Dangote: Ni laana au hasara kwa wanaomfuata?

Dangote: Ni laana au hasara kwa wanaomfuata?

Hii kampuni Haina maana, wachina ndio watu muhimu kwa Dangote. Umeme wanazalisha mwingi sana pale, kitu ambacho wanakijiji wangesambaziwa kwa bei nafuu hata kwenye shule na zahanati
 
Hana faida maana pale Lindi tunanunua 14500/ mi nikitakA kujenga nanunua nyati maana hata tangazo ni zuri
Mkuu, Lindi 14,500? Sidhan kama ni kweli. Hapa Dar nimenunua kwa Tsh 12000 Tabata -Segerea, iweje Lindi iwe bei ghali hivyo?
 
Hivi ni nani alitangaza saruji itauzwa 5,000/=..?
Je, hicho kiwanda cha Dangote tangu kimeanza kuzalisha saruji kina muda gani sasa..?
Ni sehemu gani huko wanauza saruji 15,000 /=..?
Je hizo huduma kwa jamii zinatokana na faida kwa mwenye kiwanda au zipo ndani ya OC na pia umeshatembelea vijiji vya Msijute, MKunwa, Mbuo, Mnyundo na Mgao siku za karibuni..?
By the way, kiwanda siyo sadaka, jambo hilo ni clear. Cha msingi alipe kodi stahiki na ajira kwa Watanzania ni fursa kwetu. Kwamba Lindi ni bei ghali kuliko Dar hapo bu tatizo la mji wenyewe wa Lindi. Sijajua Lindi kuna shida gani. Wakati fulani nilikaa kama siku tatu nne hivi Lindi. Dereva wa bodaboda mmoja aliniambia huwa wananunua Boxer na Pikipiki za Kichina Mtwara, nikamuuliza kwa nini, akaniambia Mtwara ni bei nafuu kuliko Lindi, nikajiuliza kulikoni wakati Lindi ni karibu kuliko Mtwara, kwa maana kama bidhaa zinaagizwa kutoka Dar, basi kiusafirishaji ingetarajiwa iwe ni bei rahisi. Wakaz wa Lindi waje watuambie kulikoni.

Nikija kwenye mada ya vijiji jirani mkuu ulivyovitaja, je kuna mabadiliko gani ambayo wanavijiji wanaweza kujivunia so far? Angalau pale Msijute kwa kuwa ni Highway, panaanza kunawiri.
 
Amini nnachokuambia maana ile simenti inavyoonekana ikitoka kiwandani ni dar moja kwa moja then ndo inarudi Lindi na mtwara maana DSM ndo kuna mawakala wakuu,
 
Amini nnachokuambia maana ile simenti inavyoonekana ikitoka kiwandani ni dar moja kwa moja then ndo inarudi Lindi na mtwara maana DSM ndo kuna mawakala wakuu,
Kwa Mtwara bei siyo ghali ni 11500
 
Kihistoria pale Lindi ni mji wa kutumia pesa na waliishi watu wenye pesa zao na kipindi hiko palijulikana kwa jina la Paris hadi leo ukienda utaona jinsi palivyopangiliwa vizuri ile mitaa yake kwa pale town tu lakini, sasa hali ile ndo imekuwa hadi leo vitu viko juu sana.
 
Ni kweli 11500 pale mtwara nimeuliza mtu wa mtwara sasa hivi ila kwa Lindi hasa pale kijjn kwangu bei ni 14500 sijui kwa nini
 
Hardware za hapa Mwenge jirani na Lugalo ni 15,000 mpaka 20,000
 
Vuta subira mkuu kwani wameanza uzalishaji wa saruji karibuni tu. Baadaye watakaporudisha gharama za uwekezaji (mtaji) wataanza kutoa hizo huduma za jamii. Shida yetu WATANZANIA tunapenda vitu viende fasta fasta kila mahali.
Tunapenda vitu viende fasta fasta ili viendane na kasi ya Raisi wetu Mtukufu John Joseph Pombe Magufuli
 
Wengi hawajui kuwa hiki kiwanda CCM walikigeuza cha kwao na wakakitumia kupigia kampeni na kikawasaidia na kuwaaminisha watanzania mambo yasiyowezekana ilihali mwenye kiwanda hajapanga bei elekezi,vilevile wajanja wamechukua Chao hapo ndo mana hamna wa kupiga kelele
 
Back
Top Bottom