Wakili Mwabukusi, Emmanuel Masonga na Mdude Nyagali wakamatwa na Polisi Mikumi wakiwa safarini kuelekea Dar es Salaam

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Sep 13, 2020
3,166
4,581
Ndugu Watanzania,

Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kuwa wakili msomi Boniface Kanjunjule Mwabukusi amekamatwa na Jeshi la Polisi kule Mikumi, Morogoro akiwa pamoja na Katibu wa Kanda wa CHADEMA, Emmanuel Masonga na Mdude Nyagali.

Inadaiwa kuwa walikuwa safarini kuelekea Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, watu waliojitambulisha kuwa ni Askari ndio wamewakamata pasipo kutaja kosa lao na wapi wanapelekwa zaidi ya kuambiwa ni Maelekezo kutoka Juu. Pia, vifaa vyao vya mawasiliano (Simu za mkononi) vimechukuliwa.

Pia soma: RPC Morogoro: Sina taarifa ya kukamatwa kwa Wakili Mwabukusi, Mdude na Masonga

20230812_180225.jpg
 
Hakuna jipya hapo, Adv Mwabukusi hajakamatwa peke yake, hata Mdude Nyagali, na kamanda Nyaisunga, nao pia wamekamatwa, wote wako kutuo cha polisi, Mikumi, Morogoro.

Hapa tuwekane sawa tu, hayupo yeyote kati ya waliokamatwa ambaye hakujua matokeo ya kile wanachokipigania, wanachokifanya polisi sio kuwatisha, au kuwaogopesha, ni kuwafanya wawe imara zaidi kwenye mapambano.
 
Matatizo ya kuishi in a shithole country, police wanapomkamata suspect ni LAZIMA haki yake apewe ikiwa ni pamoja na kuambiwa why anakamatwa, haki zake including kuwa kimya, na anapewa nafasi ya ku contact lawyer wake na ndugu yake(mmoja),watanzania watapiga kelele na kulalama humu, mabadiliko yanapatikana kwenye streets battles, igp ameogopa kivuli chake
 
Back
Top Bottom