LATRA simamieni sheria, mabasi yote yapakie na kushusha abiria kwenye stendi ya mabasi ya Magufuli Mbezi

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,136
7,711
Tabia ya kila basi kupakia na kushusha abiria sehemu yoyote katika Jiji la Dar es Salam imekuwa kwa kasi ya ajabu. Hivi sasa Mabasi yamezagaa katika kila mtaa yanapakia na kushusha abiria waendao na watokao mikoani.

Hali hii imechochea ongezeko la ajali lakini pia usalama umekuwa mdogo sana.

Swali la kujiuliza ni je? Ni lipi haswa lengo la kujengwa stendi ya mabasi ya Magufuli Mbezi?!!!

Wananchi wengi wameanza kulalamika kuibiwa na kutapeliwa kwa mabasi yanayo Pakia abiria maeneo ya Shekilango, manzese, magomeni n.k.
Hakuna usalama, lkini pia mabasi yenyewe hayakaguliwi na wakaguzi wa mabasi yaani vehicle inspectors.

Kama kuna sheria inaruhusu kila basi kupakia na kushusha popote basi sheria hiyo irekebishwe mara moja na LATRA wanao wajibu wa kusimamia na kuhakikosha mabasi yote yanafuata na kutii sheria ya kupakia na kushusha abiria kwenye stendi maalum.

Nimepita maeneo ya shekilango, manzese n.k ni vurugu tupu, mambo yanaenda ovyoovyo!!! Kila basi linajifanyia mambo yake!!! LATRA mko wapi??!

Kumbe naweza kununua basi la abiria halafu nikawa napakiza na kushusha abiria nyumbani kwangu bila tatizo lolote.

hii vurugu imekuwa ni kichaka cha uhalifu wa kusafirisha bangi na aina nyingine ya madawa ya kulevya ni lazima Mamlaka husika zichukue hatua haraka.

Nawatakia krismas njema.
Yesu Kristu azaliwe kwenye mioyo yetu, tuwe na upendo na huruma kwa binaadamu wenzetu.
 
Tabia ya kila basi kupakia na kushusha abiria sehemu yoyote katika Jiji la DSM imekuwa kwa kasi ya ajabu. Hivi sasa Mabasi yamezagaa katika kila mtaaa yanapakia na kushusha abiria waendao na watokao mikoani.

Hali hii imechochea ongezeko la ajali lakini pia usalama umekuwa mdogo sana.

Swali la kujiuliza ni je? Ni lipi haswa lengo la kujengwa stendi ya mabasi ya Magufuli Mbezi?!!!

Kama kuna sheeia inaruhusu kila basi kupakia na kushusha popote basi sheria hiyo irekebishwe mara moja na LATRA wanao wajibu wa kusimamia na kuhakikosha mabasi yote yanafuata na kutii sheria ya kupakia na kushusha abiria kwenye stendi maalum.

Unajua ukubwa wa Dar es Salaam hadi utake abiria wote wakarundikiwe hapo kituoni, hata kama ni utetezi wa ligasi usijitoe akili kiasi hicho. Dar es Salaam inapaswa kuwa na vituo hata vitano vikubwa vya mabasi.
 
ungekuja unakaa bunju halafu unatokea Arusha via bagamoyo road usingeandika ulichokiandika
Lengo la kujengwa kituo kikubwa vha mabasi cha Magufuli ni kuhakikisha Mabasi yote yanaingia hapo na sio vinginevyo.

Ila naona LATRA na wadau wengine wanaona "muhali" kuchukua hatua dhidi ya makampuni ambayo yameanzisha stendi bubu katika maeneo ya ofisi zao.
 
Tabia ya kila basi kupakia na kushusha abiria sehemu yoyote katika Jiji la DSM imekuwa kwa kasi ya ajabu. Hivi sasa Mabasi yamezagaa katika kila mtaaa yanapakia na kushusha abiria waendao na watokao mikoani.

Hali hii imechochea ongezeko la ajali lakini pia usalama umekuwa mdogo sana.

Swali la kujiuliza ni je? Ni lipi haswa lengo la kujengwa stendi ya mabasi ya Magufuli Mbezi?!!!

Kama kuna sheeia inaruhusu kila basi kupakia na kushusha popote basi sheria hiyo irekebishwe mara moja na LATRA wanao wajibu wa kusimamia na kuhakikosha mabasi yote yanafuata na kutii sheria ya kupakia na kushusha abiria kwenye stendi maalum.

Nawatakia krismas njema.
Yesu Kristu azaliwe kwenye mioyo yetu, tuwe na upendo na huruma kwa binaadamu wenzetu.
Kitu cha msingi cha kuzingatia ni usalama, haya ya kushusha na kupakia abiria mahali popote inaruhusiwa kisheria. Hivyo vituo binafsi vya kupakia abiria vimesajiliwa kisheria, hakuna sheria inayovunjwa kwa kufanya hivyo.
 
Unajua ukubwa wa Dar es Salaam hadi utake abiria wote wakarundikiwe hapo kituoni, hata kama ni utetezi wa ligasi usijitoe akili kiasi hicho. Dar es Salaam inapaswa kuwa na vituo hata vitano vikubwa vya mabasi.
Kwa sasa hakuna kituo kingine cha Mabasi zaidi ya Stendi ya mabasi ya Magufuli. Hivyo lazima utaratibu uheshimiwe.

Viongozi wetu waache kuwa na vigugumizi na uoga katika kusimamia taratibu.
 
Sioni shida yoyote

Kuhusu kushusha abiria kabla ya stendi kuu ni sawa. Fikiria basi la kutoka Kilimanjaro kupitia Bagamoyo lina abiria wa Bunju. Unataka akashushwe Magufuli(Mbezi) halafu ndio atafute daladala arudi Bunju?

