Tatizo sugu la maji Tabata, kila mara tunapewa ahadi za tatizo kuisha lakini hali ni ile ile!

SIMU YA TOCHI

JF-Expert Member
Dec 12, 2014
1,384
892
Kwa hali ya kusikitisha maeneo mengi sana ya Tabata yamekumbwa na tatizo la maji, ni zaidi ya mwaka lakini DAWASA imekuwa ikitoa majibu yaleyale kwamba watu wawe wavumilivu huduma itarejea.

Wito waziri afike ajionee msoto wananchi wanaopitia, kuanzia Tabata maeneo ya viwanja vya benki, Segerea kwa mzee Adamu, Segerea Mzimuni, Segerea Migombani, Bonyokwa na maeneo mengine mengi.
 
Waziri ameanza ziara ya kuuza sura hapa mjini kuhusu maji, huenda hayo maigizo yakaleta maji siku 2 tatu hizi.
 
jana wamepita mitani maeneo ya kinyerezi eti wanaauliza wananchi kuhusu shida ya maji mara wanasema eti mnapataga majiyenye chumvi walichowaambia ni bora hata hayo ya chumvi yangetoka hakuna maji kabisa hawana hata aibu hawa watu
 
Huku kwetu kimara stop over michungwani kuna ujinga unafanyika nashundwa kuelewa,Maji yanatoka mtaa wanyuma na mtaa wa pili mbele...ila sisi tuliokaa huku kati maji hayatoki tuna miezi4 sasa....na Dawasco wanakuja kusoma mita ambazo hazitoi maji.
 
Bill zinakuja na bei gani mkuu?
 
Back
Top Bottom