Dar Es Salaam tumieni maji ya baharini, maji ni mengi sana yale

May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
4,696
2,000
Leo nimesikia kwenye habari ya kuwa Mikoa ya Dar Es Salaam na Pwani watarajie upungufu wa maji kutokana na kina cha maji ya Mto Ruvu kupungua.

Mwanamuziki Bob Marley kwenye wimbo wake wa 'Rat race' kuna mstari anasema "in the abudance of water the fool is thirsty"...na maandiko yanasema "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa".

Nimekuwa najiuliza hili kwa miaka mingi kuhusu yale maji ya baharini, ni maji mengi sana yasiyotarajiwa kuisha milele...Miaka ya nyuma niliwahi kumsikia Mwanasayansi au Mwanasiasa sikumbuki vizuri wa hapa kwetu akisema teknolojia ya kusafisha maji yale ni ghali sana, nikajisemea 'ala' sasa ikiwa ghali ndio tupande vitandani tuchape usingizi tusubiri miujiza?.

Mambo duniani hufanywa kwa mikakati, kama tuna Wanasayansi nchini basi tuwawezeshe washinde maabara usiku na mchana mpaka wapate jibu, waje na teknolojia rahisi ya kuwezesha kutumia maji ya baharini kwa matumizi ya kila siku ya kibinaadamu na kilimo.

Marekani waliweka tu mikakati kuhakikisha Binaadamu anafika kwenye mwezi na ikawa...Hata chanjo ya corona ni mikakati tu baada ya Binaadamu kuwa cornered.

Tusisubiri kila jibu litoke kwa Binaadamu wengine ili hali hata sisi ni Binaadamu.
 
aise

JF-Expert Member
May 16, 2018
2,610
2,000
Wakati ule ndiyo nakuja mjini kwa mara ya kwanza, nilienda baharini nikashinda huko kutwa nzima, sasa nikawa na kiu na niko ufukweni mwa bahari, nikijua maji yake ni sawa tu na yale ya Ziwa Tanganyika, nikainama ili ninywe,
Loh! kumbe yana chumvi zaidi ya Uvinza.
 
Kwa sasa sio chumvi tu, binaadamu tumeshayajaza sumu za kila aina..kiufupi ni machafu sana yanahitaji kutibiwa kisawasawa ndio yamfae binaadamu.
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
52,989
2,000
Mkuu huko ni mbali sanaaaaa, ku purity maji ya bahari na kuyaondoa chumvi wakati tuu kujenga water tanks za ku tape maji ya mito wakati wa masika ni kimbembe??
Hii process ya kutoa chumvi katika maji ya bahari ni ghali, Dubai wamefanikiwa lakini gharama ni kubwa.
 
Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
14,945
2,000
Hivi Dar es Salaam na Pwani kuna water reservoirs ngapi? Maji ya mvua huwa kuna jitihada za kuyakusanya na kuyasafisha?
Hilo nalo ni la kulifikiria. Miji mingi mikubwa ya wenzetu hupata maji toka kwenye reservoirs. Lakini Dar wanategemea yanayoflow mtoni. Na karibu miji yote Bongo wanategemea hivyo. Walau Moro wana Mindu. Dar wangeweza hata kudam Ruvu au Wami na kusahau shida ya maji.
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
24,581
2,000
Mkuu huko ni mbali sanaaaaa, ku purity maji ya bahari na kuyaondoa chumvi wakati tuu kujenga water tanks za ku tape maji ya mito wakati wa masika ni kimbembe??
ni kazi yenye gharama kubwa kuliko kuangalia namna nyingine.
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
52,989
2,000
Maji ni biashara inayouzika mno kwani maji ni uhai. Wakati Muingereza bado yupo Tanzania maji yalitoka kila sehemu aliyojenga miradi ya maendeleo.
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
52,989
2,000
Hilo nalo ni la kulifikiria. Miji mingi mikubwa ya wenzetu hupata maji toka kwenye reservoirs. Lakini Dar wanategemea yanayoflow mtoni. Na karibu miji yote Bongo wanategemea hivyo. Walau Moro wana Mindu. Dar wangeweza hata kudam Ruvu au Wami na kusahau shida ya maji.
Ruvu na Wami ni mbali, yale maji ya Jangwani yanoyozuia watu kwenda makazini yale yangekwenda kwenye reservoir mbona yangeleta mabadiliko chanya.
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
24,581
2,000
Leo nimesikia kwenye habari ya kuwa Mikoa ya Dar Es Salaam na Pwani watarajie upungufu wa maji kutokana na kina cha maji ya Mto Ruvu kupungua.

Mwanamuziki Bob Marley kwenye wimbo wake wa 'Rat race' kuna mstari anasema "in the abudance of water the fool is thirty"...na maandiko yanasema "Watu wangu wnaangamia kwa kukosa maarifa".

Nimekuwa najiuliza hili kwa miaka mingi kuhusu yale maji ya baharini, ni maji mengi sana yasiyotarajiwa kuisha milele...Miaka ya nyuma niliwahi kumsikia Mwanasayansi au Mwanasiasa sikumbuki vizuri wa hapa kwetu akisema teknolojia ya kusafisha maji yale ni ghali sana, nikajisemea 'ala' sasa ikiwa ghali ndio tupande vitandani tuchape usingizi tusubiri miujiza?.

Mambo duniani hufanywa kwa mikakati, kama tuna Wanasayansi nchini basi tuwawezeshe washinde maabara usiku na mchana mpaka wapate jibu, waje na teknolojia rahisi ya kuwezesha kutumia maji ya baharini kwa matumizi ya kila siku ya kibinaadamu na kilimo.

Marekani waliweka tu mikakati kuhakikisha Binaadamu anafika kwenye mwezi na ikawa...Hata chanjo ya corona ni mikakati tu baada ya Binaadamu kuwa cornered.

Tusisubiri kila jibu litoke kwa Binaadamu wengine ili hali hata sisi ni Binaadamu.
chukua chumvi robo kilo hapo mkoani,itie kwenye kikombe chenye maji nusu rita changanya,kisha koroga uonje.

chumvi uliyosikia ndio kiwango kilichopo ktk maji ya baharini,huwezi kuyafanyia chochote hayo.

kama uko porini umechoma nyama,na ukawa nayo,unaweza yatumia kama chumvi bila kuhisi kitu chochote kupungua.
 
iam Lucha

JF-Expert Member
Aug 24, 2018
2,907
2,000
Wakati ule ndiyo nakuja mjini kwa mara ya kwanza, nilienda baharini nikashinda huko kutwa nzima, sasa nikawa na kiu na niko ufukweni mwa bahari, nikijua maji yake ni sawa tu na yale ya Ziwa Tanganyika, nikainama ili ninywe,
Loh! kumbe yana chumvi zaidi ya Uvinza.
Sisi wazamiaji wa meli wa enzi hizo kuelekea USA tunajua Ukiwa baharini ukaona hata unakaribia kufa kwa kiu kwa vyovyote vle usijaribu kuyanywa maji ya bahari ndo yatakusababishia kufa haraka zaidi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom