo mengineyo ya kiutawala, lakini this is not right na kwa namna moja au nyingine mh dc anaingilia shughuli za baraza la madiwani na halmashauri kwa ujumla.
Itoshe kusema Msando ana jambo lake Arusha mjini 2025 na naona likitimia.
 
Wakili Msomi kachanganya mkopo wa mradi wa umma na rehani ya mshahara wake.

Imagine hawa watu ndio wanaingiza Halmashauri, Mikoa na nchi kwenye mikataba.

not fit for purpose, viatu havimtoshi, huna hata mwezi kazini una mgogoro na madiwani ambao hawakujui, huwajui… ingekuwa Arusha-Moshi tungesema ana maadui. Morogoro nani ana gubu na Msando ? Wewe ndio tatizo. Failed appointment.
 
View attachment 1939573

Kinachonisikitisha Mbunge na baadhi ya Madiwani tuliowachagua wanajipanga kumkwamisha.
Wanadai maamuzi ya kukopa ni yake binafsi hivyo wao hawatahidhinisha ili hilo Deni lilipwe na Halmashauri hivyo itabidi alilipe yeye binafsi
Huyo ni Mpinzani Damu Madiwani hawana Imani nae alinunuliwa na Mzee Polepole kuunga mkono Juhudi

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
DC hana hoja hapa. Akope yeye halafu halmashauri ilipe kwani ilimtuma?
 
Kama anakatwa Tsh. 2.8 kati ya 3.1 anajikimu vipi huyu mtu? Tungekuwa na Mamlaka za Uteuzi zenye akili huyu Bwana alipaswa akamatwe ajieleze huu utopolo alioongea.. Ila hapa kwetu tusishangae akapewa u-RC kabisa.

Kuna uwezekano kaomba kupitia vyanzo vyake vyote collectively ila presentation ndio kaipamba kuwa kaomba kwa kutumia mshahara ingawa hili sina hakika pia maana wanaweza wakahitaji collateral.
 
Kama anakatwa Tsh. 2.8 kati ya 3.1 anajikimu vipi huyu mtu? Tungekuwa na Mamlaka za Uteuzi zenye akili huyu Bwana alipaswa akamatwe ajieleze huu utopolo alioongea.. Ila hapa kwetu tusishangae akapewa u-RC kabisa.
Absolutely anataka kusema madc wengine hawana utu na akili kama yy.. binafsi ni popularity anatafuta.
Kwann jambo hilo ajivike wakati kuna halmashauri, mkoa ,mbunge n.k wakushirikishaonce a traitor always a traitor.
Alafu waziwazi anamu'outshine mkuu wa mkoa
 
Hili ni somo zuri sana kwa wale wanaowaona wamachinga kuwa tatizo na kuja na mapendekezo kwamba wafukuzwe mijini.

Hongera kwa Alberto Msando kwa uwezo wako mkubwa wa kuona tatizo sio wamachinga ila miundombinu, na hongera tena kwa kutatua tatizo badala ya kulalamika na kutumia nafasi yako kuumiza hawa raia.

Hawa ndio viongozi tunaowataka Tanzania ya sasa. Viongozi wenye uwezo wa kutatua matatizo papo kwa papo na sio kuongeza matatizo

Wale mtakaochukizwa na hili ameweka wazi kwamba alifuata taratibu ili kuondoa manenomaneno
 
Hata siku moja usimwamini mwanasiasa.

Kama ameamua mkopo wake liwe jambo la wazi, aweke hadharani executed term loan / loan agreement tujionee kwa macho yetu.

Na pia collateral gani ameziweka ku secure huo mkopo?

Mkopo ni wa muda gani?

Kama amekuwa guaranteed na kazi yake, vipi akitenguliwa kesho?
 
Back
Top Bottom