Hivi kweli suluhu ya maji ya Jangwani, Dar es Salam ni daraja?

CORONAZ

Senior Member
Apr 26, 2020
181
337
Nimekuwa nikisoma na kusikia mipango ya serikali kuwa wanataka kujenga daraja kutoka Magomeni Mapipa mpaka fire.

Swali, huo ni ufumbuzi wa mafuriko hayo?

Kwanini hawajiulizi kuwa hayo maji nini kinayazuia yasiende baharini? Kwanini usichimbwe mtaro mpana nyuma ya Muhimbili ukaungana na salenda ili maji yaingie baharini?

Mito mingi ya Dar imezibwa isiishie baharini.

Wazee wa mipango miji, hamlioni hili?
 
Samahani mkuu....
Huko jangwani, salenda na faya ndio maeneo gani hapa Shinyanga??
 
Nimekuwa nikisoma na kusikia mipango ya serikali kuwa wanataka kujenga daraja kutoka magomeni mapipa mpaka fire.
Swali, huo ni ufumbuzi wa mafuriko hayo?

Kwanini hawajiulizi kuwa hayo maji nini kinayazuia yasiende baharini? Kwanini usichimbwe mtaro mpana nyuma ya muhimbili ukaungana na salenda ili maji yaingie baharini?

Mito mingi ya dar imezibwa isiishie baharini.

Wazee wa mipango miji, hamlioni hili?
Hilo daraja litajengwa na kingo hadi huko salenda ndio maana wanasema patakuwa ni enel la kitalii pia.
 
fikra za CCM ndipo zinapoishia hapo mkuu, always wanatafuta short za kuondoa lawama.
 
Back
Top Bottom