DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Maji ni uhai na kukosa Maji ni hatari kutokana na umuhimu wake ...
Ubungo Riverside mbele ya landmark kuelekea external ... Ni wiki na zaidi tunataabika na kukosa huduma ya Maji ...
 
Auwsa Arusha urban water supply.mnafunga maji bila mita .mita baada ya wiki badilisheni mfumo .fungeni mita unganisha maji kwa wakati mmoja .
 
DAWASA (DAWASCO) ni lini Maji yatafika Mbezi Makabe?? Yaan naona kama tumesahaulika, jamani na sisi tunayahitaji maji kuliko kitu kingine chochote. Maji ni uhai jamani.
 
Mimi ni mwananchi wa Kata ya Msigani wilaya ya Ubungo, Nimejaribu mara kadhaa kipitia Twitter kuwasiliana na nyinyi lkini majibu hua sipatagi, now mnimbie huu mradi wenu wa maji ambao unaendelea kwa kusua sua ni lini haswa tutaanza kuyapata maji majumbani mwetu, adha ya maji kwa upande huu ni kubwa mno, dumu moja la lita elfu moja ni shs elfu kumi na tano

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TANGU HUU UZI UMEFUNGULIWA NAKUTA TU KERO, MALALAMIKO, LAWAMA TAARIFA ZA MABOMBA KUPASUKA SEHEMU MBALI MBALI NA KADHIA MBALIMBALI LAKINI SIJAWAHI KUONA MAJIBU HATA MARA MOJA. HIVI HUU UZI ULIFUNGULIWA NA DAWASCO/DAWASA WENYEWE AU NI WATU FULANI TU WALIJISIKIA TU KUFUNGUA UZI KWA KUTUMIA JINA LA DAWASCO/DAWASA?

NI MUDA MUAFAKA SASA HUU UZI KAMA HAUJAFUNGULIWA OFFICIALY NA DAWASCO/DAWASA BASI UFUNGWE/UFUTWE TU KWA SABABU WATEJA WANAWEZA KUACHA KUPELEKA MALALAMIKO SEHEMU HUSIKA WAKAYALETA KWENYE HUU UZI WAKITEGEMEA ZITAWAFIKIA DAWASCO/DAWASA NA KUFANYIWA KAZI WAKATI HAYAFIKI SEHEMU HUSIKA NA KWA WAKATI. MATOKEO YAKE MPAKA TAARIFA ZIFIKE SEHEMU HUSIKA INAWEZEKANA KAMA NI MADHARA YAMETOKEA MAHALI YANAWEZA KUWA HAYAWEZI KUREKEBISHIKA TENA.

MWISHO NAMSHAURI MHESHIMIWA LUHEMEJA ATUSAIDIE WANANCHI WA DAR TUPELEKE WAPI KERO ZETU KWANI CUSTOMER CARE NUMBER HUWA ZINAIITA HATA SIKU NZIMA HAKUNA MPOKEAJI SIO ZA MAKAO MAKUU AU ZA HUKU TABATA. KWA MFANO SIKU CHACHE ZILIZOPITA KULIKUWA NA TAARIFA YA UHABA WA MAJI BAADA YA KUPASUKA BOMBA LINALOTOKA RUVU. LAKINI BAADA YA HAPO HAKUNA UPDATE NA WATU HATUNA MAJI WIKI SASA MABOMBA YAMEBAKIA MAPAMBO NA HATUJUI MAJI YANARUDI LINI.
Kulikuwa na matatizo madogo madogo ila sasa tumerudi rasmi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani. DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.

Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)

DAWASCO HUDUMA KWA WATEJA 0800110064
DAWASCO ILALA 0743 451879
DAWASCO KAWE 0743 451861
DAWASCO KIBAHA 0743 451875
DAWASCO KIMARA 0743 451865
DAWASCO KINONDONI 0743 451863
DAWASCO BAGAMOYO 0743 451877
DAWASCO MAGOMENI 0743 451862
DAWASCO TEGETA 0743 451881
DAWASCO TABATA 0743 451867
DAWASCO TEMEKE 0743 451866View attachment 721128
Bagamoyo Makurunge maji yanafika lini???
 
TUNASHUKURU KUWA DAWASA MMERUDI NA KUANZA KUJIBU HOJA ZETU KWANI MAJI NI UHAI. NAOMBA KUFAHAMU TENKI LINALOJENGWA TABATA MAGOZA LITAFUNGULIWA LINI NA LITAPUNGUZA SHIDA YA MAJI KATIKA MAENEO GANI?
 
Kwenu DAWASA bado sijapata mrejesho wa tenki linalojengwa Tabata Magoza.
TUNASHUKURU KUWA DAWASA MMERUDI NA KUANZA KUJIBU HOJA ZETU KWANI MAJI NI UHAI. NAOMBA KUFAHAMU TENKI LINALOJENGWA TABATA MAGOZA LITAFUNGULIWA LINI NA LITAPUNGUZA SHIDA YA MAJI KATIKA MAENEO GANI?
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom