DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

nsekwa

JF-Expert Member
Dec 18, 2015
936
1,000
Kuna tatizo kubwa sana Dawasco Kimara, tangu mwezi wa tatu hawajaleta bili, tumefuatilia tukaambiwa mita imebadilishwa na hakuna kumbukumbu lini wamebadilisha, na tangu waibadilishe hawajaisoma na hawana hata ratiba ya kuisoma. Nimepiga picha mita wakadai inasoma unit zaidi ya 150 ambazo gharama yake ni zaidi ya 240000, lakini cha ajabu ni kuwa hawana kumbukumbu lini wamebadili hiyo mita, na mpaka mara ya mwisho walikuwa wakitoa bili kwenye akaunt kwa kuunganisha kwenye uniti za mita ya zamani, na hata juzi baada ya kuwafuata ofisini walitoa bili ya kukadiria kwa kutumia namba ya zamani wakati mita imeshabadilishwa.
Mita imebadilishwa bila hata taarifa kwa wahusika, hivi kama mita imetolewa kwingine ikiwa na unit nikawekewa mimi kwa visa au fundi kahongwa huko aihamishie kwangu nitaelewaje? wasiwasi mwingine mkubwa ni kulipishwa mara mbili kwa kwa sababu inaonekana mita imefungwa zamani na wakaendelea kutoa bili kwa kukadiria kwa mita ya zamani.
Na inaonyesha kama kwamba hawana uelewa na usomaji wa hizo mita mpya. Utakuta unit 9.5 wanakwambia 95! Hivi waweza kutumia unit 95 za maji ndani ya mwezi mmoja na maji yanatoka mara mbili tu kwa wiki kwa familia moja?
Imafika kipindi tunaamini kuwa wanalazimisha kutengeneza mazingira ya kukatia watu maji ili magari yao ya mitaani waweze kuuza maji.
 

nsekwa

JF-Expert Member
Dec 18, 2015
936
1,000
Wameniboa kinoma
Maana mwezi April sikuwa na deni
Halafu mwezi huu watu tumetumia maji ya mvua mwanzo Mwisho halafu wanasema nimetumia unit 25 sawa na 35,000 huu ni wizi maana nalipa bili kila mwezi hivyo matumizi yansjulikana
Hizo unit 25 yawezekana ni 2.5, kuna mita mpya wameleta zinawashinda kusoma utafikiri wote hawajaenda shule, aibu sana kwa DAWASCO
 

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
13,760
2,000
Hongereni sana sasa hivi mnajitahidi sana kusambaza maji hata yale maeneo sugu ambayo yalikuwa hayapati maji kabisha licha ya kuwa na mtandao wa mabomba hapa dsm
 

kapuchi

JF-Expert Member
Oct 8, 2008
223
225
Dawasco Dawasco tunawaomba sana sisis wakazi wa Bunju B...Mkabala na myumba za mradi wa nyumba za watumishi wa serikali TBA ..hatuna maji kabisa na tunapata shida kubwa ya maji

Mwanamke bado anabeba ndoo kichwani ...hii ni wiki ya tatu hatuna maji tuanaomba mtandaze mabomba yenu ili tupate maji safi
kwa muda mrefu sasa tunatumia maji ya kununua kwa wenye maboza ya maji, na gharama ni kubwa sana jamani...hebu mtusaidie na sisi tufurahie huduma zenu

tumeshapiga kelele sana lakini hatuoni kinachoendelea watu wametaharuki hivi tuko somalia jangwani au ni hii Tanzania Dar es Salaam
 

nguvu

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
11,826
2,000
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani. DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.

Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)
Ubungo national housing karibu na uwanja wa mpira wa miguu wa shekilango jirani na car parking ya ubungo plaza sijui wakazi wa eneo hilo tumewakosea nini dawasco maji hatupati na ikitokea bahati nzuri tukapata basi maji ni machache kiasi kwamba wengine tunapata jioni muda mnayakata, tatizo ni nini jamani?
 

Ng'onyo

Senior Member
Sep 2, 2011
142
225
Habari, mi naishi Kiwalani lakini pia nina makazi Gongo la mboto, Kwakweli Sitambui kabisa kama kuna Shirika linaloshughulikia masuala ya Maji, toka niwe Dar es salaam mimi na Familia yangu tunakunywa na kutumia maji ya visima.
 

