Dar: Askari walioiba Tsh. Milioni 90 kwa kutumia Silaha wafutwa kazi, washtakiwa upya kama Raia huru

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,473
8,322
1698987518734.png

Upande wa Jamhuri umelazimika kubadili hati ya mashtaka dhidi ya waliokuwa Maafisa wa Jeshi la Polisi kwa kuondoa namba za Utambulisho wao ambazo ni F 7149 D/ Coplo Ramadhani (42), G. 7513 D/ Coplo Majid Abdallah na WP 6582 D/ Coplo Stela Mashaka ambapo sasa wameshtakiwa kwa majina yao halisi bila ajira za Kipolisi.

Awali, wote kwa pamoja wakiwa Waajiriwa na Jeshi la Polisi kwa nafasi za Askari Kanzu (Askari Wasiovaa Sare za Jeshi) wenye vyeo vya Koplo, walifikishwa Mahakamani Oktoba 31, 2023 na kusomewa shtaka moja la ungang’anyi wa kutumia Silaha .

Agosti 28, 2023 katika eneo la Kurasani, karibu na ofisi za Uhamiaji, Ilala, kwa pamoja Washtakiwa waliiba Tsh. Milioni 90 kutoka kwa Grace D. Matage baada ya kumtishia Bunduki. Hata hivyo wamekana Mashtaka na kurudishwa Mahabusu kwasababu kosa hilo halina dhamana na kesi imeahirishwa hadi Novemba 13, 2023.

==============

Serikali imefanya mabadiliko katika hati ya mashtaka ya shitaka linalowakabili maofisa watatu wa Jeshi la Polisi kwa kuondoa namba zao za utambulisho wa ajira.

Maofisa hao wanakabiliwa na shtaka moja la unyang’anyi wa kutumia silaha na kuiba Sh90 milioni, mali ya Grace Matage.

Kufuatia mabadiliko hayo, sasa hati mpya ya mashtaka itasomeka kama waliokuwa askari Polisi, baada ya kuvuliwa namba zao za utambulisho wa ajira na wamefukuzwa kazi na mwajiri wao, ambaye ni Jeshi la Polisi.

Wakili Serikali, Erick Kamala amewataja washtakiwa hao, kuwa ni Ramadhani Tarimo (42) maarufu kama Rasta na mkazi wa Kipawa;Majid Abdallah (35) mkazi wa Kunduchi na Stela Mashaka, ambao wote walikuwa waajiriwa na jeshi la Polisi na walikuwa askari kanzu wenye vyeo vya koplo.

Itakumbukwa kuwa Oktoba 31, 2023, washtakiwa hao walifikishwa mahakamai hapo na kusomewa shtaka moja la ungang’anyi wa kutumia silaha pamoja namba zao za utambulisho wa ajira kutoka jeshi hilo la Polisi.

Siku hiyo, washtakiwa hao walisomewa majina na mamba zao ambazo ni F 7149 D/ Coplo Ramadhani (42) maarufu kama Rasta; G. 7513 D/ Coplo Majid Abdallah (35) mkazi wa Kunduchi na WP 6582 D/ Coplo Stela Mashaka.

Wakili Kamala, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Alhamsi Novemba 2, 2023, kuwa kesi hiyo ililetwa kwa ajili ya upande wa mashtaka kufanya mabadiliko ya hati ya mashtaka kwa kuondoa namba zao za ajira askari hao.

Kamala amedai mbele ya hakimu Mkazi Mkuu, Amiri Msumi, kuwa upande wa mashtaka unaomba kufanya mabadiliko katika hati ya mashtaka chini ya kifungu namba 234(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), sura ya 20, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

Wakili Kamala baada ya kueleza hayo, aliwasomewa upya shtaka lao, ikiwemo majina yao bila kutaja namba zao za ajira.

Akiwasomewa shtaka lao, wakili Kimala, alidai kuwa washtakiwa wanakabiliwa na kesi ya jinai namna 197/2023.

Alidai washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo, Agosti 28, 2023 katika eneo la Kurasani, karibu na ofisi za Uhamiaji, lililopo wilaya ya Ilala, ambapo siku hiyo ya tukio, washtakiwa kwa pamoja waliiba Sh90 milioni kutoka kwa Grace Donald Matage.

Ameendelea kudai mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao kabla na baada ya kufanya wizi huo, walimtishia Grace kwa bunduki ili waweze kujipatia fedha hizo bila kikwazo.

Washtakiwa baada ya kusomewa shtaka linalowakabili walikana.

Upande wa mashtaka wamedai kuwa bado wanaendelea na upelelezi wa shauri hilo, hivyo wanaiomba Mahakama hiyo, ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Msumi amewaambia washtakiwa hao, kuwa shtaka linalowakabili halina dhamana kwa mujibu wa sheria hivyo, wataendelea kubaki rumande.

Baada ya kueleza hayo, aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 13, 2023 itakapotajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande.

MWANANCHI
 
Ramadhani Tarimo (42) maarufu kama Rasta na mkazi wa Kipawa;Majid Abdallah (35) mkazi wa Kunduchi na Stela Mashaka, ambao wote walikuwa waajiriwa na jeshi la Polisi na walikuwa askari kanzu wenye vyeo vya koplo.
Kutaja majina kunaweza kuamsha mjadala mwingine wa uonevu
 
View attachment 2801995

Pesa ndefu ina rahaa yake, na vile vile ina karahaa zake! Mradi tu uwe tayari kuvumilia kwa lolote lile litakalotokea huko mbeleni!!!
 
Polisi wengi ni matapeli,wanyang'anyi

Akikuhisi tu una hela mfukoni anaweza kukudhuru akusingizie wewe ni jambazi akuue,kisha achukue hizo pesa

Hili jeshi lifumuliwe,liboreshwe

Wafungwe hao
 
Back
Top Bottom