DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Maji ni uhai na kukosa Maji ni hatari kutokana na umuhimu wake ...
Ubungo Riverside mbele ya landmark kuelekea external ... Ni wiki na zaidi tunataabika na kukosa huduma ya Maji ...
 
Auwsa Arusha urban water supply.mnafunga maji bila mita .mita baada ya wiki badilisheni mfumo .fungeni mita unganisha maji kwa wakati mmoja .
 
DAWASA (DAWASCO) ni lini Maji yatafika Mbezi Makabe?? Yaan naona kama tumesahaulika, jamani na sisi tunayahitaji maji kuliko kitu kingine chochote. Maji ni uhai jamani.
 
Mimi ni mwananchi wa Kata ya Msigani wilaya ya Ubungo, Nimejaribu mara kadhaa kipitia Twitter kuwasiliana na nyinyi lkini majibu hua sipatagi, now mnimbie huu mradi wenu wa maji ambao unaendelea kwa kusua sua ni lini haswa tutaanza kuyapata maji majumbani mwetu, adha ya maji kwa upande huu ni kubwa mno, dumu moja la lita elfu moja ni shs elfu kumi na tano

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kulikuwa na matatizo madogo madogo ila sasa tumerudi rasmi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bagamoyo Makurunge maji yanafika lini???
 
TUNASHUKURU KUWA DAWASA MMERUDI NA KUANZA KUJIBU HOJA ZETU KWANI MAJI NI UHAI. NAOMBA KUFAHAMU TENKI LINALOJENGWA TABATA MAGOZA LITAFUNGULIWA LINI NA LITAPUNGUZA SHIDA YA MAJI KATIKA MAENEO GANI?
 
Mwezi sio tarehe moja hadi 30 ni kuanzia tarehe yoyote ili mwezi utimie!
 
Kwenu DAWASA bado sijapata mrejesho wa tenki linalojengwa Tabata Magoza.
TUNASHUKURU KUWA DAWASA MMERUDI NA KUANZA KUJIBU HOJA ZETU KWANI MAJI NI UHAI. NAOMBA KUFAHAMU TENKI LINALOJENGWA TABATA MAGOZA LITAFUNGULIWA LINI NA LITAPUNGUZA SHIDA YA MAJI KATIKA MAENEO GANI?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…