Sio kosa Mara mojamoja kumpakia Mkeo Mundende au Vumbi La kongo

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,895
SIO KOSA MARA MOJAMOJA KUMPAKIA MKEO MUNDENDE AU VUMBI LA KONGO.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Angalizo, Asome mwenye umri kuanzia miaka 18. Na yeyote mwenye mke, na yeyeto anayetarajia Kuwa na Mke(Kuoa).

Mambo haya ni yafaragha, nafahamu wapo maelfu ya vijana ambao hawana wazazi au walezi wa kuwaambia mambo haya. Na wale wenye hao walezi au wazazi huenda kwa namna moja au nyingine wanaweza wasiwaambie baadhi ya ishu kama hizi. Lakini mimi Mtibeli, kutoka nyota ya Tibeli, Kuhani katika Hekula Jeusi nitachukua muda wangu huu mdogo kuwasaidia.

Kila jambo duniani ni jema likitumika kwa dhamiri iliyonjema. Na kila jambo duniani ni baya lilitumika kwa nia mbaya. Watibeli hatuangalii matendo ya mtu lakini tunaangalia NIA ndio hiyo DHAMIRI ya mtu kwa yale ayafanyayo.

Sio dhambi wala kosa kumpakia Mkongo au mundende Mkeo uliyemuoa, unayempenda, mama watoto wako mara mojamoja.

Usitumie mara kwa mara kwa sababu ni dawa. Dawa hutumika kwa dharura au kwa muda fulani mahususi. Dawa ukiitumia mara kwa mara huwa na madhara. Maelekezo ya kutumia dawa ni muhimu kuliko dawa yenyewe kwa sisi madaktari tunawaambia haya wateja wetu.

Mpakie Mkongo mkeo.
Mpakie Mkongo shemeji yetu.
Mfurahishe! Mfanye ajihisi Furaha. Usiwe mjinga. Wewe ni mwanaume. Uliambiwa utawale dunia na sio dunia ikutawale. Oooh! Shauri yako.

Utafiti wangu unaonyesha kuwa wanaume wengi hutumia mbinu za kimedani hasa ya kuongeza uwezo wa kuzagamua pale wanapocheza mechi za nje na michepuko.
Haipo hivyo.

Kwa Watibeli ni bora tutumie Mbinu hizo za kimedani kwa mke kuliko Nje.
Tunalinda ndani, tunalinda ngome, tunalinda Ikulu kuliko kwa jirani.

Huwezi ipata heshima kwa jirani, mchepuko. Itakuwa heshima ya muda tuu.
Heshima mtu huipata ndani ya nyumba yake. Wanasema mcheza kwao hutunzwa.

Nafahamu kuna ile dhana kwamba mke wangu akijua ninatumia mbinu hizi za kimedani huenda atanidharau. Au akiona performance yako umefanya kwa kiwango cha juu atahisi kuna namna haipo sawa.

Sikiliza ndugu yangu, wewe ni mwanaume. Túmia akili, tumia mdomo wako kumuweka sawa.
Unaweza kumwambia kuwa kuna namna ukimwona unahisi mwili wako unashikiwa na nguvu kama za Samsoni. Hasa ukiyatazama macho na vile mwili wake unavyotetema, msifie. Mwanamke anapenda sifa kuliko hata Kula chakula.
Kama vile sisi wanaume tunavyopenda kuheshimiwa.

Kikawaida mechi kubwa zisiwe kila siku zikazoeleka. Ndio maana nikakuambia mara mojamoja walau mara moja kwa mwezi. Unapiga kombora ambalo litasambaratisha kiu yake yote.

Sio dhambi! Wala sio kosa kutumia Mbinu za kimedani kwa Mkeo. Kwanza mbinu hizo ndio zipo mahususi kwaajili ya Watu wapendanao.
Hutaki kumkunjua mkeo akakunjuka? Hutaki mkeo akajihisi Mwanamke na amepata dume linalokamia.

Sio unafanya yololololo! Yololololo! Unapiga kimoja hata dakika tatu hazijafika hivi hata wewe utakuwa umeenjoy kweli? Haya mambo najua hatupendi kuyazungumzia lakini yanawapa Watu tabu. Wanawake wanateseka kwani hawafurahii viungo vyao vya siri wakiwa ndoani na wanaume nasi tumejikatia tamaa.

Hakikisha mnakuwa na mawasiliano ya karibu. Hakikisha hakuna mwenye ubinafsi kati yenu mkiwa mchezoni. Hakikisha umesoma code na unadecode na encoding taarifa zote katika mwili wa mwenzako. Kamia mechi lakini wote mkiwa mchezoni.

Ukimpa mkeo uhuru mchezoni acheze kama Kahaba ndio utafurahia ndoa yako. Nawe ucheze kama mhuni wa filamu za pono. Nia ikiwa kila mmoja afurahie.

Kwenye dimba, Usilete mazoea, usilete uchungaji au usheikhe.

Taikon nimemaliza.

Nawatakia maandalizi mema ya Sabato.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Aah sasa unamlambisha asali af unapotea unarudi kimoja chali, unatafuta nini ?

Na izo mara moja ziishie front tu

Mwanamke ukiweza kumridhisha vizuri walau mara moja kwa mwezi inatosha kabisa.
Kwa sababu wao kwenye siku 30 za mwezi wanakuwa na hamu katika siku 6 tuu.
Hizo nyingine itategemea na anavyokuona wewe au jinsi unavyomfanyia
 
Back
Top Bottom