DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

bitoz dawasco haiwezi kukupa bili kwa maji usiyotumia. kaangalie kwenye mita yako uangalie jinsi mita yako ilivyozunguka na uzidishe kwa bei ya Tsh 1663 kwa unit
Nilichoongelea siyo mahesabu
Sijatumia sana maji mwezi huu mvua zimenyesha mwanzo mwisho hizo unit 25 nilizotumia {km mbili yenu inavyodai) zimetoka wapi?
Bomba huwa nafunga na kufuli
Jaiwezekani bili ya April izidi ya May ambapo nilikuwa na maji kibao ya huwezi
Kuna walakini mkubwa
 
hujatumia sana maji ni lugha ngumu kidogo..bili uliyotumiwa ndio matumizi yako ya Maji. kwan hayo maji ya mvua uliyaunganisha kwenye mfumo wa dawasco? tafadhali kalipe bili yako kuepuka usumbufu
 
Kwanza napenda niwashukuru kwa hilo najua had I kuja humu ndani ya jamii furum in kwa sababu ya kupata Katibu mkuu Mpya Kitila Mkumbo anajua faida ya mitandao ya kijamiii kama istagram fb jamii forum

Niwape changamito ya kuongeza mapato ya dawasco ongezeni kasi ya kusambaza mabomba kwenye mitaa ya jiji la daresalam. Wateja mrawapata wengi sana. Kama Maji yanu yatakua yanapatikana kama ipasavyo

Sambazeni mabomba ya Maji taka zaidi mitaani kama eneo la Mbezi beach Na Mbezi juu mtapata Wateja wengi sana Na mtaongeza kipato watu wamechoka kunyonya Maji taka kwenye magari
Mkieza hilo mtakua mnefanikia. Kama vile tanesco wanajitaidi sana kusamabaza umeme wao kwa Wateja
 
hujatumia sana maji ni lugha ngumu kidogo..bili uliyotumiwa ndio matumizi yako ya Maji. kwan hayo maji ya mvua uliyaunganisha kwenye mfumo wa dawasco? tafadhali kalipe bili yako kuepuka usumbufu

Mbona unalazimisha mteja kulipa akara ya Maji ambayo yeye anaona hastahili? Hoja Yake huoni ina msingi? Mimi nilitarajia umshauri aende ofisi ya Dawasco iliyo karibu nae apeleke malalamiko Yake ili fundi wa Dawasco afike pale akaangalie hiyo mita pengine kuna tatizo la kiufundi kwenye hiyo mita! Sasa mambo Kama hayo mnashindwa kujiongeza!
 
Mimi ndo maana siwaelewagi kabisa Dawasco! Hadi nitakapotaka huduma ya Maji yenu ndo yumkini nitaanza kuwaelewa! Unakuta Watu wanakaa mita chache toka Bomba kubwa la maji ya Ruvu lakini miaka nenda wanababaishwa Na Dawasco! Over 55 years of Independence of Tanganyika bado tunaongelea kukosekana Kwa huduma ya msingi ya binadamu maji ninao uhakika wa zaidi ya 100% kuwa Kama mkoloni angeendelea kututawala ukosefu wa public utilities zote ingekuwa tunajifunza Kama historia! Africa tuliwahi sana kudai ukombozi na mambo yenyewe yanatushinda
 
Halafu cha kushangaza hata sasa bado swala la Maji halipewi kipao kabisa ndo kwanza Watu wananunua ndege
 
Bunju b barabara inayoelekea Mabwepande ,opposite na nyumba za watumishi wa umma Mradi wa TBA
 
Bunju b ,eneo ambalo ni opposite na nyumba za mradi wa nyumba za ser

Eneo ambalo hatuna maji ya Dawasco ni ,ni Bunju b opposite na Nyumba za watumishi wa serikali zinazomalizika kujengwa na Tanzania Building Authority TBA

Na kule Mivumoni na Madale (yes anakoishi Diamond) ambako walipaji bili wapo na huduma ya maji haipo DAWASCO
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani. DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.

Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)
Dawasco unazingua, mbona hujibu project mpya ya maji maeneo kama mpiji magoe,msakuzi,machimbo,tumejaza form kitambo tunaambiwa maji yanakuja hadi sasa hakuna kitu
 
Habari za kazi na poleni na majukumu,

Msimu wa mvua umeisha na muda si mrefu barabara za mitaani zitaanza kurekebishwa, kwani zimeharibika sana. Nauliza mumejipanga vipi kulinda miundo mbinu ya maji isiharibiwe, bomba zisikatwe kutokana na uchongaji wa barabara? Nimeuliza kwasababu, imekuwa ni kawaida kila mwaka bomba kukatwa sehemu mbalimbali wakati wa kurekebisha barabara kwa kutumia mashine hasa graders. Na ukizingatia sehemu nyingi hakuna alama za kuonyesha bomba imepita chini ya ardhi. Na hii inasababisha usumbufu wa kufatilia, hasara zisizo za lazima na inapelekea kaya zingine kukosa maji kabisa kwa kutojua tatizo limetokea wapi.

