Dar Es Salaam tumieni maji ya baharini, maji ni mengi sana yale

illegal ya wapi hiyo,kijijini kwetu huko huwa wanavuna maji ya kutosha maelfu ya Lita,nyumba nyingi Zina chemba za maji Tena ya kutosha kabisa...
 
Mimi naona majibu rahisi ya 'aghali sana' bila kufafanua ughali sana wake ni upi, ni majibu ya 'wabunge vihiyo' wanaojibu bila utafiti ama kwa ghilba za ubinafsi.

Maana kuna nchi, hii teknolojia wanayo kitambo sana.

Wao wameweza wana nini na sisi tumeshindwa tunanini?

Maana ingelikuwa ni ghali kama tunavyopotoshwa, waIsraeli wasingelikuwa na ubavu wa kuyachuja kutosheleza hadi ziada ya kumwagilia mashamba.

WaTz ama waAfrika sijui huwa kwanini tunapenda kubweteka hadi akili, maana zamani ilikuwa kuongelea kwa mfano treni za umeme kwenye nchi kama ya kwetu hii, unaonekana mtu kama unaota, lakini kumbe dhamira chanya ikiwepo hakuna linaloshindikana!
 
Nilimtembelea binamu yangu anaishi kijijini. Nilimkuta ana simtank ya litre 10,000 amezungusha gutters bati lote. Ameweka umeme wa solar na ana mtungi wa gas kwa kupikia. Anasema kabla ya litre 10,000 hazijaisha mvua inakua imenyesha tena.
Mkuu hiyo figures za tarakimu nadhani umekosea!

Mimi nina tanki lita 5000 nalitumia karibia siku8, hivyo lita 10,000 almost 2 weeks only!
 
.. Wami ndio tunajenga Daraja jipya kwanza....baada ya Miaka 60 ya Uhuru Mkuu !!
 
Hahahaha sio pow
 
Hili suala ni linawezekana kutumia Yale maji, ishu juu ndiyo hiyo uthbutu wa kuanza hatuna, tunatishika na gharama za uendeshaji
 
Hata tusihangaike na maji ya bahari kwa sababu ni gharama kuyafanya yawe safi...

Tunaweza tukafanya vitu viwili vya uhakika...
1. Kuvuna maji ya mvua na kuyatumia wakati kunapotokea uhaba wa maji ya mto

2. Matumizi ya visima virefu sababu mikoa ya Dar na Pwani yana maji chini ya ardhi
 
Kwa mvua tunazopata Tanzania, hatuhitaji kuingia gharama hizo, kwanza wananchi wahamasishwe kupanda miti hata mijini, moja ya faida za miti ni kuleta mvua.

Water reservoirs kujengwa zikusanye maji ya kutosha hata miaka miwili mvua ikikosekana.
 
Yule dada alietoa ushuhuda wa Hamza alienda kujisaidia baharini, nikukumbushe
 
Ruvu na Wami ni mbali, yale maji ya Jangwani yanoyozuia watu kwenda makazini yale yangekwenda kwenye reservoir mbona yangeleta mabadiliko chanya.
Jumlisha na Bonde la mto Mzinga ambalo maji yake hupotea baharini kupitia kijichi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…