David Kafulila ajivua uanachama CHADEMA

Status
Not open for further replies.

Heshima kwako Mwafrika.

Naona povu linakutoka kwa kushabikia ujinga na unafiki wa CHADEMA.Taratibu kaka / dada kuna watu wasiopenda kuburuzwa na siasa za hila ambazo CHADEMA wamekuwa wakizifanya.Ni nani asiojuwa Kafulila katoswa kwasababu alikuwa akimuunga mkono Mheshimiwa Zitto,kama si unafiki ni nini au unafikiri ni rahisi kutuhadaa na hizo propaganda zenu za kitoto.

Mkuu Ngongo Heshima Mbele

Ni kweli kwamba Kafulila na Wengi tu akina Msafiri walikuwa wanamuunga mkono Zitto na inawezekana kabisa hakufurahishwa na Uamuzi wa Zitto kukubaliana na Ushauri wa Wazee!

Lakini baada ya Uchaguzi Makundi yanavunjwa ili Chama kisonge mbele, sasa inaonekana kuna Baadhi ya Watu bado wana Kinyongo kile cha kwa nini Zitto alijitoa ( Zitto alisema kitu kimoja kwamba baada ya uchaguzi yeye na Mbowe watakuwa kitu kimoja ila akawaonya Wapambe Nuksi), Nadhani akina Kafulila walifikiri maneno haya Zitto alikuwa anayaelekeza kwa wale waliokuwa wanamuunga mkono Mbowe kumbe ilikuwa ni kwa Pande zote.

Sasa uchaguzi umeisha Zitto kavunja Makundi lakini wapambe nuksi hawakubalini, sasa wanatumia kila namna kuwachonganisha Zitto na Viongozi wenzake ionekane kuna Mpango wa kumng'oa Zitto, sasa baada ya kukosa uungwaji mkono ulitaka wafanye nini sasa! Ni kujitoa kwa aibu tu
 
Kaka/Dada Ngongo,

Mimi ni mmoja wa watu wasiojuwa kuwa Kafulila kafukuzwa kwa sababu ulizozitaja hapo. Naona wewe ndio mapovu yanazidi kutoka huku ukitaka watu wote wakubaliane nawe kuwa kafulila kafukuzwa kwa ajili ya Zitto - kitu ambacho nina hakika kuwa Zitto atakipinga hapa muda si mrefu.
Mwafrika.

acha ujinga hivi na wewe uko kwenye hiyo NGO ya kina Ndesamburo,Mtei,Mbowe ?.Nilidhani una akili kumbe tayari virusi vya upumbavi vimeshakuvamia.Chadema si chama cha siasa Kafulila kagundua ingawa kachelewa sana bora aende CUF,NCCR au TLP hivi ni vyama vya siasa makini si chadema hata kidogo.

Hata ningekuwa mimi Kafulila ningejitoa tu, Yaani napanda Mbegu za Chuki halafu siungwi mkono come on
 
Hakuna kaogopa SULULU unafikiri sululu mchezo wewe!!

Unajua mkuu ilikuwa hivi!

Mwandishi Mtanzania: Unajua kuwa Viongozi wako wanafanya mkutano Dom wa kukung'oa?

Kafulila: Aah, mimi mbona sifahamu hizo habari, hebu nipe ishu mkuu

Mwandishi Mtanzania: Ndiyo hivyo mkuu, Wamekaa Mbowe, Slaa, Mdee nk wanajdili kukung'oa wewe, Jandu na ( ili kumtia hasira Kafulila na Kumconnect na Zitto) mama yake Zitto

Kafulila ( Bila kupima): Dah mi sina habari mkuu hicho kitakuwa ni Kikaao cha Gheto

Mwandishi Mtanzania akakata simu kecho kwenye Front Page

Bundi Lainyemela Chadema

1: Kikao chafanyika kuwang'oa wafuasi wa Zitto
2: Kiliendeshwa kwa Siri
3: Yeye Kafulila asema ni kikao cha Gheto

Sasa wewe ungekuwa Dr. Slaa ungefanyaje
 
Mwafrika.

acha ujinga hivi na wewe uko kwenye hiyo NGO ya kina Ndesamburo,Mtei,Mbowe ?.Nilidhani una akili kumbe tayari virusi vya upumbavi vimeshakuvamia.Chadema si chama cha siasa Kafulila kagundua ingawa kachelewa sana bora aende CUF,NCCR au TLP hivi ni vyama vya siasa makini si chadema hata kidogo.