Nawashauri mtoe tangazo kwa umma, kabla ya kuanza kurekebisha miundo mbinu ya barabara wawasiliane na nyie ili muweze kutoa ushirikiano wa kuwaonyesha., au mkutane na mamlaka husika wa barabara mpange jinsi gani mtafanya kazi pamoja kuliko kuacha bomba ziharibiwe.

Asante.
 
Mbona unalazimisha mteja kulipa akara ya Maji ambayo yeye anaona hastahili? Hoja Yake huoni ina msingi? Mimi nilitarajia umshauri aende ofisi ya Dawasco iliyo karibu nae apeleke malalamiko Yake ili fundi wa Dawasco afike pale akaangalie hiyo mita pengine kuna tatizo la kiufundi kwenye hiyo mita! Sasa mambo Kama hayo mnashindwa kujiongeza!
Wameniboa ila nimeamua kukausha
Nalipa bili kila mwezi
Halafu mwezi ambao mvua zimenyesha mwanzo mwisho na bomba nimelipiga kufuli naletewa bili kubwa kuliko miezi mingine ambayo nafungulia bomba kila siku
Halafu bado wananiona mjinga kulalamika
Labda mita zao zinasoma hadi maji ya mvua!!!
Wapotezee
 
Dawasco mnawezaje kujihakikishia kuwa hawa wanao uza maji hawawaibii? mna utaratibu gani wa kuwafatilia?
 
Dawasco mnawezaje kujihakikishia kuwa hawa wanao uza maji hawawaibii? mna utaratibu gani wa kuwafatilia?
ndugu mwananchi hawa wauza maji kwa magari maarufu kama bowsers kwanza tumewasajili kujua idadi yao na point wanazozichukulia maji...pili maji yanayofungwa kwenye vioski vya kuwauzia wao Maji tumeiweka kwenye system ya pre~paid meter hivyo wanalipa kulingana na kiasi wanachonunua.
kwa wauzaji wadogo wadogo (vendors) hatuwasimamii sisi kama Dawasco ila tunajitahidi kupeleka huduma ya Majisafi kwenye maeneo biashara inapofanyika ili kuipunguzia makali. mfano biashara hiyo iko sana maeneo ya magomeni na dawasco ilichofanya imejenga vizimba vya maji na tunauza kwa bei ya chini ili kurahisisha upatikanaji wake.
 
Habari za kazi na poleni na majukumu,

Msimu wa mvua umeisha na muda si mrefu barabara za mitaani zitaanza kurekebishwa, kwani zimeharibika sana. Nauliza mumejipanga vipi kulinda miundo mbinu ya maji isiharibiwe, bomba zisikatwe kutokana na uchongaji wa barabara? Nimeuliza kwasababu, imekuwa ni kawaida kila mwaka bomba kukatwa sehemu mbalimbali wakati wa kurekebisha barabara kwa kutumia mashine hasa graders. Na ukizingatia sehemu nyingi hakuna alama za kuonyesha bomba imepita chini ya ardhi. Na hii inasababisha usumbufu wa kufatilia, hasara zisizo za lazima na inapelekea kaya zingine kukosa maji kabisa kwa kutojua tatizo limetokea wapi.

Nawashauri mtoe tangazo kwa umma, kabla ya kuanza kurekebisha miundo mbinu ya barabara wawasiliane na nyie ili muweze kutoa ushirikiano wa kuwaonyesha., au mkutane na mamlaka husika wa barabara mpange jinsi gani mtafanya kazi pamoja kuliko kuacha bomba ziharibiwe.

Asante.
asante kwa ushauri tumeupokea
 
Mimi kilio changu uku maeneo ya ubungo, Mabomba mengi yamepasuka sana na maji yanatoka Mara 4 kwa wiki. Barabara zote zinavuja maji. Mito inajaa maji ivi kweli amna kitengo maalum cha kuzibiti upotevu huu wa maji au mpaka Muheshimiwa Raisi aone ni tatizo la uvujaji wa maji
 
Aseee sijawai kutoa au kusema chochote kuhusu
DAWASCO. Ukweli ni kwamba last Week mmetoa maji yananuka Dawa bana sijui kama ni salama
 
Back
Top Bottom