DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Tandika Azimio,wilayanI Temeke takriban mwezi mmoja sasa mabomba yanatoa maji yenye uchafu, kuna chembe chembe nyeusi zimechanganyika na maji. Hii ni hatari sana kwa afya za watumiaji.
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani. DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.

Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)

DAWASCO HUDUMA KWA WATEJA 0800110064
DAWASCO ILALA 0743 451879
DAWASCO KAWE 0743 451861
DAWASCO KIBAHA 0743 451875
DAWASCO KIMARA 0743 451865
DAWASCO KINONDONI 0743 451863
DAWASCO BAGAMOYO 0743 451877
DAWASCO MAGOMENI 0743 451862
DAWASCO TEGETA 0743 451881
DAWASCO TABATA 0743 451867
DAWASCO TEMEKE 0743 451866

Hello DAWASA, ninaishi mbezi beach, tatizo langu no namba iliyoandikishwa kwenye meter haitumiki kwa sasa kwa kuwa nilimuandika mke wangu na ameenda masomoni nje ya nchi hivyo sipati bili za maji kwa wakati na hii inanisababishia usumbufu mkubwa sana including kukatiwa maji kwa bili ndogo mno.

Nifanyaje niweze kubadili namba ili niweze kuweka ya kwangu ili nipate bili za maji na kulipa kwa wakati?
 
Kazi nzuri na ninafurahiya huduma yenu. Ila mkipewa taarifa ya maji kuvuja mahali mfike mapema kwani hasara ni kwenu. Maji yakivuja kuanzia kwenye MITA yangu nashughulika chapchap kuogopa bili kubwa.
 
Naomba kuuliza kupewa bili kwanjia ya simu, ni mda sasa kila nikijaribu kuangalia bili kwa njia ya cm sipewi majibu na salio nakua nalo.
Swali lingine ni kuhusu namba za malipo (control number) kwa mwaka huu hamtakua mkizibadilisha Tena? Naomba majibu tafadhali
 
Naomba kuuliza kupewa bili kwanjia ya simu, ni mda sasa kila nikijaribu kuangalia bili kwa njia ya cm sipewi majibu na salio nakua nalo.
Swali lingine ni kuhusu namba za malipo (control number) kwa mwaka huu hamtakua mkizibadilisha Tena? Naomba majibu tafadhali
Control no kwasasa hazibadiliki,
Ulitaka kuiangalia bill yako,download GEPG then nenda DAWASA itakuwa unaona bill yako.

NOTE
Mimi ni mteja kama Wewe,ndo huwa naangalia hivyo
 
Hello DAWASA, ninaishi mbezi beach, tatizo langu no namba iliyoandikishwa kwenye meter haitumiki kwa sasa kwa kuwa nilimuandika mke wangu na ameenda masomoni nje ya nchi hivyo sipati bili za maji kwa wakati na hii inanisababishia usumbufu mkubwa sana including kukatiwa maji kwa bili ndogo mno.

Nifanyaje niweze kubadili namba ili niweze kuweka ya kwangu ili nipate bili za maji na kulipa kwa wakati?
Nenda kwenye ofisi zao ukiwa na barua ya kuomba kubadilishiwa no ya Simu,uiweke hiyo inayopatikana! Au mtafute anaewasomea meter umuelezee atakusaidia. But muhimu uwe unaijua acc no yako
 
Nenda kwenye ofisi zao ukiwa na barua ya kuomba kubadilishiwa no ya Simu,uiweke hiyo inayopatikana! Au mtafute anaewasomea meter umuelezee atakusaidia. But muhimu uwe unaijua acc no yako
Thanks nilimpata anaesoma bili nikamuelezea I hope mwezi huu nitapata bill kwa namba yangu.
 
Nipo Chalinze, Nimelipia kuwekewa huduma maji kwa matumizi ya nyumbani toka mwezi Septemba 2021 mpaka sasa hawajaniunganisha na huduma ya maji,kila nikienda ofisi zenu wanadai vifaa havipo wameagiza Dar havijafika, sasa najiuliza si bora mruhusu wananchi wanunue vifaa wenyewe kuliko kupokea hela halafu mnashindwa kutoa huduma kwa wakati.
 
Ukweli Ni kwamba ninyi idara za maji mmekuwa siyo wabunifu!

