Dangote: Ni laana au hasara kwa wanaomfuata?

Dangote: Ni laana au hasara kwa wanaomfuata?

Ni kampuni imbayo ilivumishwa kama mwokozi kwa mnyonge. Sementi zake zingeuzwa sh. 5000 soon. Leo zinauzwa 15000. Mbaya zaidi, kampuni ya Dangote inatuhumiwa kwa kukwepa kodi na pia kuwanyanyasa wafanyakazi

Mbaya zaidi, kampuni ya Dangote Haina mchango wowote kwa jamii. Vijiji vya jirani na Dangote, havina, maji, wala umeme. Wala hakuna huduma za Afya huku ardhi yao kubwa sana imechukuliwa na kampuni hii ya cement. Je Dangote inafaida gani kwa watanzania?
Jamani, si ndio kwanza wanaanza uzalishaji! Wapeni muda.
 
Ni kampuni imbayo ilivumishwa kama mwokozi kwa mnyonge. Sementi zake zingeuzwa sh. 5000 soon. Leo zinauzwa 15000. Mbaya zaidi, kampuni ya Dangote inatuhumiwa kwa kukwepa kodi na pia kuwanyanyasa wafanyakazi

Mbaya zaidi, kampuni ya Dangote Haina mchango wowote kwa jamii. Vijiji vya jirani na Dangote, havina, maji, wala umeme. Wala hakuna huduma za Afya huku ardhi yao kubwa sana imechukuliwa na kampuni hii ya cement. Je Dangote inafaida gani kwa watanzania?

Kwahiyo?
 
Haya mawazo ya watu kufikiria kwamba mwekezaji akiwekeza sehemu ni lazima alete MAJI na UMEME sijui hasa hua tunatoa wapi? Utasikia, sehemu zilizo na migodi eti wenye migodi ndio wafanye hizo kazi; hivi serikali kazi yake ni nini? Yaani ichukue kodi kwa mwekezaji na halafu mwekezaji aanze kuwahudumia wananchi ambao kimsingi hao wananchi ni mali ya nchi na sio mwekezaji.
Suala la Dangote kukwepa KODI(kama ni kweli lakini) huo ni uzembe wa serikali yenyewe, ninailaumu serikali kwa kuwawezesha wawekezaji kukwepa KODI na pia kuwaruhusu Wawekezaji kuleta wafanyakazi toka nje ya nchi. Nafasi kama Boiler makers (Welders) mechanical engineering, Uhasibu, ugavi/procurements hatuhitaji hata mtu 1 kutoka nje ya nchi, tunavyo vyuo vya kutosha vya kutengeneza watu wenye sifa za aina hiyo.
 
Mkuu sio serikali yangu,ni serikali yetu,hayo magari ya dangote yanaendeshwa na wanigeria? Afu bakhresa ametoka wapi tena,acha kubadili gia,katika hii generation utawashangaza wengi ukisema kwamba automation ni unyonyaji,elewa technology ndio inaendesha dunia ewe wild beast,sasa unamlaumu dangote kujitengenezea umeme afu unataka dangote asitumie technology eti kisa aajili watu wengi!..ubongo umempa nani akushikie!?
Kampa Yericko na CDM
 
Hiyo kampuni tangu imeanza kufanya kazi Ina MDA gani wazee WA mapovu
Swala sio muda, ila makubaliano yalisemaje..
Unajua tofautisha akili yako unapokuwa kule fcbk kwa low thinkers na unapokuja huku jf kwa great thinkers..
 
Mleta mada inaweza ikawa ni mteja wa twiga bado hajasurrender kwa dangote subr utamsoma tz itakuja kuwa dangote peke yake huyu jamaa anahistoria akishaingia sokoni huwa ni balaa viwanda vingne vyote ni chali
 
Hebu kwanza tuoneshe ni wapi Dangote walisema sementi yao watauza 5,000/=? Au unakumbuka 2010 Dr. Slaa alipogombea urais kupitia chadema, waliomtema, alipoahidi kuwa akichaguliwa kuwa Rais sementi itakuwa 5,000 tu?

