Now we go....
Baada ya kupata umeme tunakuja kwenye amplifier yenyewe
Ambayo msukaji yani wewe mwenyewe utaamua usuke kwa kutumia nini yaani ic Au transistor
Nikukumbushe tu kua unapoanza kusuka lazima uwe na imaginations kichwani ya aina ya sound unayoitaka
Kisha ndio uta select aina ya circuit (tuite ramani) unayotaka
Na hizi ic zimetofautiana uwezo
Kwahyo kabla ya kusuka utachagua ic na kila ic ina specification zake yaani ina mashart na maelezo yake kuihusu yenyewe
Kwamfano kuna ic kama TDA2050 na nyingine TDA 7379 hizi zoote ni za amplifier lakini kila moja inauwezo wake na mashart yake
Kwamfano hiyo 2050 inaingiza hadi volts 25 na inakupa hadi watts 50 lakini ni inakupa channel moja tu (kuhusu channel ntakuelezea baadae)
Lakini hiyo 7379 inakupa channel 4 ila ina watts 38
Sasa basi kabla ya kusuka kujua unachohitaji ni kitu cha muhimu sana
Kwahivyo basi ni muhimu kuisoma ic husika kabla yakuanza kuitumia il kuijua kabla yakuanza kuisuka
Hiyo itakusaidia usiunguze na kuiharibu
Na hiyo itakupa hasara sana.
Kwa wale wenye android wanaweza ku download datasheet za ic husika kwa kuandika neno pdf mbele kisha ita downtown
Kwamfano
Andika Tda 2030 pdf download ukisha download itakuja mfano wa kitabu kisha utakisoma ili kusijua
Na waweza download nyingi ili kuzijua kwa wingi
TDA 2050
.......2030
........7379
........2040
........2003
KA2206
LA4440
na nyinginezo nyiiiiingi mno
(Utachagua wewe tu kulingana na matumizi yako)
Kwanini nasema kulingana na matumizi yako[emoji848][emoji848][emoji848]
Kwa mfano wewe una sora hizo tda 2050 zinaweza kua sio rafiki kwako kutokana na umeme wako
Kwahyo itakubid utumie za single power supply ingawa zote ni ic na zote zina fanya jazi moja.