Nipe muda nitakuonyesha upumbavi na ujinga
 
Unajua mkuu ilikuwa hivi!

Mwandishi Mtanzania: Unajua kuwa Viongozi wako wanafanya mkutano Dom wa kukung'oa?

Kafulila: Aah, mimi mbona sifahamu hizo habari, hebu nipe ishu mkuu

Mwandishi Mtanzania: Ndiyo hivyo mkuu, Wamekaa Mbowe, Slaa, Mdee nk wanajdili kukung'oa wewe, Jandu na ( ili kumtia hasira Kafulila na Kumconnect na Zitto) mama yake Zitto

Kafulila ( Bila kupima): Dah mi sina habari mkuu hicho kitakuwa ni Kikaao cha Gheto

Mwandishi Mtanzania akakata simu kecho kwenye Front Page

Bundi Lainyemela Chadema

1: Kikao chafanyika kuwang'oa wafuasi wa Zitto
2: Kiliendeshwa kwa Siri
3: Yeye Kafulila asema ni kikao cha Gheto

Sasa wewe ungekuwa Dr. Slaa ungefanyaje

Ningekuwa kama DR Kafulila lazima ningefanya alivyofanya hasa hasa nikikumbuka Kitufe alichokipata maremu Wangwe. No way ni kulala mbele kukaa mbali na jopo la wazee wa busara.
 
Kumbe Kafulila naye ni Dr? Tuhabarishane ni wa u dr. wa kitu gani?
 
Well, tatizo la wanasiasa wetu walio wengi ni kwamba siasa kwao ni kazi. Akinyang'anywa cheo maana yake ni kwamba wamemnyang'anya namna ya kuishi hapa mjini. Sasa mdogo wangu Kafulila naye inaonekana yumo kwenye kundi hilo. Taarifa tulizo nazo ni kwamba anaenda NCCR na ameahidiwa mambo kedekede ikiwemo kupangishwa nyumba na mshahara wa kila mwezi. It is not about philosophical and policy issues; it is about instrumental needs! What a shame!

Chadema kwa sasa ni taasisi. Huu ni mchujo mzuri, watabaki wanasiasa wa kweli na wenye mapenzi ya kweli ya kufanya siasa na kuleta ukombozi katika nchi hii. Hatukatishwi tamaa, tunaendelea kukanyaga kwenda mbele hadi kieleweka. Tutaweweseka lakini hatuanguki na tunasonga mbele.

Kila la heri mdogo wangu Kafulila huko uendako. Uwe makini sana huko, na uangalie usije ukawa unaruka mkojo....but then it is too late, you have already made your decision. Best wishes!

Kitila kwani hujui kuwa Mbowe anaishi mjini kwa mgongo wa Chadema? hapa umejichanganya kwani toka mwanzo unajulikana wewe ulikuwa kwa Zitto Kabwe ambako Kafulillah yuko wakati wa mkakati wa kumpata Mwenyekiti wa Chama.

umeona uliyotaka hayajawa sasa unawaruka wenzako.huu ni unafiki mkubwa. kama Mbowe ambaye kila cheque lazima asaini wakati wenyeviti wa CCM,CUF NA NCCR hawashiriki kwenye kusaini Cheque.

najua unajikomba kwa Mbowe baada ya Zitto kukosa uenyekiti na wewe ukaonekana msaliti kwa Mbowe.
 
Swahiba wa Zitto Kbwe ajitoa uanachana Chadema

broken-heart.jpg
Na Ramadhan Semtawa

MSHIRIKA wa mkubwa kisiasa wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe, David Kafulila, ametangaza uamuzi mzito wa kujitoa katika chama hicho huku akidaiwa kujiandaa kukimbilia NCCR Mageuzi.

