Dangote: Ni laana au hasara kwa wanaomfuata?

Dangote: Ni laana au hasara kwa wanaomfuata?

Ni kampuni imbayo ilivumishwa kama mwokozi kwa mnyonge. Sementi zake zingeuzwa sh. 5000 soon. Leo zinauzwa 15000. Mbaya zaidi, kampuni ya Dangote inatuhumiwa kwa kukwepa kodi na pia kuwanyanyasa wafanyakazi

Mbaya zaidi, kampuni ya Dangote Haina mchango wowote kwa jamii. Vijiji vya jirani na Dangote, havina, maji, wala umeme. Wala hakuna huduma za Afya huku ardhi yao kubwa sana imechukuliwa na kampuni hii ya cement. Je Dangote inafaida gani kwa watanzania?
Majungu, Wivu na uongo kiwango cha lami
 
Hahahahahaaaaaaaaaaaaaa, umenichekesha. Kuna aliyeniambia Bwana Mungu baada ya kuumba Tanzania akaitazamaaaa kisha akaanza kuangua kicheko!
Kuna mwingine eti africa ingekuwa binadam tz ingekuwa matako.hahaha
 
Godfather alisema vijana wanalalamika bila kutoa njia mbadala
 
Ukweli ni upi? leta habari !
Lini walitangaza cement itauzwa 5,000?
Ni sehem gani hiyo cement inauzwa 15,000?
Je, Dangote ana muda gani tangu aanze kuzalisha cement? Hii ni biashara sio NGO mkuu ya kusaidia
Katoa ajira kiasi gani hapo?

Jamaa ameajiri watu kiasi chake japo kuna ukandamizaji unaotokana na management ya kiwanda, pili ananunua Gypsum kutoka kwa wachimbaji wadogowadogo kutoka Ruangwa (Lindi) hii yote anaongeza pato kwa wananchi wa sehem hiyo, Bei ya cement yake iko chini kulinganisha na viwanda vingine ambavyo vimekaa sokoni kwa muda mrefu.
Ana mpango wa kujenga Bandari Mtwara kwa ajili ya kupakia na kushusha materials zake, ana mpango wa kuomba kuchimba makaa ya mawe hii yote itatyengeneza ajira za kutosha.

Cha msingi alipe kodi stahiki na kutekeleza majukumu yake ya Corporate Social Responsibility (CSR).

BTW:
Mkuu hakuna muwekezaji anaeweza kukuletea maendeleo kwako kabla hajaona faida ya biashara yake, Dangote hajamaliza hata mwaka unataka akujengee nyumbs ya kuishi, shule, hospitali, visima, Duuh waTZ hatariiii, hv vitu Serikali iliyoko madarakani imekaa miaka 50 haijavileta, unataka Dangote avilete ndani ya miezi 7.
 
Mkuu ungetulia ukafanya utafiti na kuja na analysis nzuri tu. Hiki ulichokisema ni upuuzi, uwongo,na majungu kwa asilimia nyingi sana.
Sina maslahi na hiyo kampuni lakini nimewahi kuishi Mtwara siku za karibuni niliumiza kichwa kidogo. Ngoja nikupe data ujione ulivyo zuzu.
Bei ya mfuko ya sement ya Dangote ni Tsh 13,000/- kwa mfuko mmoja. Hujajua production cost yake. Inaelezwa kuwa mipango ya awali ilikuwa Dangote apewe kitalu/kisima achimbe gas kama chanzo cha nishati. Alipowafuata wenye mamlaka akapewa quotation ya hatari utadhani ananunua dhahabu kwenye soko la dunia. Akaona bora ku-opt kutumia dizeli kuliko hayo ma gas yetu. Ana matank ya diseli ya lita 100,000/- kama 100 hivi opposite na jengo lake la utawala. Ana generators super heavy duty anayotumia kama nishati. Inaelezwa kuwa bado hayo matank yakawa hayampi returns alizotegemea. Akaopt kutumia makaa ya mawe ya Mchuchuma. Figisu zikaanza tena. Kumbuka swahiba wake aliyemleta, Alhaj Jehi Kehi ameshaondoka amekuja huyu wa kusomesha namba. Nasikia na Mchuchuma kachemsha. Sikusikia tena kama aliendelea na dizeli au ilikuwaje. Kwa Tanesco sina haja ya kueleza kwanza angetumia umeme wote wa Lindi na Mtwara na bado usingemtosha. Production cost iko juu sana. Bei ya simenti kufika hapo ni neema pia. Hao wanaokuuzia 15,000/- ni walanguzi.