Hilo la kusaidia vijiji vya jirani, hiyo ni sadaka na utoapo kulia haitakiwi hata kushoto ielewe na pia si lazima. Dangote hakuja kuwekeza ili atoe misaada.

Halafu huo mfuko wa sementi wa 15,000 upo mkoa upi wa Tanzania?
 
Ndo unajua leo!me cku nimezaliwa tu kujikuta niko bongo nikaanza kulia

Hahahahahaaaaaaaaaaaaaa, umenichekesha. Kuna aliyeniambia Bwana Mungu baada ya kuumba Tanzania akaitazamaaaa kisha akaanza kuangua kicheko!
 
Mbona tulishasema kitambo sana humu ? Hivi kuna aliyedhani ccm ina huruma na mtu ! Basi nimpe pole , subirini mjengewe matundu manne ya vyoo vya soko hapo nanjilinji viwasaidie .
Chadema mna mabilionea wa Tanzania wengi sana, kwanini hamuoneshi mfano wa kujenga kiwanda mkauza sementi 5,000?

Ya nini mnaandikia mate na wino upo?
 
Chadema mna mabilionea wa Tanzania wengi sana, kwanini hamuoneshi mfano wa kujenga kiwanda mkauza sementi 5,000?

Ya nini mnaandikia mate na wino upo?
Hivi wewe kuna siku unatumiaga akili kidogo kuongea mambo ya maana kweli?
 
Ni kampuni imbayo ilivumishwa kama mwokozi kwa mnyonge. Sementi zake zingeuzwa sh. 5000 soon. Leo zinauzwa 15000. Mbaya zaidi, kampuni ya Dangote inatuhumiwa kwa kukwepa kodi na pia kuwanyanyasa wafanyakazi

Mbaya zaidi, kampuni ya Dangote Haina mchango wowote kwa jamii. Vijiji vya jirani na Dangote, havina, maji, wala umeme. Wala hakuna huduma za Afya huku ardhi yao kubwa sana imechukuliwa na kampuni hii ya cement. Je Dangote inafaida gani kwa watanzania?
Mkuu ungetulia ukafanya utafiti na kuja na analysis nzuri tu. Hiki ulichokisema ni upuuzi, uwongo,na majungu kwa asilimia nyingi sana.
Sina maslahi na hiyo kampuni lakini nimewahi kuishi Mtwara siku za karibuni niliumiza kichwa kidogo. Ngoja nikupe data ujione ulivyo zuzu.
Bei ya mfuko ya sement ya Dangote ni Tsh 13,000/- kwa mfuko mmoja. Hujajua production cost yake. Inaelezwa kuwa mipango ya awali ilikuwa Dangote apewe kitalu/kisima achimbe gas kama chanzo cha nishati. Alipowafuata wenye mamlaka akapewa quotation ya hatari utadhani ananunua dhahabu kwenye soko la dunia. Akaona bora ku-opt kutumia dizeli kuliko hayo ma gas yetu. Ana matank ya diseli ya lita 100,000/- kama 100 hivi opposite na jengo lake la utawala. Ana generators super heavy duty anayotumia kama nishati. Inaelezwa kuwa bado hayo matank yakawa hayampi returns alizotegemea. Akaopt kutumia makaa ya mawe ya Mchuchuma. Figisu zikaanza tena. Kumbuka swahiba wake aliyemleta, Alhaj Jehi Kehi ameshaondoka amekuja huyu wa kusomesha namba. Nasikia na Mchuchuma kachemsha. Sikusikia tena kama aliendelea na dizeli au ilikuwaje. Kwa Tanesco sina haja ya kueleza kwanza angetumia umeme wote wa Lindi na Mtwara na bado usingemtosha. Production cost iko juu sana. Bei ya simenti kufika hapo ni neema pia. Hao wanaokuuzia 15,000/- ni walanguzi.

