bolingo zilikuwa zamani hakika...
na binafsi yangu ukinitajia Mtindo wa Bolingo ninaoukubali basi sisiti kuutaja mtindo uliitwa Soukous...
Na kama utazungumzia Soukous basi Sokous Stars ndo bendi.
Na miongoni mwa nyimbo za Soukous ninazozikubali basi...
1. Rose
2. Robin pretty
3. Sophia
4. Rhoda.
5. Aba goimo
Kisha ktk kundi la sokous alikuwepo shangazi mmoja alieitwa Yondo Kusala maarufu kama Yondo Sister ambae nae alitamba na vibao kama...
1. Cayina
2. Bazzo
3. Mwana kento
4. Wapi yoo
Na nyingine nyiingi sana.
Halafu pakawepo na mtu alieitwa Luciana Bokilo.
Bokilo yeye alitamba na...
1. Aziza
2. Missete
3. One way.
Kisha akaja kamanda mwingine alieitwa Lokasa ya Mbongo ambae nae akapiga ngoma kali kama...
1. Adiza
2. Marijose
3. Monica.
4. Nairobi night amabao kwa pamoja alishirikiana na makamanda wenzie waliounda Soukous Stars.
Machi/5/1989 katika hotel ya New Morning mjini Paris Mpiga gitaa la Bass Ngouma Lokito akiwa na nguli mwenzie ambae ni mcharaza Gitaa la Rythim Lokasa ya Mbongo walianzisha Band ambayo waliibatiza jina la Soukous Stars.
Miongoni mwa members wengine walikuwemo Paris Shimita,
Yondo Sister, Balu kanta na Zitani Nell.. nyota wengi ktk bara hili kama Manu Dibango, Jacob Desvarieux, Jocelyn Kiambukuta na Sam
Mangwana, walikuwapo siku hiyo.
Kituo kikubwa cha matangazo nchini Ufaransa RFI (Radio France International) walirusha LIVE tukio hilo la kumbukumbu.
Mara moja bendi ikawa na ikaanza kufanya maonesho ya LIVE karibu Duniani kote huku wakishirikiana na nyota wengine Barani Efrica.
Baada ya miaka kadhaa kupita Soukous Stars wakajinyakulia umaarufu wa hali ya juu.
miongoni mwa nyota waliokuwepo ktk kundi hilo ambao walitoka nchi mbali mbali barani Africa ni Yondo Sister, Shimita, Nyomba,
Luciana de Mingongo toka Kinshasa, Democratic
Republic of Congo;.
Kisha wakawepo Ballu Canta, Zitani Nell, Pierre
Belcos, Lucien Bokilo toka Congo Brazzaville;
Saladin Saladin wa Central Africa Republic;
Arsene Kounde toka Benin na Joseph Koujojo toka
Cameroon.
Balantanda njoo uwazungumzie Wenge BCBG walipotoka mpaka walipo sasa.