KWELI mnashindwa Kuandaa mkakati wa kuvuna maji kwenye maeneo ambayo maji yanasumbua Kama Newala?

KWELI mnashindwa kufanya project ya kuvuta maji mto Ruvuma ili kusambaza maji kwenye Mkoa MZIMA wa Mtwara na hata Mikoa Jirani?

Watu Kila kukicha wanahangaika maji Serikali mpo kupitia idara yenu! Halafu mfano Masasi wananchi wanatumiwa sms eti maji hayatoki sababu ya Umeme kuwa mdogo? Ukweli mnachekesha! Hivi haya yanasamabishwa na Nini Kama siyo ukosefu wa matumishi bogus ambao hawako na creativity?

Nyambafu
 
Mimi naomba nitoe maoni kuhusu hawa wafanyakazi wa dawasa...Hivi mfano wale wanao soma meter number!! ili wangalie kma bill ya maji imelipwa au haijalipwa lakini pale unapomkosa mwenyewe... muhusika wa eneo hilo unachukuaje hatua ya kumkatia maji hamuoni kama mnaenda kinyume na taratibu

Sent from my TECNO CC7 using JamiiForums mobile app
 
Habar kwenu Mamlaka ya MAJI DAWASA.

Tulipokea gharama ziada ya matumizi yetu.
Tukafikisha malalamiko haraka ofisi zenu za TABATA SEGEREA.
MKAIKALIA uvunguni barua hiyo miezi mitatu, bado tuliendelea kufuatilia malalamiko yetu bila majawabu.
Mwisho timu yenu ikahamia kwetu kuchunguza tatizo.
Mkasema ni uunganishwaji wa Tank yetu ndio umesababisha gharama iwe kubwa.
Ufafanuzi wenu hauna mashiko, mkaingia mpaka vyoo vya ndani ili muone, tuliwaruhusu japo si sheria zenu.
Jawabu lilikosekana.

Mkaja kutufungia mita ili tusipate huduma hiyo, sasa ni mwaka bila sabab za msingi.

Tumejitahidi kutaka kuonana na mkuu wenu wa kituo, lakini nafasi hiyo ikawekewa vipingamizi vya kutoonana nae.

Sasa tumeshindwa kuwa elewa kutuzuia kumuona kiongozi wenu ili iwe faida kwenu ipi?

Ni makosa kuonana na kiongozi ili ajue kero za wateja wenu?

Sasa mnatishia kuwa peleka wateja Mahakamani kuwa hawa lipi huduma.

Mbona malalamiko yetu hamjayatatua?

Mahakama ndio sehemu ya kuongea wateja ambao hawajatatuliwa malalamiko yao?

Kuhusu kuwa peleka mahakamani waliotumia halali huduma zenu hilo sijapinga.

Nmeandika malalamiko kwa Mh Waziri, huenda nikapata utatuzi.

Tokea mwanzo hatukushindwa kulipia huduma Bali TULILALAMIKIA GHARAMA AMBAZO HAZIJATOKEA KATIKA MATUMIZI YETU.

Haraka sana tukafikisha malalamiko yetu ofisini kwenu kwa maandishi, mkakaa kimya.

Ukimya huo ni dharau.

Namba yetu ya mita ni AC 90239945.

NAWATAKIENI KAZI NJEMA.
 
Ununio mnara wa Tigo kwa mjumbe mtaa wa Mombo kuna bomba limepasuka maji yanamwagika ovyo!

Nimetaarifiwa na msamalia mwema hapa ofisini.
 
Dawasco habari?kwanza fanyeni malekebisho kwenye namba ambazo hazifanyi kazi,pili inastaajabisha kuona hadi leo 2022 ndani ya jiji kama la Dar kunasehemi eti hawapati maji hii ni aibu,ukija huku mabwepande,kibesa ,mpigi magoe ni ndoto kuzungumzia maji ya dawasco wakati nyinyi mnalipwa mishahara na posho mbalimbali lakini utendaji wenu ndio huu sasa sijui hata mnakwama wapi!
 
DAWASA Ilala
Maombi ya Kuunganishiwa Maji wakazi wa Mtaa wa Taliani kata ya Nyeburu na viunga vyake.

-Mheshimiwa Sana Meneja wa DAWASA Wilaya ya Ilala.

