Dar: Mwandishi Bollen Ngetti adaiwa kutekwa tena na watu wasiojulikana; apatikana

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
1577109453574.png

Ikiwa ni siku 4 tangu Afisa Programu na Elimu kwa Umma wa LHRC, Tito Magoti ‘atekwe’ na wasiojulikana, kuna taarifa kuwa mwandishi Bollen Ngeti naye ametekwa na wasiojulikana leo maeneo ya Msasani, Dar

POLISI: HATUNA TAARIFA UTEKWAJI WA MWANDISHI.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni kupitia kamanda Mussa Taibu limesema halina taarifa za kutekwa kwa mwandishi wa habari nchini Tanzania, Bollen Ngeti, ambaye inadaiwa kuwa ametekwa leo na watu wasiojulikana eneo la Msasani, DSM.

=======

UPDATES

Kwa mujibu wa mke wa Bollen Ngeti, mumewe alimfahamisha kuwa amekamatwa akiwa maeneo ya Banana jijini Dar na alikuwa anahofia usalama wake

> Bollen alimtaka mkewe awafahamishe watu haraka na alihisi ni katika sakata la Tito Magoti

#JFLeo #FreeBollenNgeti #FreeTitoMagoti

Zaidi soma:




 
Nimeona hii habari nikabaki nashangaa.

Kupitia twitter,mtu anaejiita Martini M.M kapost hii habari tangu saa 11:28 alfajiri ya leo ila nashangaa sijui watu hawakuiona hii tweet maana reaction ni kama haikuwepo kabisa jambo linaloshangaza sana.

Hivi sasa inaonekane ame-post tena kama dakika 29 hivi zilizopita ila ukiifungua hiyo tweet inaonekana ni ya leo saa 11:28 alfajiri.

Anyway,labda tatizo ni mfumo wa masaa unaotumika ndio unaleta huu mkanganyiko.
 
Back
Top Bottom