Uamuzi huo ambao unatokana na majeraha ya uchaguzi mkuu wa Septemba, umekuja siku chache baada ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbroad Slaa kutengua ajira ya Kafulila ambaye alikuwa ni Afisa Habari na Danda Juju, aliyekuwa Afisa Mwandamizi wa mambo ya Bunge.

Wakati uamuzi huo umeibua hisia na misimamo tofauti ndani ya Chadema huku wenyeviti 11 wakidaiwa kumpinga Dk Slaa, jana Kafulila aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kutangaza msimamo huo wa kujitoa Chadema na kumshambulia Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe na Dk Slaa.

Ingawa alisita kuweka bayana wapi atakimbilia, lakini habari zilizotufikia zilidokeza kwamba, anajianda kukimbilia NCCR-Mageuzi, ambacho kina nguvu Kigoma Kusini anakotarajia kuwania ubunge mwakani.

Hata hivyo, Kafulila alisema alifikia uamuzi huo baada ya kuona lengo lake la kujenga upinzani imara linahujumiwa na Dk Slaa kwa kumwekea uzio asiweze kuchaguliwa.

Akitangaza uamuzi huo alisema: "Kwa dhamira yangu binafsi, baada ya kukaa kufikiria na kisha kujiridhisha na kupata ushauri kwa watu ninaowaheshimu sana, nimeamua kujitoa Chadema kuanzia leo, ... mimi si mwanachama wa Chadema," alitangaza Kafulila na kufanya ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo kuzizima na kuongeza:

“Ni uamuzi mzito, lakini roho yangu ni nyeupe, sina kinyongo na mtu nimefanya uamuzi huu kwa nia ileile na sitatoka nje ya mstari,... lengo ni kujenga Strong Opposition (upinzani imara) nchini.

"Sijasukumwa na mtu, ni uamuzi ambao umeanzia katika nafsi yangu mwenyewe, ikaja ngazi ya familia na kuendelea juu.

"Nimeondoka Chadema, ila natoa rai kwa wanachama hasa vijana wenzangu kwamba, uhai wao ndani ya chama hicho utategemea sana utiifu wao wa, zidumu fikra za Mwenyekiti Mbowe na Katibu Mkuu Slaa.

“Nataikumbuka Chadema kwa kuwa mnamo Desemba7, 2008, damu yangu ilimwagika wakati wa utumishi wangu katika kazi ya ujenzi wa chama hicho."

Kafulila mwenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja, kuchapa kazi, alisema uamuzi huo umeangalia mbali kutokana na kuona dhahiri amenyang'anywa fursa ya kuchaguliwa na kubakiziwa ile ya kuchagua tu.

Kafulila ambaye aliwahi kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Taifa la chama hicho (Bavicha) katika uchaguzi wa chama hicho hivi karibuni ambayo matokeo yake yalibatilishwa, alidai kuwa hatua ya Dk Slaa ilimuondolea nafasi ya kuchaguliwa na kufifisha ndoto yake ya kujenga upinzani imara nchini.

"Lengo langu limekuwa ni kujenga upinzani imara, lakini niliondolewa fursa hii ndani ya Chadema, katiba ya Chadema inataja mwanachama anaweza kuondoka kwa kujiondoa au kuondolewa kwa kifo kama Chacha Wangwe, sasa mimi nimejiondoa mwenyewe siyo kifo," alifafanua Kafulila.

Alidia kwamba, alifukuzwa uanachama kwa siri ikiwa ni kwasababu ya uongozi mbovu Mbowe. " Si mwanasiasa (Mbowe) ni mfanyabiashara, yuko radhi abaki na wabunge wawili ili aangalie biashara zake, lakini si maslahi ya chama."

Kafulila aliongeza kwamba, kiutaratibu wanachama wote wa Chadema wako chini ya uongozi wa chama, lakini yeye akatakiwa awe nje ya uongozi wa chama.

Alisema kuwa chuki na baadhi ya viongozi hao wa juu, kwamba inatokana na msimamo wake wa kuhoji matumizi ya fedha za chama, zikiwemo Sh35 milioni, za ruzuku ya Desemba ambazo mpaka sasa hazijulikani zilipo.

