Dar Lux, kampuni bora ya mabasi inayoelekea kaburini

ilikuaje chief?
Nilifanya Booking kwenye System yao ya Online Ticket. Bus ya kahama...nimepita hatua zote mpaka kutuma pesa.Sasa issue ikawa wao kunitumia zile namba.
Nilitumia Tigopesa,Tigo walileta ujumbe wa kupokelewa.

Kuja kupiga Customer care,kuna mtu alinijibu kuwa nilikosea booking kuwa Bus ilikuwa imejaa.Nikamweleza kuwa naelewa nilichokuwa nafanya.System yao haikonesha kuwa Bus imejaa..Seat zilikuwa wazi..tena akaenda mbali sana kuwa kwanini nilitumia online booking System.
Nikaona si taabu mana tuliwatumia hao kama mara 3 hivi kwa safari na huwa natunza Ticket..nikapiga simu Dar Es Salaam.

Nikawaelezea jinsi ilivyokuwa,wakaanza tena oh eeh..nikawaambia si kila mtu ni mjinga kama ni System algorthim kuna watu inaweza kuwa tunafahamu msipende kuwa waongo sema kweli.Ikabidi kutoa kipindi kuhusu system yao.

Niliwaambia si jukumu la mteja kujua System inafanya refresh kila baada ya millsecond ngapi..kazi ya Mteja ni kufanya Booking tu.

Kama mliona kuwa System inashinda kuji Update ..mlishindwa nini kutoa ujumbe kuwa kuna shida?Wangapi mtakuwa mmetuibia..haya sasa kama nisingekuwa na Option ya fedha ya ziada inaa maana nisingalisafiri kwa ajili ya Upuuzi wenu.

Wakasema hiyo ni shida kubwa basi wakanipa namba za mtu wajuu ili atoe Authorization ya kurudishwa Fedha.Nilipiga hakupokea.Na hili la kurudishiwa Fedha ni baada ya kuwaeleza kuwa nilikuwa na screenshots zote za Ushahidhi wa hiyo System yao kila hatua niliyokuwa nafanya.

Waliniudhi sanaa maana ilikuwa ni muhimu sana hiyo safari ikabidi kuzogeza muda mbele wa Safari kitu ambacho kiliathiri mambo mengi tu.

Nilimaliza kwa kuwaeleza tu kama mtaendelea hivyo wateja wengi watagundua tu hayo matatizo na msipojiangalia mtashuka taratibu kwa ajili ya malalamiko na usumbufu huo ambao nyie mnaona ni kawaida kwenu.

Ilikuwa Mwaka jana Mwezi wa Kumi.
 
Mkuu mie nimeongelea njia ya Mwaza Dar
hayo mabus labda ya uko kwenu ndo yamechoka kutokana na umbali wa safari, DAR LUX za kwenda moshi/arusha ni noumaaa yana bei ya juu lkn ni shidyaaa yanapendwa na watu haswa na ukipata unafika kwa muda mzuri
 
Back
Top Bottom