Mbunge Mahawanga azindua Jukwaa la Wanawake kata ya Ndugumbi na kusisitiza ushirikiano

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

MBUNGE MAHAWANGA AZINDUA JUKWAA LA WANAWAKE KATA YA NDUGUMBI NA KUSISITIZA USHIRIKIANO.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Mahawanga Janeth amezindua Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi katika Kata ya Ndugumbi Wilaya ya Kinondoni ikiwa ni muendelezo wa kufanya ziara ya kukutana na Wanawake sambamba na Vijana na Mabinti ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Uzinduzi huo umeweza kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni sambamba na Viongozi wa Chama na Jumuiya zake vilevile Viongozi wa Umoja wa Wanawake kutoka Kata jirani sambamba na Wanachama wa Majukwaa kutoka Vikundi 197 vya Kata ya Ndugumbi.

Mhe. Mahawanga kupitia Uzinduzi huo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ndiyo Muasisi wa Majukwaa kwa maono chanya na kiu yake ya kuwakwamua Wanawake kiuchumi kupitia fursa mbalimbali.

Mhe. Mahawanga ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni kwa kuwawezesha Wanawake wa Kata ya Ndugumbi kwa kupitia mikopo ya 10% kwa kuwawezesha kiasi cha 380,716,000/= kwa mwaka 2021 - 2023 sambamba na Wanawake 151 kunufaika na fursa mbalimbali ikiwemo mafunzo ya haki za Wanawake, Biashara, Ujasiriamali wa bidhaa mbalimbali. Elimu ya afya ya uzazi, Fursa n.k

Aidha, Mhe. Mahawanga amesisitiza ili majukwaa yaweze kuendelea na kuwa imara ni muhimu Viongozi na wanachama kuendeleza upendo, ushirikiano, kuchangamkia fursa zinazotuzunguka, kuwa wabunifu sambamba na kumtanguliza Mungu katika shughuli za kila siku.

Mhe. Mahawanga amekemea vikali vitendo vya kutokuheshimiana katika jukwaa na kuwataka wanachama na Viongozi kuheshimiana, kukosoana kwa staha, kusameheana wanapotofautiana na kusimamia malengo mahususi ya majukwaa kama inavyoelekeza miongozo ya majukwaa.

Aidha, Mhe. Mahawanga amewaahidi kuwa nao bega kwa bega kuhakikisha Jukwaa la Wanawake Kata ya Ndugumbi pamoja na Majukwaa yote ya Mkoa wa Dar es Salaam yanafanikiwa pamoja na kuendelea kupokea changamoto zote na kuzifanyia kazi.

Pia, Mhe. Mahawanga amewasisitiza Wanamajukwaa kuelekea Ucahguzi wa Serikali za Mitaa 2024 Wanawake wajitokeze kwa wingi kuchukua fomu na kugombea.

WhatsApp Image 2023-11-30 at 13.05.47.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-30 at 13.05.47(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-30 at 13.05.48.jpeg
 
Back
Top Bottom