Alifafanua kwamba, watia saini katika hundi za kuchukua fedha za ruzuku ya chama ni Mbowe, Dk Slaa na Anthony Komu, na kuhoji Mwenyekiti kuwa mtia saini wakati yeye ndiye anapaswa kuiwajibisha Sekretarieti endapo itafanya ufisadi.

Kafulila alimtaka Mbowe kujiondoa kwenye orodha ya watiaji saini, kwani huko ni kukiuka taratibu za uendeshaji taasisi.

“Ajifunze kwa CCM, NCCR, CUF. mbona Lipumba (Ibrahim), Mbatia (James) si watia saini; kwanini yeye ang'ang'anie?" alihoji na kudai:

"La kushangaza watia saini katika fedha za mfuko wa kuchangia chama kwa njia ya SMS pia ni Mbowe na Komu tu; hata hivyo, watu hawa wawili hawakuteuliwa na kikao chochote kufanyakazi hiyo".

Alisema Mkurugenzi wa Fedha (Komu), ndiye mwamuzi kwa kiasi kikubwa katika hatua zote za kuandaa bajeti, kuchukua fedha benki, kuidhinisha matumizi na kufanya maamuzi.

" Hii ni kinyume na utaratibu wa kanuni za matumizi ya fedha za taasisi," alidai

Kijana huyo ambaye aliwahi kuanguka kutoka ghorofa ya kumi akifanya kazi ya kuimarisha Chadema, alisema aliwahi kuhoji fedha hizo, lakini akazimwa na kuelezwa kwamba, yeye ni mwandishi wa muhtasari wa vikao na si mjumbe hivyo akae kimya.

"Nilimwambia Dk Slaa, siwezi kukaa kimya kuzungumzia mambo ya msingi, ni bora niende kuwa mfagiaji kuliko kuzuiwa kusema ukweli unaohusu chama," alidai.

Kafulila aliongeza kwamba, alishangazwa pia na mwendelezo wa chuki dhidi yake ambao ulikuwa ukifanywa na Dk Slaa, kwa kutaka kumchukulia hatua kwa madai ya kumpigia kampeni Zitto, wakati uchaguzi ulikwishapita.

"Dk Slaa alinihoji na kutaka kunichukulia hatua kwasababu nilishiriki kumfanyia kampeni Zitto Kabwe. Lakini John Mrema, John Mnyika, Komu na Benson Kigaila waliokuwa wakimfanyia kampeni Mbowe hawakuhojiwa," alidai na kuongeza:

"Haki haikutendeka kwa kuwa sisi sote tulikuwa watendaji wa makao makuu ya chama. Moja ya sababu kuu iliyonishawishi kumuunga mkono Zitto ni hoja yake aliyotoa bungeni kutaka CAG akague matumizi ya fedha za ruzuku za vyama vya siasa. Ni Ukweli usiopingika inawezekana Chadema kuwa kati ya vinara katika taasisi zenye matumizi mabaya ya ruzuku".

Hii ni hatua nyingine ya Chadema kupita katika wakati mgumu kisiasa, baada ya kukumbwa na hali kama hiyo wakati wa akina Dk Amani Walid Kabourou ambaye alijitoa Chadema kutokana na kutoelewana na baadhi ya viongozi wa juu.

Kujitoa kwa Kafulila ni matokeo ya majeraha ya uchaguzi wa Septemba, ambayo Baraza la Wazee wa chama hicho wakiongozwa na mzee Edwin Mtei, ambao waliokoa jahazi katika uchaguzi uliopita kwa kumshauri Zitto amwachie Mbowe nafasi ya uenyekiti taifa.
 