Ni kweli wafanyakazi wananyanyaswa. Sio Dangote anayefanya hivyo. Dangote ali hire management ya Wahindi kwenye kuajiri na utawala. Ni wahindi ndio mabosi wa wafanyakazi. Sina haja ya kueleza hulka za wahindi lakini wananyanyaswa na Wahindi sio Dangote.

Vijiji havina maji. Hii sijui kama ilikuwepo kwenye mkataba wake na haobwaliompa eneo la kujenga kibanda. Ninachojua ni kuwa pesa za fidia walizokubaliana, Dangote alilipa zaidi ya pesa walizokubaliana. Ni katika hali hiyo, wananchi walikuwa radhi kuachia maeneo yao yaliyo pembezoni mwa bahari ya hindi ili Dangote atumie kwa ajili ya biashara yake. Sikusikia mwanakijiji akimlaumu au kumsema vibaya Dangote. Vijana wote wa Msijute, Mbuo, Mikindani na maeneo jirani wameajiriwa na kampuni ya Dangote ikiwa ni sharti kuwa wenye maeneo jirani wafaidike hata kama ni kazi za vibarua. Mji umebadilika, biashara ndogo ndogo zimeibuka pale, mama lishe wanatunza familia zao kuliko awali kutokana na influx ya watu.

Ni laana tumepewa Watanzania ya kulaumu tuuuuuu. Jitu linakaa nyuma ya keyboard linalaumuuu ukiliuliza, umefanya utafiti? Hajui hata anatakiwa afanye nini. Ni vizuri kufanya utafiti kwanza kabla ya kukurupuka kumwaga uharo humu

Umetoa analysis nzuri ila umekose kukubaliana na mtoa mada!!! Cement ya Dangonte haiuzwi 15000 hasa miloa hii ya jirani, mimi nauza Cement nipo Kibaha nauza rejareja 11500 na 11000 kwa mtu anayechukua zaidi ya mifuko 50. Haiwezekan ikauzwa 15000 Lindi au Mtwara.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Morogoro bei za cement leo tar 23/6/2016
-Twiga 12,800/=
-Nyati 12,800/=
-Dangote 12,700/=
 
Ni kampuni imbayo ilivumishwa kama mwokozi kwa mnyonge. Sementi zake zingeuzwa sh. 5000 soon. Leo zinauzwa 15000. Mbaya zaidi, kampuni ya Dangote inatuhumiwa kwa kukwepa kodi na pia kuwanyanyasa wafanyakazi

Mbaya zaidi, kampuni ya Dangote Haina mchango wowote kwa jamii. Vijiji vya jirani na Dangote, havina, maji, wala umeme. Wala hakuna huduma za Afya huku ardhi yao kubwa sana imechukuliwa na kampuni hii ya cement. Je Dangote inafaida gani kwa watanzania?
Cement ya Dangote tumetangaziwa inauzwa elfu kumi. Sasa hiyo 15000 imekuwaje? Yaani mnataka Dangote awaletee maji na umeme? Yeye kaleta ajira nyie wenyewe ndiyo mboreshe makazi yenu msimuonee baba wa watu. Awape pesa halafu aboreshe makazi yenu? Pesa zenu zinafanya nini?
 
Wewe upo nairobi umejuaje mambo ya mtwara kule...
 
Mkuu umeeleza vizuri sana ila hapo nilipoQuote fuatilia kidogo.

Dangote hakuwahi kuahidiwa kupewa kisima cha gesi na hakuwahi kuomba.
Ila alipanga kutumia Gesi kwa ajili ya mitambo yake na hadi leo yuko hatua za mwisho kukamilisha mitambo yake ya kutumia gesi (ataanza kuiendesha Sept.kwa mjibu wake).

ISSUE: iliyopo ni BEI YA GESI jamaa anataka auziwe gesi kwa bei ya chini kabisa hata kuliko ile Tanesco anayonunulia, japo bado wako kwenye majadiliano ya bei. Kwa namna nyingine anajipangia bei.
Na tusikubali mwekezaji anayetaka kujipangia kila kitu , huu utakuwa ujinga sana
 
Back
Top Bottom