CUF hawana mbunge hata mmoja TZ bara wote hao wanatoka zanzibar!!
Chukua mfano ungekuwa ni mwanasiasa ambaye huna chama kwa mfano lakini unauwezo mzuri wa kuongoza na kushawishi. Sasa tutakupa kazi ya uenezi wa chama, Tukikuambia uchague unataka tukupe uenezi utachagua lipi kati ya haya.
1. Kuitangaza na kuijengea image nzuri CUF Tanzania bara na tutakupima kwa idadi ya wanachama utakao wasajili na idadi ya washindi wa nafasi za kisiasa kwenye duru mbali mbali za uchaguzi.
2. Kuitangaza na kuipa kuikuza CHADEMA Tanzania Visiwani na utapimwa kwa usajili wa wanachama na idadi ya washindi wa viti mbali mbali wakati wa chaguzi
Pia ndugu yangu naomba nikuambie, wengi walimpinga mzee mwanakijiji kwenye ile thread aliyouliza CHADEMA wamefanya nini kuaminiwa kushika dola, wapingaji wakasema wafanye nini wakiwa Chama cha upinzani? wao walidhani mwanakijiji anauliza kama wamefanya kazi za ujenzi wa barabara, umeme, miradi ya maji, kilimo nk.
Wengine tunaona tofauti, tulimuelewa Mzee mwanakijiji tofauti, Chama cha upinzani kinapimwa kwa msukumo na mbinyo kinaotoa kwa serikali kutekeleza majukumu ambayo serikali inapaswa kuyafanya kwa wanachi wake. Kwa mfano kama CHADEMA wangekuwa na wabunge wengi bungeni leo hii hoja ya EPA ambayo waliasisi ingekuwa ilishafungwa siku nyingi. Na hili ndilo wanachi tungewapima nalo. Sasa hivi wao na ajenda yao ya ufisadi imekosa ufanisi wa kuwapimia na matokeo yake Anna kilango, Selelii, Mwakyembe wanachukua Credit kwa hiyo.
Kama CHADEMA wangekuwa na wabunge wakutosha bungeni, leo hii suala la Richomnd isingekuwa ajenda ya CCM ana kamati za Mwinyi, ingekuwa ni ajenda ya watanzania, Leo hii tungekuwa tunajua kwa uhakika huduma za shirika la reli zinamwelekeo gani, na kama wenzetu wa kanda ya ziwa watasafiri krismass kwenda nyumbani kwa usafiri wa uhakika?
CHADEMA wanapaswa kuwa na mkakati wa makusudi wa kushika dola, hata ndani ya baraza la mawaziri kuna kutofautiana, kama Rais atakuwa wakati wote analazimisha hoja zake zipite bila kujali hoja za mawaziri wake basi serikali hiyo itakuwa ya "one man show" na matokeo yake Rais ansimamishwa barabarani kwasababu wanachi wanataka matuta kwenye bara bara kuzuia magari yasiende kasi, kitu ambacho hata mwenyekiti wa kitongoji angeweza kukimaliza.
CHADEMA lazima wakubali it was not a right time to make a move they made, CHAMA kitatulia hakutakuwa na choko choko kama kilivyokuwa kimetulia wakati wa uenyekiti wa Edwin Mtei, wakati wa Bob Makani lakini je kitafika nchi ya ahadi (Kuongoza dola)