" Hii ni kinyume nakanuni za matumizi ya fedha za taasisi," alidai utaratibu wa

Hii ni hatua nyingine ya Chadema kupita katika wakati mgumu kisiasa, baada ya kukumbwa na hali kama hiyo wakati wa akina Dk Amani Walid Kabourou ambaye alijitoa Chadema kutokana na kutoelewana na baadhi ya viongozi wa juu. Kujitoa kwa Kafulila ni matokeo ya majeraha ya uchaguzi wa Septemba, ambayo Baraza la Wazee wa chama hicho wakiongozwa na mzee Edwin Mtei, ambao waliokoa jahazi katika uchaguzi uliopita kwa kumshauri Zitto amwachie Mbowe nafasi ya uenyekiti taifa.
 
Kitila kwani hujui kuwa Mbowe anaishi mjini kwa mgongo wa Chadema? hapa umejichanganya kwani toka mwanzo unajulikana wewe ulikuwa kwa Zitto Kabwe ambako Kafulillah yuko wakati wa mkakati wa kumpata Mwenyekiti wa Chama.

umeona uliyotaka hayajawa sasa unawaruka wenzako.huu ni unafiki mkubwa. kama Mbowe ambaye kila cheque lazima asaini wakati wenyeviti wa CCM,CUF NA NCCR hawashiriki kwenye kusaini Cheque.

najua unajikomba kwa Mbowe baada ya Zitto kukosa uenyekiti na wewe ukaonekana msaliti kwa Mbowe.

Wakati mwingine inachekesha sana.

Mbowe amenyanganywa lini bilicanas?
 
Mkuu Kanda 2

Kitila kwani hujui kuwa Mbowe anaishi mjini kwa mgongo wa Chadema? hapa umejichanganya kwani toka mwanzo unajulikana wewe ulikuwa kwa Zitto Kabwe ambako Kafulillah yuko wakati wa mkakati wa kumpata Mwenyekiti wa Chama.

Huo ndio utoto, sasa ulitaka Dr. Baada ya Uchaguzi anedeleze Makundi? Hiyo ndiyo Tofauti iliyopo kati ya Zitto na Kafulila na Dr .Kitila na Kafulila kwa Upande Mwingine

umeona uliyotaka hayajawa sasa unawaruka wenzako.huu ni unafiki mkubwa. kama Mbowe ambaye kila cheque lazima asaini wakati wenyeviti wa CCM,CUF NA NCCR hawashiriki kwenye kusaini Cheque.

Hizo ni taratibu tu ndugu yangu, ningekuona wa maana kama ungekuja hapa na Kusema CHADEMA wamekiuka kipengele huki na hiki, CCM, CUF nk wana utaratibu wao wa Kusign Cheque ambao siyo lazima ufanane na CHADEMA

najua unajikomba kwa Mbowe baada ya Zitto kukosa uenyekiti na wewe ukaonekana msaliti kwa Mbowe.

Mkuu Najua ungempa thanks nyingi sana Dr. kama angecheza Ngoma inayipigwa na Kafulila
 
Kitila kwani hujui kuwa Mbowe anaishi mjini kwa mgongo wa Chadema? hapa umejichanganya kwani toka mwanzo unajulikana wewe ulikuwa kwa Zitto Kabwe ambako Kafulillah yuko wakati wa mkakati wa kumpata Mwenyekiti wa Chama.

umeona uliyotaka hayajawa sasa unawaruka wenzako.huu ni unafiki mkubwa. kama Mbowe ambaye kila cheque lazima asaini wakati wenyeviti wa CCM,CUF NA NCCR hawashiriki kwenye kusaini Cheque.

najua unajikomba kwa Mbowe baada ya Zitto kukosa uenyekiti na wewe ukaonekana msaliti kwa Mbowe.

Daaaaaaaaa
Rafiki ,siamini maneno yako Dr mzima kweli anaweza kujikomba kwa Mbowe ?? teh teh teh

si mchezo - - ooo
 
Unajua mkuu ilikuwa hivi!

Mwandishi Mtanzania: Unajua kuwa Viongozi wako wanafanya mkutano Dom wa kukung'oa?

