Mbunge Ameir Abdallah: Tafiti zipi Taasisi za 'Tiba Asili' Zimekamilisha na Kuwa Suluhisho la Maradhi Kama Tiba Mbadala?

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942

Mbunge Ameir Abdallah: Tafiti zipi Taasisi za 'Tiba Asili' Zimekamilisha na Kuwa Suluhisho la Maradhi Kama Tiba Mbadala?

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amewataka wasomi nchini kubadili fikra zao kwa kutumia akili vumbuzi na sio akili kibarua ili kulisaidia taifa kusonga mbele kwa maendeleo

Dkt. Mollel amesema hayo, Alhamisi Februari 15.2024 jijini Dodoma wakati akijibu swali namba 223 kwa niaba ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu lililoulizwa na Mbunge kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar Ameir Abdallah Ameir aliyeuliza ni tafiti zipi ambazo taasisi za 'Tiba Asili' zimekamilisha na kuweza kuwa suluhisho la maradhi mbalimbali kama tiba mbadala?

Akijibu swali hilo Dkt. Mollel amesema kuwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2021 hadi 2024 zaidi ya tafiti 50 zimefanyika ndani ya nchi juu ya ubora na usalama wa dawa zinazotumika kwa tiba asilia kwa kupitia taasisi ya Taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR)

Ameongeza kuwa baadhi ya tafiti hizo ni pamoja na utafiti wa dawa ya Saratani ya NIMREGENIN, dawa ya TANGHESHA inayotibu Selimundu, dawa ya PERVIVIN inayotibu tezi dume, dawa ya WARBUGISTAT inayotibu magonjwa nyemelezi na dawa ya NIMRICAF inayotibu mfumo wa upumuaji

Aidha Dkt. Mollel ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanatunza miti inayotumika kutengeneza dawa za tiba asili ili kuendelea kuzalisha dawa za tiba asili za kutosha nchini
 

Attachments

  • WhatsApp-Image-2024-02-12-at-8.09.39-AM.jpeg
    WhatsApp-Image-2024-02-12-at-8.09.39-AM.jpeg
    214.3 KB · Views: 1
  • 1AAA-1-1024x682.jpg
    1AAA-1-1024x682.jpg
    84.2 KB · Views: 1
  • GGX4j03WYAAUc_K.jpg
    GGX4j03WYAAUc_K.jpg
    495 KB · Views: 1
Ttz vibari vya kuuza dawa wanagawa ovyo ili linasababisha wasio waanifu nao kutuuzia mizizi feki.
 
Back
Top Bottom