DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Maji yapo lakini hayatoi maji kabisa eneo la mbezi


Maji yanamwagika mitaani majumbani hakuna

Ukiwapigia simu wanakujibu kwa nyodo na wiki nzima hawatokei maji yana mwagika na kuharibu barabara

Uzembe mkubwa huu hatuutaki kabisa sisi


Fanya ziara Dar es salaam na ondoka na huyu MTU leta mwingine

Tumechoka


USSR
 
Maji yapo lakini hayatoi maji kabisa eneo la mbezi


Maji yanamwagika mitaani majumbani hakuna

Ukiwapigia simu wanakujibu kwa nyodo na wiki nzima hawatokei maji yana mwagika na kuharibu barabara

Uzembe mkubwa huu hatuutaki kabisa sisi


Fanya ziara Dar es salaam na ondoka na huyu MTU leta mwingine

Tumechoka


USSR
Sisi wakazi wa Mbezi Makabe tulifungiwa maji kwa gharama kubwa maji yakatoka miezi minne tena kwa kuunga unga leo yanatoka siku nne hayatoki but leo zinaenda week tano maji hamna zaidi tunanunua na vi-Canter vya wapemba na wachagha.

Ipo hujuma imefanyika hawa watu wa kuuza maji kwa magari wamekusanya pesa wakahonga engineers wa Dawasa na mkurugenzi maji yafungwe ili wao wauze maji kwa wananchi maana hai-make sense mtaa mmoja zamani tukipata maji pamoja ila ghafla leo wao wapate mpaka yanamwagika hovyo barabarani wengine kilometre moja mbele tukose.

Inakera zaidi unatumiwa bill ambayo hujui hayo maji uliyatumia lini natamani niwafate niwaambie wakang’oe takataka zao walizonifungia!
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani. DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.

Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)

DAWASCO HUDUMA KWA WATEJA 0800110064
DAWASCO ILALA 0743 451879
DAWASCO KAWE 0743 451861
DAWASCO KIBAHA 0743 451875
DAWASCO KIMARA 0743 451865
DAWASCO KINONDONI 0743 451863
DAWASCO BAGAMOYO 0743 451877
DAWASCO MAGOMENI 0743 451862
DAWASCO TEGETA 0743 451881
DAWASCO TABATA 0743 451867
DAWASCO TEMEKE 0743 451866

Punguzeni kudai bill,yani mkituma Leo kesho mnaanza kutuma msg mbilimbili za kudai,nyie ndio shirika mnaongoza kwa kudai mpaka kero
 
Meneja wa DAWASA Mkoa wa Ilala,ni lini miundo mbinu ya maji,itasogezwa karibu na wananchi wa Serikali ya mtaa Taliani karibu na shule ya Msingi Taliani ambayo inajengwa sasa hivi, kata ya Buyuni.

Miundo mbinu ya maji bado hajasogezwa karibu,japokuwa Wananchi wengi walichukua fomu za maombi ya awali January 2021.Hivi karibuni DAWASA wametandika mabomba mita chache kuelekea ilikohamia ofisi ya Serikali ya mitaa hivi sasa.

Wananchi wa Mtaa wa Taliani tunasubiri kwa hamu kusogezewa huduma miundo mbinu ili tulipie gharama za kuingiziwa maji majumbani mwetu.

Ushauri
1).Kwa kuwa gharama za vifaa kutoka inapoishia miundo mbinu ya DAWASA (mita 60) ni kubwa kwa sisi wananchi wa kipato Cha wastani.Tunashauri utaratibu wa kulipia connection fee kwa instalment 3 mpaka 6 kama walivyofanya Temeke kata ya Yombo Vituka,ufuatwe.

2). DAWASA wafanye survey kwa kila nyumba ambayo iliomba huduma ya maji na Wananchi wanaweza kuanza kulipia instalment za vifaa hivyo kuonyesha commitment yao wakati wanasubiri kupewa huduma.

3). DAWASA iwashirikishe Serikali ya mitaa na viongozi wa mashina katika, kuliendea hili

4). Serikali ya mitaa inaweza kuwadhamini wakazi wa mtaa kwao, watakao pewa huduma kwa mkopo. Maji ni uhai.
 
Yaani dawsco .. control number wamenpa nikalipa kuunganishiwa maji toka April 2022 Hadi Leo hakuna kitu ukiuliza eti vifaa hakuna
 
Hivi hamna namna ya kuwapeleka wafanyakazi wenu kwenye maeneo ya kazi kwa kutumia usafiri unaowatosha tofauti na kuwapakia kwenye pick-up wanabanana mno wafanyakazi wa kike wanapakatwa hamuoni kuwa sio poa?
 