Kafulila: Aah, mimi mbona sifahamu hizo habari, hebu nipe ishu mkuu

Mwandishi Mtanzania: Ndiyo hivyo mkuu, Wamekaa Mbowe, Slaa, Mdee nk wanajdili kukung'oa wewe, Jandu na ( ili kumtia hasira Kafulila na Kumconnect na Zitto) mama yake Zitto

Kafulila ( Bila kupima): Dah mi sina habari mkuu hicho kitakuwa ni Kikaao cha Gheto

Mwandishi Mtanzania akakata simu kecho kwenye Front Page

Bundi Lainyemela Chadema

1: Kikao chafanyika kuwang'oa wafuasi wa Zitto
2: Kiliendeshwa kwa Siri
3: Yeye Kafulila asema ni kikao cha Gheto

Sasa wewe ungekuwa Dr. Slaa ungefanyaje

Hili igizo tamu sana, lakini chungu. Dr. Slaa na kikaa walimuamuru Kufulila kuomba radhi na kukanusha hizo taarifa. Jamaa akakataa wewe ungekuwa maneja na mtumishi anakataa maagizo ya kikao ungefanyaje?
 
Kitila,
Acha kumchafua kijana Kafulila, maana mchawi hapa anaonekana wazi kuwa ni Mbowe. Kafulila hakutaka kuondoka CHADEMA ila Mbowe ndiye aliyesisitiza kuwa aondolewe uongozini na kwenye chama. Kama una sababu za kutetea uamuzi wa Mbowe ziweke wazi, lakini usimpake kijana wetu matope.

Well, tatizo la wanasiasa wetu walio wengi ni kwamba siasa kwao ni kazi.
Kama mtu anapigania maendeleo/ukombozi wa nchi yake, lazima siasa iwe ni kazi. Niambie ni msomi gani anayeweza kukubali kudhalilishwa na kihiyo kwa vile tu ana pesa na madaraka?

Akinyang'anywa cheo maana yake ni kwamba wamemnyang'anya namna ya kuishi hapa mjini. Sasa mdogo wangu Kafulila naye inaonekana yumo kwenye kundi hilo.
Kama Kafulila angekuwa anataka kukaa mjini kwa starehe si angekuwa ameshakimbilia CCM kuliko na madaraka yenye marupurupu kibao?

Taarifa tulizo nazo ni kwamba anaenda NCCR
na ameahidiwa mambo kedekede ikiwemo kupangishwa nyumba na mshahara wa kila mwezi. It is not about philosophical and policy issues; it is about instrumental needs! What a shame!
Kwa hiyo unataka kutuambia Kafulila kilichokuwa kinamuweka CHADEMA ni mshahara? Unafikiri kwa elimu yake hangeweza kupata mshahara mnono kuliko wa CHADEMA au NCCR? Shame on you Kitila. You should apologize to Kafulila.

Chadema kwa sasa ni taasisi.
Huu ni mchujo mzuri, watabaki wanasiasa wa kweli na wenye mapenzi ya kweli ya kufanya siasa nakuleta ukombozi katika nchi hii.
Eti CHADEMA ni taasisi? What a joke? Taasisi gani yenye kufuata maamuzi ya mtu mmoja tu, Mbowe/Mtei?

Hatukatishwi tamaa, tunaendelea kukanyaga kwenda mbele hadi kieleweka. Tutaweweseka lakini hatuanguki na tunasonga mbele.
Kitila, Kama wewe hujakatishwa tamaa na yanayoendelea ndani ya CHADEMA, basi una sababu nzito za kukumbatia uongozi wa Mbowe/Mtei.

Lakini dalili za hapa mtandaoni kama zitakuwa ni sambamba na Watanzania walioipenda Chadema, ni wazi kuwa wengi wameshaanza kukata tamaa. Hii ni pamoja na watu kama Mwanakijiji (angalia article yake ya jana juu ya upinzani) ambaye kwa mbali ameanza kuikosoa CHADEMA, kitu cha kushangaza kidogo.

Kuweweseka kwa CHADEMA ni kilio cha taifa. Na kama CHADEMA itafifia kama ilivyokuwa NCCR, wa kulaumiwa ni watu kama wewe Kitila ambao mnaweka maslahi binafsi mbele badala ya kuongea ukweli juu ya madudu ya Mbowe.

I am sure Zitto is next on the guilotine.
 
Swahiba wa Zitto Kbwe ajitoa uanachana Chadema
Na Ramadhan Semtawa
MSHIRIKA wa mkubwa kisiasa wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe, David Kafulila, ametangaza uamuzi mzito wa kujitoa katika chama hicho huku akidaiwa kujiandaa kukimbilia NCCR Mageuzi.

Uamuzi huo ambao unatokana na majeraha ya uchaguzi mkuu wa Septemba, umekuja siku chache baada ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbroad Slaa kutengua ajira ya Kafulila ambaye alikuwa ni Afisa Habari na Danda Juju, aliyekuwa Afisa Mwandamizi wa mambo ya Bunge.

Wakati uamuzi huo umeibua hisia na misimamo tofauti ndani ya Chadema huku wenyeviti 11 wakidaiwa kumpinga Dk Slaa, jana Kafulila aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kutangaza msimamo huo wa kujitoa Chadema na kumshambulia Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe na Dk Slaa.

Ingawa alisita kuweka bayana wapi atakimbilia, lakini habari zilizotufikia zilidokeza kwamba, anajianda kukimbilia NCCR-Mageuzi, ambacho kina nguvu Kigoma Kusini anakotarajia kuwania ubunge mwakani.

Hata hivyo, Kafulila alisema alifikia uamuzi huo baada ya kuona lengo lake la kujenga upinzani imara linahujumiwa na Dk Slaa kwa kumwekea uzio asiweze kuchaguliwa.

Akitangaza uamuzi huo alisema: "Kwa dhamira yangu binafsi, baada ya kukaa kufikiria na kisha kujiridhisha na kupata ushauri kwa watu ninaowaheshimu sana, nimeamua kujitoa Chadema kuanzia leo, ... mimi si mwanachama wa Chadema," alitangaza Kafulila na kufanya ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo kuzizima na kuongeza:

“Ni uamuzi mzito, lakini roho yangu ni nyeupe, sina kinyongo na mtu nimefanya uamuzi huu kwa nia ileile na sitatoka nje ya mstari,... lengo ni kujenga Strong Opposition (upinzani imara) nchini.

"Sijasukumwa na mtu, ni uamuzi ambao umeanzia katika nafsi yangu mwenyewe, ikaja ngazi ya familia na kuendelea juu.

"Nimeondoka Chadema, ila natoa rai kwa wanachama hasa vijana wenzangu kwamba, uhai wao ndani ya chama hicho utategemea sana utiifu wao wa, zidumu fikra za Mwenyekiti Mbowe na Katibu Mkuu Slaa.

“Nataikumbuka Chadema kwa kuwa mnamo Desemba7, 2008, damu yangu ilimwagika wakati wa utumishi wangu katika kazi ya ujenzi wa chama hicho."

Kafulila mwenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja, kuchapa kazi, alisema uamuzi huo umeangalia mbali kutokana na kuona dhahiri amenyang'anywa fursa ya kuchaguliwa na kubakiziwa ile ya kuchagua tu.

Kafulila ambaye aliwahi kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Taifa la chama hicho (Bavicha) katika uchaguzi wa chama hicho hivi karibuni ambayo matokeo yake yalibatilishwa, alidai kuwa hatua ya Dk Slaa ilimuondolea nafasi ya kuchaguliwa na kufifisha ndoto yake ya kujenga upinzani imara nchini.

"Lengo langu limekuwa ni kujenga upinzani imara, lakini niliondolewa fursa hii ndani ya Chadema, katiba ya Chadema inataja mwanachama anaweza kuondoka kwa kujiondoa au kuondolewa kwa kifo kama Chacha Wangwe, sasa mimi nimejiondoa mwenyewe siyo kifo," alifafanua Kafulila.

Alidia kwamba, alifukuzwa uanachama kwa siri ikiwa ni kwasababu ya uongozi mbovu Mbowe. " Si mwanasiasa (Mbowe) ni mfanyabiashara, yuko radhi abaki na wabunge wawili ili aangalie biashara zake, lakini si maslahi ya chama."

