DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani. DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.

Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)
Lini mnaleta maji mbezi msigani maana kila cku tunajaza form mara mko kwenye upembuzi hadi kero na hata majibu yenu yanakatisha tamaa. pitia na hapa Serikali: Tatizo la Maji Dar mwisho 2017
 
DAWASCO nawapongeza sana kwa kufungua ID hapa JF naomba msikilize kero zetu na kuzitatua, wenzenu TANESCO wanajitahidi sana
 
Bomba zenu zikipasuka, ni jukumu la raia au lenu kuja kuzirekebisha? Kuna baadhi ya bomba zenu zinakuwa zimepasuka na zinavuja sana ila unaweza ziona kwa karibu mwezi na zaidi hazirekebishwi licha ya mleta bili wa dawasco ambaye natumai ni mfanyakazi wenu kusisitizwa awasilishe taarifa. Mipasuko hiyo inasababisha shinikizo dogo la maji kutoka ktk mabomba.
 
mabibo jeshini kuna mibomba imepasuka inamwaga maji kama ruvu vile;hivi wahudumu wenu wanaosoma mita huwaga hawaoni wakaleta taarifa au ndio mnafanya kazi kwa mazoea kama enzi zile!,kwanini mnapokuja kuwaunganishia wateja maji hamchimbii sana chini kama ule mhimili uliojichimbia chini zaidi ya mingine ili yasipasuliwe kwa kukanyagwa?.Hivi hili shirika linatatizo gani?,maji mengi sana yanapotea huku mjini wakati wanao ishi hapo mbezi msakuzi mnawafanyia mradi wa maji ya canter.
 
kwa upande wa hapo mabibo makuburi bomba limepasuka na hatua zimechukuliwa kuthibiti maji yanayopotea. bomba la ukubwa wa inch 4 limepasuka likiwa chini ya barabara ya lami na Dawasco tumeomba kibali toka Tanroad ili tuweze kukata kipande kile cha lami ili matengenezo yaweze kufanyika.
tunashukuru kwa taarifa
 
Bomba zenu zikipasuka, ni jukumu la raia au lenu kuja kuzirekebisha? Kuna baadhi ya bomba zenu zinakuwa zimepasuka na zinavuja sana ila unaweza ziona kwa karibu mwezi na zaidi hazirekebishwi licha ya mleta bili wa dawasco ambaye natumai ni mfanyakazi wenu kusisitizwa awasilishe taarifa. Mipasuko hiyo inasababisha shinikizo dogo la maji kutoka ktk mabomba.
tafadhali tunaomba kujua eneo linalovuja ili team yetu iweze kufika kwa wakati
 
Kunduchi mtongani pia kuna bomba lenu limepasuka. Maeneo ya karibu na kota za polisi ila ukitokea mtongani kwenyewe ile barabara ya mikokoni ambako gari haIpiti kuelekea kota za polisi kuna bomba lenu linavuja sana.
 
kwa upande wa hapo mabibo makuburi bomba limepasuka na hatua zimechukuliwa kuthibiti maji yanayopotea. bomba la ukubwa wa inch 4 limepasuka likiwa chini ya barabara ya lami na Dawasco tumeomba kibali toka Tanroad ili tuweze kukata kipande kile cha lami ili matengenezo yaweze kufanyika.
tunashukuru kwa taarifa
Sio kule makuburi mkuu,nendeni mpaka pale msikitini karibia na Loloya high school muingie kule kota za jeshi za zamani karibia na kwa wakurya maeneo hayo mtayaona hayo mabomba yapo barabarani,note: muende maji yakiwa yamefunguliwa.
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani. DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.

Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)
Jaribuni kupitia Tena taratibu za Malipo ya Huduma zenuza Maji. Mfano mimi binafsi nina nyumba na majengo ya biashara mnanitumia message ya kulipia maji tarehe 5 friday May 2017 mnanitumia ya kulipa bili ya Maji ya Mwezi May na vitisho juu kuwa mtakata maji.

Kwanini hizi message msiwe mnatuma kuanzia tarehe 20 ya kila mwezi na window period ya kulipia iwe tarehe 27 ya kila mwezi hapo wengi wanakuwa wamepata mishahara yao na kuweza kucover hizo cost za maji.