Come27

JF-Expert Member
Dec 1, 2012
6,017
2,000
Habari, mi naishi Kiwalani lakini pia nina makazi Gongo la mboto, Kwakweli Sitambui kabisa kama kuna Shirika linaloshughulikia masuala ya Maji, toka niwe Dar es salaam mimi na Familia yangu tunakunywa na kutumia maji ya visima.
Dawasco ipo wilaya ya kinondoni na ubungo na ilala sehemu chache za kariakoo, Buguruni, Posta, na wilaya ya Temeke sehemu chache za keko
 

DAWASA

Senior Member
Oct 7, 2010
132
225
Ubungo national housing karibu na uwanja wa mpira wa miguu wa shekilango jirani na car parking ya ubungo plaza sijui wakazi wa eneo hilo tumewakosea nini dawasco maji hatupati na ikitokea bahati nzuri tukapata basi maji ni machache kiasi kwamba wengine tunapata jioni muda mnayakata, tatizo ni nini jamani?
ndugu mteja tangu jana kuna matengenezo ya bomba la ukubwa wa inch 4 maeneo ya shekilango hivyo ikalazimu kufunga maji eneo hilo mpaka matengenezo yatakapokamilika. pole kwa usumbufu..tunategemea kurudisha huduma ya Majisafi Leo
 

Mantombazane

JF-Expert Member
Sep 7, 2014
552
500
Kusema kweli DAWASCO sasa hivi wanafanya kazi!. Mimi ni mkaziwa Mbezi kwa Musuguri eneo ambalo limekuwa na shida KUBWA ya maji kwa muda mrefu sana kiasi kwamba wenye makenta/magari ya kuuza maji walijitangazia utawala na ufalme huku kwa kuwa ndiko soko lao kubwa liliko na wengine wakaendelea kuongeza magari ya kuuza maji kutokana na tatizo sugu la maji lililokuwepo huku. Yaani licha ya kufungiwa mabomba ya mchina miaka mingi iliyopita hatukuwahi kuwa na maji kwa kisingizio eti hayana nguvu ya kufika huku yakawa yanaishia mtakuja karibu na line kubwa za Tanesco ambako kusema kweli yule bwana kapiga hela sana kwa sisi huku kukosa maji. Hivyo kwa muda mrefu tukabaki na mabomba na mita kama mapambo na baadhi ya miundo mbinu ikaanza kuharibika ingawa tulikuwa tunaambiwa wanaouza maji ndio wanaofanya tusipate maji kwakuwa walikuwa wanawahonga baadhi ya maofisa wa shirika ili maji yasifike huku ili wao wafanye biashara ya maji. Lakini sasa hali ni tofauti. Kila siku tunaona wafanyakazi wa DAWASCO wakiwa katika bajaji zao au pick ups wakizungukia maeneo yote ya mabomba na nyumba zote zilizofungiwa mabomba ya mchina na kwa mara ya kwanza kabisa sasa watu wameanza kupata maji majumbani na mimi nikiwa mmoja wapo. Juzi nilishangaa naamka asubuhi nakuta nyumba nzima imelowa maji kumbe maji yalitoka usiku maana tulishakata tamaa na maji ya dawasco.

MUNGU AWABARIKI SANA NA PONGEZI SANA KWA UONGOZI KUSAMBAZA MAJI KWA WINGI KWANI NI WAZI MNAPOKUWA NA WATEJA WENGI NDIVYO MNAVYO PATA PESA ZAIDI. KEEP IT UP vile vifanyakazi vijizi vijizi na viofa vifisadi fisadi fukuzia mbali vikaisome namba huko. Naomba pia mkabiliane na mtandao wa wafanyabiashara ya maji ambao unaweza kuvuruga miundo mbinu yenu ili maji yasitufikie ili wao wafanye biashara kwani tuhuma kama hizi zipo kwa muda mrefu. Pia muwachunguzi maofisa wenu wanaoshirikiana na wafanya biashara wa aina hiyo na wengine wanamakenta ya kubeba maji hivyo wasije kutuletea shida tena. Ni vizuri pia mkawa na mamenenja au wasimamizi wa maendeo kama kata au mitaa au vitongoji kwa ajili yakufuatilia huduma zenu kuhakikisha kuwa hazikatiki au hazihujumiwi. KEEP IT UP!!!
 

Nkasumuni

JF-Expert Member
Nov 18, 2015
449
250
Hi naomba muangalie bomba la kinondoni kwenye njia mbovu kama unaelekea bar ya four ways ukitokea biafra kuna mfereji umejaa maji ambayo yanavuja siku kibao angalieni mnpoteza maji
 

kapuchi

JF-Expert Member
Oct 8, 2008
223
225
Dawasco Dawasco Mungu anawaona nasikitikita kusikia kuna maeneo mengi hapa jijini kna mabomba yanamwaga maji wakati Bunju B, Mabwepande mkabala na nyumba za mradi wa nyumba za watumishi wa Serikali unaojengwa na wakala wa majengo TBA , hatuna maji hata kidogo,hili linatia uchungu sana ukizingatia wanachi tunaokaa huku niwanachi wapiga kura katika serikali hii

Inatubidi tuombe maboza kutuletea maji ambayo yanatozwa kwa gharama kubwa sana ambayo hatuwezi kuilipa kutokana na gharama za maisha.

Tumetoa malalamiko mengi lakini Dawasco hawana majibu ya kutosheleza kwa nini hawaji kutandaza mabomba maeneo yetu haya na sisi tujisikie tu miongoni mwa watanzania wanaofurahia matunda ya serikali yao nzuri ya awamu ya Tano

Kilio hiki kimuendee Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,na Mh Mbunge wetu wa Jimbo la Kawe Mb Halima Mdee
 

kivava

JF-Expert Member
Apr 2, 2013
5,778
2,000
Dawasco tafadhalini sana mabomba yenu yaliyipo kwenye barabara itokayo Tandale Chama hadi Mwananyamala Manjunju yanamwaga maji usiku na mchana barabarani
Barabara imeharibika kabisa kwa maji yanayomwagika ,kiasi tunakwazika kwenda hospital ya Mwananyamala
Bajaj na bodaboda haziwezi kuelea kwenye bwawa mnalotengenezs
 

Eudorite

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
1,134
2,000
MALALAMIKO kwa uongozi wa DAWASCO. Ni mteja wa shirika kwa account namba 90084914 naishi Tabata kisiwani. Sijawahi kudaiwa na huwa nalipa bili IPASAVYO. Pia ni mtumishi wa wizara ya maji na umwagiliaji hivyo taratibu nazifahamu.

Nilipatiwa bili ya maji jumatano iliyopita. Jana jumanne wakati naelekea kibandani kulipia nikapigiwa simu na Dada wa kazi kwamba wamekuja kukata maji. Nikamwambia awaambie wasikate naelekea kulipia. LAKINI WAKAKATA.

Nikawasiliana na wahusika ofisi ya DAWASCO TABATA kwa simu. Wakasema hakuna operesheni ya kukata maji labda yamekatika. Leo asubuhi nimewapigia tena Tabata wakasema watakuja kurudisha maji. Saa tisa alasiri nawapigia wanasema WAMEKOSA MUDA hivyo LABDA KESHO.

Tafadhali naomba kufahamu yafuatayo:
1. Ni ndani ya siku ngapi mteja anapaswa kulipia bili TOKA SIKU ALIYOPATIWA BILI HUSIKA kabla hajakatiwa maji?

2. Ni deni kubwa kiasi gani ambalo litalazimu mteja kukatiwa maji?

3. Inachukua muda gani mteja kurudishiwa huduma baada ya kuwa mmemkatia na amekidhi matakwa yenu.

4. Utaratibu wa mafundi kukatia maji wateja ukoje. Iweja jana nimewaeleza kwamba naelekea kulipia wao wakakata? Iweje waje kukata wakiwa hawana vitambulisho na hawajaacha taarifa yoyote ya maandishi kutoka ofisini. Na iweje wakate maji pasipo kuwakumbusha kwanza wateja kulipia huduma?

Mwisho ni kwamba kuna uvujaji mkubwa wa maji maeneo ya huku tabata kisiwani lakini mafundi wenu wanajua kukatia maji wateja na siyo kuzuia uvujaji wa maji.

Pia watumishi wenu wa tabata hawana lugha nzuri kwa wateja na hawawajibiki kutatua shida ya wateja kwa wakati. Naomba mfuatilie.
 

BONGE LA BWANA

Senior Member
Apr 14, 2015
173
250
huku mbagala kata ya kibondemaji mmeanzisha mrad mzur tu wa maji, lkn tuna wiki sasa maji hayatoki na hamtoi sbabu kwa nini...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom