hahahahhh. Kumbe
king'asti we wa juzi juzi tu. Basi kwa taarifa yako gitaa la solo la huo wimbo lilipigwa na nene tchakou, rythm lokassa ya mbongo na sometimes nene alikuwa akisaidia kuimba. Lakini pia dally kimoko alipiga gitaa la solo kwenye baadhi ya nyimbo kwenye hiyo album, kama ule wimbo wa wallow. Upo hapo?
Duh. Ndugu
ndoa, hiyo album ninayo nzima nzima, niliinunua kariakoo 2005, iko bomba sana. Gitaa la solo kapiga dally kimoko akisaidiwa na caen madoka (kumbuka kwamba hao vijana ni product ya loketo). Kwenye rap za hiyo album yumo
albert
william
longomba (awilo) na aurlus mabele. By then, kila mwanakikundi wa loketo alisaidiwa na kundi kutoa album, kwa hiyo akina mack macaire, jean baron, lutchiana j toto, lucien bokilo, djunny claude, dally kimoko, awilo, mabele na wengineo wote walitoa album kipindi hicho. Umenikumbusha mbali sana. Huwa na enjoy sana hizo nyimbo, ninazo kwenye flash najiburudisha nikiwa na nafasi.