Imefikia kipindi hizi kero za kutoka kwa wasoma mita wetu zinatufanya kufikiria kuchimba visima kwa sisi wafanyabiashara badilikeni. Huyo aliyewapa hiyo strategy hafai kabisa
 
ndugu Dan..bili zinatolewa pindi tu mita yako inaposomwa na msoma mita wetu. inawezekana kupata bili yako hata tarehe 1 na kuendelea kutokana na usomaji mita. jinsi unavyosomewa mita ndivyo utakavyopokea bili yako. ukisomewa bili yako Leo utapokea bili yako kwenye simu kesho yake
 
Swala langu ni kuwa. Kwanini mnalazimisha watu kulipa bili kabla hata ya Tarehe 25 kufika?

Bili ikitoka tarehe 5 huyo msoma mita anakufuata na vitisho kibao kukata maji hii sio haki. Kwa mwezi mmoja napokea simu za wasoma mita zaidi ya 8 ambao wanasoma mita kwenye assets zangu tofauti. Ni vitisho na kelele.

Atleast basi hizo message hata kama zitakuja mwanzo wa mwezi au katikati ya mwezi iweke deadline ya kufanya malipo ili tusumbuliwe baada ya huo muda kupita.

Mfano ukinitumia bili ya maji then iandike before tarehe fulani uwe umeshafanya malipo kuliko ilivyo sasa. Mnawapa mwanya wasoma mita kuchukua rushwa kwasababu inabidi umpoze ili asikate maji mpaka karibu na mwisho wa mwezi ufike watu tufanye malipo
 
tutajie eneo husika. maelezo yako bado hayajajitosheleza
MBEZI/ MOROGORO ROAD
WATER.jpg
 
Swala langu ni kuwa. Kwanini mnalazimisha watu kulipa bili kabla hata ya Tarehe 25 kufika?

Bili ikitoka tarehe 5 huyo msoma mita anakufuata na vitisho kibao kukata maji hii sio haki. Kwa mwezi mmoja napokea simu za wasoma mita zaidi ya 8 ambao wanasoma mita kwenye assets zangu tofauti. Ni vitisho na kelele.

Atleast basi hizo message hata kama zitakuja mwanzo wa mwezi au katikati ya mwezi iweke deadline ya kufanya malipo ili tusumbuliwe baada ya huo muda kupita.

Mfano ukinitumia bili ya maji then iandike before tarehe fulani uwe umeshafanya malipo kuliko ilivyo sasa. Mnawapa mwanya wasoma mita kuchukua rushwa kwasababu inabidi umpoze ili asikate maji mpaka karibu na mwisho wa mwezi ufike watu tufanye malipo
unatakiwa kulipa bili yako ndani ya siku 7 tangu kutumiwa kwenye simu yako. ni haki yako kumwambia msoma mita juu ya sheria inayokulinda mteja kulipa Maji ndani ya siku 7. msoma mita ataweza kukusumbua kulipa iwapo utakuwa umepitiliza muda uliopangwa. na kumbuka ukisitishiwa huduma ya Maji itakubidi kulipa Tsh 30,000/= kama gharama ya kuja kurudishiwa huduma iliyositishwa
 
kwahiyo kama imetoka tarehe 3 May then tarehe 10 May niwe nimelipa? Hawa wateja mnaowafikiria ni wafanyabiashara pekee au ni wafanyakazi wa maofisini ambao wanategemea mishahara ya mwisho wa mwezi? Hamko serious kabisa.

Hiyo mnayofanya ni kupoteza wateja. Jaribu kupitia tena hizo taratibu zenu. Ndio maana mmebaki na wateja wa mjini tu na maeneo ya karibu ya mji. Kwa huu usumbufu wenu acha tuhamie kwenye Visima
 
kwahiyo kama imetoka tarehe 3 May then tarehe 10 May niwe nimelipa? Hawa wateja mnaowafikiria ni wafanyabiashara pekee au ni wafanyakazi wa maofisini? Hamko serious kabisa.

Hiyo mnayofanya ni kupoteza wateja. Jaribu kupitia tena hizo taratibu zenu. Ndio maana mmebaki na wateja wa mjini tu na maeneo ya karibu ya mji. Kwa huu usumbufu wenu acha tuhamie kwenye Visima
ndugu mteja mbona bili nyingine mnalipa kwa wakati ?kwanini bili ya Maji inakuwa na malalamiko mengi. tafadhali kama unatumia Maji jitahidi kuyalipia kwa wakati. Maji ni uhai
 
Back
Top Bottom