-kuanzia 02 January 2021 wakazi wa Mtaa wa Taliani walijaza fomu za maombi ya huduma ya maji kwenye ofisi ya serikali ya mtaa Taliani

-wananchi waliahidiwa kuwa fomu za maombi zitafanyiwa kazi na DAWASA watasambaza au watasogeza miundo mbinu ya maji mitaani au karibu na Wananchi,ili kuleta wepesi Wananchi kulipia gharama za uunganishaji.

-Mpaka Machi 2022 wananchi eneo karibu na Shule ya msingi Mtuki kwa Mjumbe Amina Vunja na Sanga bado DAWASA hawajatandika mabomba ya njia kuu na mradi huu unasusua .

-Mradi huenda ukachukua miaka mingi kukamilika.

-Mradi huwa na kipindi maalum cha utekelezaji (Time frame).

-Mradi ambao hauna time frame hauna maana,

-kwa speed hii, time frame itamalizika kabla ya mradi kukamilika.

-Ni dhahiri Serikali imewekeza fedha nyingi kwenye ujenzi wa miundo mbinu ya maji toka Ruvu Juu/Chini,

-Ni dhahiri Serikali huenda imekopa fedha kwa niaba ya wananchi au tumepata kutoka kwa wafadhili

- Ni vema Mradi ukakamilika ili wananchi wapate huduma iliyokusudiwa na Serikali ikaanza kurejesha mkopo au kukusanywa maduhuli kwa ajili ya kuwekeza maeneo mengine.

Ushauri
1). Meneja DAWASA (w) Ilala apeleke miundo mbinu ya maji mitaani au karibu na Wananchi

2). Wananchi walipe gharama za uunganishaji maji kutoka bomba kuu,

3).Meneja DAWASA Ilala, aige mfano wa Meneja DAWASA-Temeke,(kuna ndugu zangu wanakaa Mtaa wa vituka, DAWASA walitandaza miundo mbinu ya maji,mitaa yote na kuwaunganishia maji kwa mkopo,na kuwaamiua wateja walipe gharama za uunganishaji ndani ya miezi 6.Malengo ya serikali yametimia,wananchi wanakunywa maji safi na Shirika linapata mapato yake)

4). Meneja wa DAWASA Ilala awe proactive na mbunifu,"maji ni uhai".

5). Mamlaka husika zifanye performance evaluation audit kujua kama mambo yanakwenda kama ilivyo pangwa.
 
Kuna wafanyakazi wa Dawasa wanajihusisha na kufungia watu maii kwa njia ya wizi? Mitaa ya huku airport karakata, kuna mama anapita kukusanya majina ya watu wanaotaka maji na baadae huchukua hela na kumleta fundi wa dawassa kuunganisha maji.

Mapungufu.
1.pomba ni la kuungaunga
2.mita inakaa ndani
3.bei ya hati punguzo, mpk elfu 65
unaunganishwa.
4.hulipii kwa controll number.
5. Huna account a dawasco.
6.mtu aliyelipa kihalali akishaunganishwa, nao wanavizia hapohapo na kuja kufukua mtaĺo ili e wapitishe bomba Lao.

Acheni uzembe nye dawasco , mtafirisika.

Nalalamika kwa sbb nye wenyewe dawassa mkishindwa kufikia malengo yenu ya makusanyo hamawiagi kutubambikizia madeni
 
Watu wenu wa Bagamoyo niwasumbufu sana then waache kutisha Watu yani Unaletewa bili ya maji leo baada ya Masaa 2 unatuniwa mesiji na mtu wenu kuwa unadaiwa Unatakiwa ulipe Watu wa operation wako mtaani, hujakaa sawa unapigiwa huu ni usumbufu yani mtu ukae standby unasubiria msg ya Dawasa ikiingia tu ukalipe?

Mbaya zaidi mimi sio mteja msumbufu mnatakiwa mfanye hivyo kwa Watu ambao sio walipaji au wasumbufu, na msg za Kutoka Dawasa zinatosha maana zenyewe tu ni kero bado unatumia na namba nyingine mbona DAR HAWAFANYI HIVYO? HUU UTARATIBU WENU BAGAMOYO NI KERO MNO MNOO

Sent from my SM-N950F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom