DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Habari, naona upo online. Mie ni mnifaika wa maji ya mkopo Kibamba. Toka nimefungiwa yale maji sijapewa invoice yoyote ya kuomyesha ni kiasi gani nadaiwa. Mmeanza kunitumia bili mwezi wa pili mwaka huu. Nahitaji kulipa ila niko nje ya mkoa, naomba muongozo
 
Hivi humu kuna msaada Kweli? Maana naona watu wanauliza ila sioni majibu.
Wasoma meter na wakata maji wa DAWASA hivi wana kiwango gani cha elimu. Maana ni wabishi na wasiotaka kuelewa. Mfano wamekata maji na kutoa notification ambapo bill ya notification ilishalipwa. Sasa waje kurudisha maji, wamekuja wamerudisha maji sasa pale walipofunga kwa kukunja panavuja, wanakuambia funga na mpira wewe mteja wakati wao ndio wameharibu. Naomba kujua kiwango cha elimu cha watu hawa.
 
DAWASCO AU DAWASA SISI HAPA KIMANGA KARIBU NA CLUB YA WAZEE KUNA BOMBA LINAMWAGA MAJI ZAIDI MIEZI 3.TUMEWAJULISHA MARA NYINGI HAKUNA KILICHOFANYIKA?AU KWAKUWA MAJI MNAYAPATA BURE RUVU?SISI BARABARA ZETU ZINAHARIBIKA.MBONA KUKATA MAJI MNAKUJA FASTER?
 
Dawasa mnakera
Nimepeleka maombi ya kufungiwa maji
Mwezi wa pili huu
Kuja kufanyiwa tathimini tu nishakuja ofisini kwenu tabata mara 3
Ofisi za serikali urasimu mwingi...kila siku saundi tu...hapo ni utathimini tu....daah
 
Goba njia nne upande wa kuja matosa lini tutapata maji tunateseka sana tunauziwa maji unit 1 elfu 13000/= tusaidieni na sisi
 
Yaani kama kuna kitengo kinafanya kazi KIPUMBAVU NA KIPUUZI ni hiki chenu, SINZA mmekata maji Leo siku ya pili sababu ni watu baadhi kutolipa maji kwa wakati, SWALI: wale waliolipa kwa wakati why wapate kadhia ya maji na waunganishwe kwenye kosa lisilo Lao?. Kama mmeona njia ya kutoa meter haifai basi tafuteni namna nyingine na si njia hii ya kukata maji KIPUMBAVU.
 
Eneo la (Mivumoni) pamoja na Madale limepimwa na Municipal toka 2007 ila Maji huku ni Mtihani Ujenzi wa Tank kuuubwa maeneo ya Bwawani Wazo Hill UMEKAMILIKA ... KONGOLE KWENU... Ila naona bado mnasuasua kuunganisha wateja tatizo ni nini? Uchaguzi wa Serikali za Mitaa au Uchaguzi Mkuu?
 
Dawasa haka katia kenu katosoma mita ya mteja na kuanza kumkadiria mtu matumizi ni UJINGA tena nawashauri muachemnaweza kuua watu kwa presha maisha ni magumu sana sasa iv. EBOOOOOO
 
Inakuaje wajenzi wa barabara wanakata miundo mbinu yenu hamuwachukulii hatua kurejesha mapema iwezekanavyo na bado mnawapelekea madai ya malipo wateja wenu?
 
Dawasco kulikoni leo siku ya 3 Mbezi hatupati maji. Isingekuwa hii mvua hali sijui ingekuwaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…