Abiria atashushwa njiani na bado basi litaenda stendi kuu kushusha abiria wengine. Watakaoamua kubaki kwenye basi waende kushuka kwenye ofisi za hilo basi kwa ajili ya unafuu wa kwenda waendako ni sawa pia

Ukija upande wa kupandisha abiria. Wakipandisha abiria kwenye ofisi zao bado basi litaenda stendi kuu kupakia abiria wengine. Na hapa abiria aliyepandia ofisini kwa sababu ya ukaribu na anapotoka amepunguziwa gharama ya kwenda stendi kuu

Biashara ina ushindani mkubwa customer care nzuri muhimu sana kuvutia wateja
 
Tabia ya kila basi kupakia na kushusha abiria sehemu yoyote katika Jiji la DSM imekuwa kwa kasi ya ajabu. Hivi sasa Mabasi yamezagaa katika kila mtaaa yanapakia na kushusha abiria waendao na watokao mikoani.

Hali hii imechochea ongezeko la ajali lakini pia usalama umekuwa mdogo sana.

Swali la kujiuliza ni je? Ni lipi haswa lengo la kujengwa stendi ya mabasi ya Magufuli Mbezi?!!!

Kama kuna sheria inaruhusu kila basi kupakia na kushusha popote basi sheria hiyo irekebishwe mara moja na LATRA wanao wajibu wa kusimamia na kuhakikosha mabasi yote yanafuata na kutii sheria ya kupakia na kushusha abiria kwenye stendi maalum.

Nimepita maeneo ya shekilango, manzese n.k ni vurugu tupu, mambo yanaenda ovyoovyo!!! Kila basi linajifanyia mambo yake!!! LATRA mko wapi??!

Nawatakia krismas njema.
Yesu Kristu azaliwe kwenye mioyo yetu, tuwe na upendo na huruma kwa binaadamu wenzetu.
Mkuu hebu fikiri, mtu anaishi Bunju basi linatoka Moshi linapita Bunju yaani limpitishe mpaka Kimara aanze kuhangaika na mizigo kurudi Bunju?
 
Tabia ya kila basi kupakia na kushusha abiria sehemu yoyote katika Jiji la DSM imekuwa kwa kasi ya ajabu. Hivi sasa Mabasi yamezagaa katika kila mtaaa yanapakia na kushusha abiria waendao na watokao mikoani.

Hali hii imechochea ongezeko la ajali lakini pia usalama umekuwa mdogo sana.

Swali la kujiuliza ni je? Ni lipi haswa lengo la kujengwa stendi ya mabasi ya Magufuli Mbezi?!!!

Kama kuna sheria inaruhusu kila basi kupakia na kushusha popote basi sheria hiyo irekebishwe mara moja na LATRA wanao wajibu wa kusimamia na kuhakikosha mabasi yote yanafuata na kutii sheria ya kupakia na kushusha abiria kwenye stendi maalum.

Nimepita maeneo ya shekilango, manzese n.k ni vurugu tupu, mambo yanaenda ovyoovyo!!! Kila basi linajifanyia mambo yake!!! LATRA mko wapi??!

Nawatakia krismas njema.
Yesu Kristu azaliwe kwenye mioyo yetu, tuwe na upendo na huruma kwa binaadamu wenzetu.
Bila shaka wewe ni agent au mkatisha tiketi hapo Magufuli stand 😂😂

Yaani nitoke Dodoma nishuke Magufuli stand wakati gari linafika MBAGALA na mimi naelekea maeneo hayo hayo ya Mbagala?

Halafu si kweli kusema magari yanashusha na kupandisha kila sehemu

Gari ikitoka Magufuli stand huwa haishushi ila kwenye kituo chake

Halafu usichofahamu kuna ushindani mkubwa wa kibiashara na ndio maana magari mengine yanaanzia kutoka mbali ili kuokoteza abiria, na wanasaidia sana watu.

Post ya kipumbavu ya kufungia mwaka
 
Acheni uchawi kwani kuna basi halipiti Magufuli ???Yanapita pale na wanashuka wale wanaotaka kushuka pale na wengine km mnataka kushuka shekilango na sehem ofsi za mabas hayo mnabaki.Hujui tu yanasaidia sana kutupunguzia gharama za kukodi gari toka mbezi mpaka tunakokaaa Ww kwa kua umekaa tu nyumbani hujui sisi tunao safiri na tunarudi na mizigo ni msaada mkubwa sana tunapata kwa kutusogeza town.Ningekuona una akili ungelalamika kuhusu kupanda gharama za nauli unakuja kulalamika upuuzi tu.
 
Kama maghufuli stand wanalipwa Hela Yao ya basi hata lisipopaki hapo shida Nini wao si wanataka pesa.
Wananchi wengi wameanza kulalamika kuibiwa na kutapeliwa kwa mabasi yanayo Pakia abiria maeneo ya Shekilango, manzese, magomeni n.k.
Hakuna usalama, lkini pia mabasi yenyewe hayakaguliwi na wakaguzi wa mabasi yaani vehicle inspectors.
 
1. Kuingia Magufuli kunaepushaje ajali?
2. Umewahi kushuhudia foleni ya kuingia na kutoka mabasi stand ya magufuli?

Nashauri tusirudie urasimu wa Nyerere enzi hizi.
Hiyo stand ni ndogo hawezi kukidhi wingi wa mabasi.

Basi inaweza kuchukua zaidi ya saa moja ikiwa kwenye foleni ya kutoka tu, hii haikubaliki
 
Back
Top Bottom