Kafulila aliongeza kwamba, kiutaratibu wanachama wote wa Chadema wako chini ya uongozi wa chama, lakini yeye akatakiwa awe nje ya uongozi wa chama.

Alisema kuwa chuki na baadhi ya viongozi hao wa juu, kwamba inatokana na msimamo wake wa kuhoji matumizi ya fedha za chama, zikiwemo Sh35 milioni, za ruzuku ya Desemba ambazo mpaka sasa hazijulikani zilipo.

Alifafanua kwamba, watia saini katika hundi za kuchukua fedha za ruzuku ya chama ni Mbowe, Dk Slaa na Anthony Komu, na kuhoji Mwenyekiti kuwa mtia saini wakati yeye ndiye anapaswa kuiwajibisha Sekretarieti endapo itafanya ufisadi.

Kafulila alimtaka Mbowe kujiondoa kwenye orodha ya watiaji saini, kwani huko ni kukiuka taratibu za uendeshaji taasisi.

“Ajifunze kwa CCM, NCCR, CUF. mbona Lipumba (Ibrahim), Mbatia (James) si watia saini; kwanini yeye ang'ang'anie?" alihoji na kudai:

"La kushangaza watia saini katika fedha za mfuko wa kuchangia chama kwa njia ya SMS pia ni Mbowe na Komu tu; hata hivyo, watu hawa wawili hawakuteuliwa na kikao chochote kufanyakazi hiyo".

Alisema Mkurugenzi wa Fedha (Komu), ndiye mwamuzi kwa kiasi kikubwa katika hatua zote za kuandaa bajeti, kuchukua fedha benki, kuidhinisha matumizi na kufanya maamuzi.

" Hii ni kinyume na utaratibu wa kanuni za matumizi ya fedha za taasisi," alidai

Kijana huyo ambaye aliwahi kuanguka kutoka ghorofa ya kumi akifanya kazi ya kuimarisha Chadema, alisema aliwahi kuhoji fedha hizo, lakini akazimwa na kuelezwa kwamba, yeye ni mwandishi wa muhtasari wa vikao na si mjumbe hivyo akae kimya.

"Nilimwambia Dk Slaa, siwezi kukaa kimya kuzungumzia mambo ya msingi, ni bora niende kuwa mfagiaji kuliko kuzuiwa kusema ukweli unaohusu chama," alidai.

Kafulila aliongeza kwamba, alishangazwa pia na mwendelezo wa chuki dhidi yake ambao ulikuwa ukifanywa na Dk Slaa, kwa kutaka kumchukulia hatua kwa madai ya kumpigia kampeni Zitto, wakati uchaguzi ulikwishapita.

"Dk Slaa alinihoji na kutaka kunichukulia hatua kwasababu nilishiriki kumfanyia kampeni Zitto Kabwe. Lakini John Mrema, John Mnyika, Komu na Benson Kigaila waliokuwa wakimfanyia kampeni Mbowe hawakuhojiwa," alidai na kuongeza:

"Haki haikutendeka kwa kuwa sisi sote tulikuwa watendaji wa makao makuu ya chama. Moja ya sababu kuu iliyonishawishi kumuunga mkono Zitto ni hoja yake aliyotoa bungeni kutaka CAG akague matumizi ya fedha za ruzuku za vyama vya siasa. Ni Ukweli usiopingika inawezekana Chadema kuwa kati ya vinara katika taasisi zenye matumizi mabaya ya ruzuku".

Hii ni hatua nyingine ya Chadema kupita katika wakati mgumu kisiasa, baada ya kukumbwa na hali kama hiyo wakati wa akina Dk Amani Walid Kabourou ambaye alijitoa Chadema kutokana na kutoelewana na baadhi ya viongozi wa juu.

Kujitoa kwa Kafulila ni matokeo ya majeraha ya uchaguzi wa Septemba, ambayo Baraza la Wazee wa chama hicho wakiongozwa na mzee Edwin Mtei, ambao waliokoa jahazi katika uchaguzi uliopita kwa kumshauri Zitto amwachie Mbowe nafasi ya uenyekiti taifa.

Source: Gazeti la Mwananchi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom