Dar es Salaam ili uende kazini na kurudi lazima uandae elfu 10 ya usafiri pamoja na chakula. Maskini hana chake hapa nchini

Sema na kuishi mbali sana jau,
Hapo mkuu kama hio ratiba ni kweli nakuonea huruma,

Sometimes tunakimbilia viwanja vya bei rahisi ila mara mia ulipe pesa kubwa upate sehemu nzuri sio kujificha huko porini.
Una hoja mkuu, ila jiji linakua hili kuna kipindi pori litatoweka jijini
 
Naandika hii mada nikiwa na uchungu moyoni.

Sasa hivi nina miezi kama 4 hivi natumia Daladala kwenda na kurudi kazini na mara chache, tena chache sana huwa natumia bodaboda kazini mpaka home, home mpaka kazini.

Kutoka Nyumbani mpaka kazini nikipanda bodaboda direct ni elfu 15. Go and return inalala 30000 sh
Nikipanda bodaboda 1500 sh. mpaka kituo cha Daladala na nikipanda Daladala moja mpaka kazini awali nilikuwa natumia 1000 sh. Jumla 2500 sh, kwenda na kurudi natumia sh. 5000 kamili, nikipanda gari mbili nilikuwa natumia kama elfu 6 hivi. Pesa ambayo himilivu kwangu.

Ila sasa nikipanda Daladala itanilazimu nitumie takribani 7000 kwenda na kurudi.

Hapo ukiweka na chakula na maji around 5000.

Kwahiyo Mimi tu inabidi nitumie angalau elfu 12 kwaajili ya kazini. Familia kwa sasa hali ilivyo kwa siku ni sh. 10 -20 hapo mahitaji yote muhimu kama gas, mkaa, chumvi, Michele na unga viko ndani. Kama havipo lazima uangushe 20.

Kwahiyo inanilazimu kwa siku nitumie kuanzia elfu 30.

Vipi kwa anayelipwa laki 2.5 au laki tatu kwa Wahindi?

Vipi anayelipwa elfu 7 kiwandani kwa siku?

Kipato changu kidogo nahisi kupata msongo wa mawazo.
Kwa mwezi natumia karibu milioni 1 kwa chakula nyumbani , kazini , usafiri na dharura ndogondogo.
Hapo ukiweka dharura kubwakubwa kama kufiwa na ada za shule watoto mwezi mmoja naangusha zaidi ya milioni.

Serikali ipunguze nauli, watu wanashindia mihogo makazini Ili kubana nauli za kurudia nyumbani jioni.

Hakuna mtumishi wa umma au mwajiriwa wa sekta binafsi Dar es Salaam anaweza kununua kiwanja center labda awe fisadi. Wengi tunajuchanga tunapata viwanja Chanika, Bagamoyo, Kisarawe, Pugu n.k.

Kwa nauli hizi Ili ugeuke na gari upate seat lazima ujipange. Unakuta kila ukipiga hesabu 20 imeenda kwa usafiri na misosi.

Umaskini utaendelea kutupiga maana hatuna mtetezi.
pole chief
 
sasa mkuu huko Kimara na Maramba si ni yale yale tu, bora useme Keko, Chang'ombe, Magomeni, Kinondoni, Manzese nk.

Lakini pia mkuu, hakuna anayependa kuishi Kibaha ndanindani, umasikini mkuu, jamii ya kubwa ya Watanzania ni masikini.
Vipi anaekaa Bunju halafu anafanyia kazi kariakoo au posta?
 
Dar hii wapi watu wana maeneo makubwa? Viwanja vyetu ni hivi hivi 400sqm -700sqm,

Halafu kama una madeal mengi huko kibaha basi utakuwa huna haja ya kulalama nauli
Huyu mwamba kama ameamua kukaa mashambani sijui kwa nini analalamika! Nilitegemea aseme anaziba mapengo mengine kwa kulima ili mahitaji mengine yatoke shambani. Kama mke hana kazi kwa nini anamwacha afuge tako tu badala ya kulima mazao madogo madogo hapo nyumbani? Ni aibu familia iko Kibaha inashindwa hata kuweka mchicha!
 
Mzee kituo Gani cha polisi nikanunue boda boda
Vituo vyote vikubwa vya polish unavyovijua wewe kwa hapa dar au nje y dar wanauza pikipiki.

Kwa kuorodhesha.
Polisi kiluvya gogoni
Polisi stakishari
Polisi ostebay
Polisi central
Polisi kibaha
Polisi buguruni
Polisi mabatini K/nyama
Polisi Tazara hapo ndiyo Kama sagulani

NB: Kuna kuwaga na minada na unaweza kununua nje ya minada.
HAKUNA boda ambayo utauziwa M.

Kumbuka.
Hizi boda zinazouzwa polisi ni zile ambazo zimekamatwa kwenye matukio ya ki uhalifu na wahusika wamekimbia/wametelekeza vyombo vyao.
Au zile ambazo zilipata ajali na wenye Nazo wamezitelekeza.
 
JF kila mtu matawi..et natumia 15k kwenda kazini na kurudi mara chache dalaladala huwa natumia daladala..humu mnatupanga sana kama una uwezo wa kutumia 15k unalalamika nini hiyo nauli? Au ndo kipato chako laki 2.5 unajifanya unasemea wengine?
Hizi ndio roho za kimasikini za wabongo tunazozisema kila siku yani ukipiga hesabu ya matumizi ya mtoa mada kwa haraka haraka ni kama 1M kwa mwezi, je vipi kama mshahara wake ni 1.2M huo ni mshahara wa kawaida sana watu wengi tu humu maofisini wanalipwa hiyo, sasa sijui wewe mwenzetu ulijua huo mshahara ni mkubwa sana na wanaolipwa ni wachache au ulijua wanaotumia jf wote ni masikini sana
 
Boda boda mpya 1lt inapiga 50Km
Ikishakuwa chakavu inapiga 35-42Km
Ukienda kuibana cableta inapiga 55-60Km

Kwa rate hiyo mtu unaweza kukaa bunju na kufanya kazi kariakoo kwa Lita 1 tu go and return ambayo ni 3200 per lita.

Kwa common sense kutoka bunju had kariakoo huwezi kumkosa abiria hata 1 ambaye ukimuambia akupe buku 5 au buku nne hawezi kukataa.
Sasa ukipiga hesabu umeenda na kichwa kimoja kakupa elfu 4 means kakulipia hela ya mafuta.

Kurudi umepata kichwa kingine kakupa buku 4 means umepata hela ya msosi kazini.

Kwa mantiki hii hautakuwa na kuhangaika na mshahara wako.

Note. Service za boda boda siyo ghali na kubwa kinachotakiwa ni kubadilisha oil kila baada ya week 2 au siku 10. Na hiyo oil ni buku ,8-10

Kwa boda boda ambayo private haiwezi kupata hitilafu.

Bei ya boda boda, polisi unaweza kuuziwa kuanzia laki 5-9.

Za mtaani kuanzia laki 8-2M
Ukienda dukani jipange na 2.6-3.1M

Kupanga ni.kuchagua.
Mkuu,
Niwie radhi hii comment yako sikuiona. Kweli kupanga ni kichagua!!
 
Sema na kuishi mbali sana jau,
Hapo mkuu kama hio ratiba ni kweli nakuonea huruma,

Sometimes tunakimbilia viwanja vya bei rahisi ila mara mia ulipe pesa kubwa upate sehemu nzuri sio kujificha huko porini.
Ahamie eneo karibu na kazini mbona kama Dar vyumba bei rahisi viko kibao sehemu ambayo unapanda basi moja tu
 
Hili suala wengi hawazingatii, wewe unalipwa laki tatu halafu unakaa kilomita 45-50 mbali na kazini utakuwa maskini mpaka uzeeni... kaa mbali kama una usafiri wako nje ya hapo unazingua
Wengine shida ujuaji mwingi anataka lazima ajenge
Badala ya angepanga nyumba bei rahisi angebaki Hadi na chenji na kwenda na kurudi kazini akiwa na furaha
 
Sometimes tuache kulalamikia serikali kila siku,

Wew unajua una kazi ya kudumu kkoo,
Unaenda nunua na kujenga nyumba huko kibaha kwa mfipa tena ndani kabisa, unataka serikali ifanyaje ?
Sometimes tusikwepe majukumu yetu na uzembe wetu wa kupiga hesabu, mtoa mada angejua maisha yake pengine angejichanga zaidi apate kiwanja karibu na kazini
Kwahyo umeona mfano wako uuweke kwa mfipa tu mkuu unatuonaje wa kwa mfipa??
 
Back
Top Bottom