DAWASA MNATOA MAJI KARIBU NA MWISHO WA MWEZI ILI MPATE BILL WHAT A FU.CK TUFUNGULIENI MAJI MJE MCHUKUE HELA YENU
 
Naomba kufahamu iwapo ofisi za DAWASA pale Kinyerezi zinakuwa wazi siku za Jumapili, asante
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani.

DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.

Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)

DAWASCO HUDUMA KWA WATEJA 0800110064
DAWASCO ILALA 0743 451879
DAWASCO KAWE 0743 451861
DAWASCO KIBAHA 0743 451875
DAWASCO KIMARA 0743 451865
DAWASCO KINONDONI 0743 451863
DAWASCO BAGAMOYO 0743 451877
DAWASCO MAGOMENI 0743 451862
DAWASCO TEGETA 0743 451881
DAWASCO TABATA 0743 451867
DAWASCO TEMEKE 0743 451866

Je DAWASA hamna utaratibu wa kumvumilia mteja? kwa mfano kama mteja anadaiwa na kaonyeha juhudi za kulipa angalau asilimia 75 ya bill hadi kufikia usomaji mwingine.

Apa kimara kuna watu wa DAWASA kila ikifika wakati wa usomaji wakikuta ata unadaiwa elfu 20 kati ya elfu 80 ulizotakiwa kulipa wanakata maji na wanataka uwape shilingi elfu 15 cash ili waje kufungua baada ya kulipa.

Ata kama ni faini Je, nyie hamna utaratibu wa kulipa izo fine kwa control number? Coz naona huu ni mtaji wao ndo maana wanakimbilia kukata maji coz wanajua tutawapigia na wanataka uwe na elfu 15 mkononi yaani 'nipe nikupe'.

Naomba ufafanuzi
 
Meneja wa DAWASA kibaha.sisi wateja wa Serikali ya Mtaa Mwanalugali A hatujapata maji toka Alhamisi 28Juni 2022 mpaka leo, -kuna tatizo gani?
- Kwa nini isitolewe taarifa kwa wateja wenu?

-Au ndiyo mnafanya stock taking ya vifaa vyenu na maji pia?
Pili, tarehe 01July 2022 nilitembelea ofisi za DAWASA Kibaha, kuomba huduma ya kuunganishiwa maji, lakini nimeambiwa DAWASA wamesitisha kutoa control number mpaka tarehe 20July2022 kwa kuwa wanafanya stock taking,

-hivi kweli taasisi (DAWASA) inasitisha huduma muhimu Kama hii kwa wananchi na taasisi inakosa maduhuli( kwa muda wa wiki tatu na zaidi) kwa kuwa wanafanya stock taking,?

-hapa siyo kwamba Kuna hujuma Serikali ya awamu ya sita ambayo imelipa fedha za kujenga miundo mbinu ya maji.

Ushauri
1). DAWASA iwe inatoa taarifa ya ukatikaji wa maji kwa wateja wao,pindi wanapofanya matengenezo ya kawaida au dharura.

2). DAWASA, iendelee na kukusanya maduhuli sambamba na kufanya stock taking.

3).Stock taking ichukue wiki moja au mbili badala ya kuchukua wiki tatu au nne(ni inefficiency,)

4). vifaa vyote viingizwe kwenye computer(Computerized inventory Management system) ili kusaidia manejiment kujua status ya kila wiki au mwezi ya stock position na ile physical stock taking ni kufanya verification ya figure tu.

5). Waziri mwenye dhamana na maji,tafadhali ingilia kati urasimu na inefficiency ya DAWASA, Serikali imetumia mabilioni ya mikopo au misaada toka kwa wahisani,ambayo inabidi kulipwa

6). Waziri wa maji msaidie Mama Samia kwenye kampeni yake ya kumtua mama ndoo kichwani Kwa kuboresha huduma kwa wateja na utunzaji wa miundo mbinu ya maji.

7). Mtendaji Mkuu wa DAWASA na wafanyakazi wote wa DAWASA simamieni vema miundo mbinu ya maji na ukusanyaji wa maduhuli ili kulipa madeni yaliyokopwa nje.
 
DAWASA mtaa wa Mwananchi ulipo tabata, Wilaya ya Ilala kuna tatizo toka Majuzi, Maji yamekatika na hakuna dalili ya kurudi na inavyosemekana kuna mahali bomba limepasuka hivyo kupelekea maji kumwagika tu.
 
jamani ingawa kuna watu hawapendi kulinganisha tawala
ukweli unaonekana

sasa hivi wanakata mtaani bila hata taarifa na mnaweza kukaa wiki na zaidi

halafu yanakuja kutoka usiku saa tano

Mama yenu ana kazi ya ziada
 
Back
Top Bottom