mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,076
- 4,113
Ni mambo ya ajabu sana huku tulipofikishana. Septemba 21 mwaka huu DAWASA iliuhakikishia umma wa Tabata kuwa kutakuwa na uhakika wa maji, lakini mpaka leo navyopandisha mnakasha huu kuna baadhi ya mitaa maji kwetu yamebaki kuwa ndoto.
Hata kama ni mgao, ndio wiki nne na zaidi? Hapana kwakweli tumevumilia tumechoka, tunaomba maji na sisi tufurahie kama wengine.
Mbunge wetu Bonnah Kamoli tuliyempitisha kwa kura za kutosha naona hana msaada kabisa kwetu japokuwa anaishi Bonyokwa.
Mvua zinazoendelea nchini nilitegemea zipunguze shida ya maji kwa asilimia kubwa, lakini inaonesha DAWASA bado hawajajipanga na wanafanya kazi kwa mazoea.
Sisi wakazi wa Bonyokwa, mtaa wa Shedaffa na mitaa jirani tunaomba mtufungulie maji nasi tufurahie maisha, kama ninyi mnavyofurahia kututumia bill kubwa kwa huduma ambayo mnatunyima kwa asilimia 80.
Pia soma > DAWASA, Segerea kuna mgao wa maji kimyakimya? Wiki ya pili mitaani hakuna maji!
Asanteni kwa kunisikiliza.
UPDATES:
- Dar: DAWASA imeanza kutekeleza kazi ya kufunga kifaa cha kusukuma maji kwenda Bonyokwa