Tayana-wog
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 28,849
- 37,556
Noma sn na inasikitisha.Mkuu acha kuendelea kumjibu huyo. Inawezekana anaelewa na anajua kinachoendelea ila anafanya distraction ili watawala waendelee kulala usingizi wa pono wasijue kinachoendelea au ni kweli akawa ni chawa ambaye mambo magumu kama haya hawezi kabisa kuyachambua.
Ninachozidi kujifunza ni kwamba tuna viongozi wachache sana wenye uelewa mkubwa wa mambo ya nchi yanavyoenda kwasababu kwa akili ya kawaida tu kabisa kama uko vizuri kichwani ukifuatilia series za Tumia akili unajua kila kitu kinachoendelea na matakwa ya taifa ni yapi kwa sasa lakini naona viongozi wetu ni kama wametiwa ganzi wasijue chochote kilichowekwa wazi hata kama kuna codes ngumu. Iliposemwa makamu wa rais alijiuzuru kwa usaliti na makamu mwingine akachaguliwa siyo lazima kweli awe amesaliti pengine yeye amesoma alama za nyakati na kuyaona yanayokuja. Sote tunaona Mpangomzima alivyoacha na Mchimbachumvi kuanza kupiga jaramba tunasubiri tu skendo ya watergate iondoke na mkulu mwenyewe.
Kuna wakati nawaona usalama wa taifa hawalisaidii taifa ila napokutana na nyuzi za kina Tumia akili nawaona walivyo na mpango wa kulifanya hili taifa kuwa la wananchi hapo baadaye kidogo.
Credits nyingi sana kwa mkuu Yoga maana hapa pamekuwa ndiyo majumuisho ya mambo yote mazito yanayoendelea. Nawaomba wenye nchi muendelee na hii mipango wengine tunaumia sana mali za Tanganyika zinapobebwa utadhani hazina wenyewe, sisi sote tupo tu kwenye hili mia la 2000 mpaka 2100 baada ya hapo hatutakuwepo ya nini kufuja mali za watanzania wajao baada ya sisi kuwa tumeondoka.
The state endeleeni na mipango yenu ya kuliwekea taifa misingi imara kwasasa Tanzania unapokuwa upande tofauti na lile lichama unakuwa kama mhamiaji haramu na unaweza ukauawa kama kuku kisa tu umewakosoa watu wa chama kile.
Ahsante.
Ila sijabahatika kumsoma tumia akili ,naomba uwe unani tag kaka