Ni kweli wafanyakazi wananyanyaswa. Sio Dangote anayefanya hivyo. Dangote ali hire management ya Wahindi kwenye kuajiri na utawala. Ni wahindi ndio mabosi wa wafanyakazi. Sina haja ya kueleza hulka za wahindi lakini wananyanyaswa na Wahindi sio Dangote.

Vijiji havina maji. Hii sijui kama ilikuwepo kwenye mkataba wake na haobwaliompa eneo la kujenga kibanda. Ninachojua ni kuwa pesa za fidia walizokubaliana, Dangote alilipa zaidi ya pesa walizokubaliana. Ni katika hali hiyo, wananchi walikuwa radhi kuachia maeneo yao yaliyo pembezoni mwa bahari ya hindi ili Dangote atumie kwa ajili ya biashara yake. Sikusikia mwanakijiji akimlaumu au kumsema vibaya Dangote. Vijana wote wa Msijute, Mbuo, Mikindani na maeneo jirani wameajiriwa na kampuni ya Dangote ikiwa ni sharti kuwa wenye maeneo jirani wafaidike hata kama ni kazi za vibarua. Mji umebadilika, biashara ndogo ndogo zimeibuka pale, mama lishe wanatunza familia zao kuliko awali kutokana na influx ya watu.

Ni laana tumepewa Watanzania ya kulaumu tuuuuuu. Jitu linakaa nyuma ya keyboard linalaumuuu ukiliuliza, umefanya utafiti? Hajui hata anatakiwa afanye nini. Ni vizuri kufanya utafiti kwanza kabla ya kukurupuka kumwaga uharo humu
 
Vuta subira mkuu kwani wameanza uzalishaji wa saruji karibuni tu. Baadaye watakaporudisha gharama za uwekezaji (mtaji) wataanza kutoa hizo huduma za jamii. Shida yetu WATANZANIA tunapenda vitu viende fasta fasta kila mahali.
Ukishafika huo muda wanatangaza hasara na kusepa.
 
Ni kampuni imbayo ilivumishwa kama mwokozi kwa mnyonge. Sementi zake zingeuzwa sh. 5000 soon. Leo zinauzwa 15000. Mbaya zaidi, kampuni ya Dangote inatuhumiwa kwa kukwepa kodi na pia kuwanyanyasa wafanyakazi

Mbaya zaidi, kampuni ya Dangote Haina mchango wowote kwa jamii. Vijiji vya jirani na Dangote, havina, maji, wala umeme. Wala hakuna huduma za Afya huku ardhi yao kubwa sana imechukuliwa na kampuni hii ya cement. Je Dangote inafaida gani kwa watanzania?
Wewe unaishi mkoa gani huko inakouzwa elf 15?Hapa Tanzania (Dar),inauzwa elf 11 tu
 
Inaelezwa kuwa mipango ya awali ilikuwa Dangote apewe kitalu/kisima achimbe gas kama chanzo cha nishati. Alipowafuata wenye mamlaka akapewa quotation ya hatari utadhani ananunua dhahabu kwenye soko la dunia. Akaona bora ku-opt kutumia dizeli kuliko hayo ma gas yetu. Ana matank ya diseli ya lita 100,000/- kama 100 hivi opposite na jengo lake la utawala.
Mkuu umeeleza vizuri sana ila hapo nilipoQuote fuatilia kidogo.

Dangote hakuwahi kuahidiwa kupewa kisima cha gesi na hakuwahi kuomba.
Ila alipanga kutumia Gesi kwa ajili ya mitambo yake na hadi leo yuko hatua za mwisho kukamilisha mitambo yake ya kutumia gesi (ataanza kuiendesha Sept.kwa mjibu wake).

ISSUE: iliyopo ni BEI YA GESI jamaa anataka auziwe gesi kwa bei ya chini kabisa hata kuliko ile Tanesco anayonunulia, japo bado wako kwenye majadiliano ya bei. Kwa namna nyingine anajipangia bei.
 
Back
Top Bottom