Dada yake MBOWE aikacha CHADEMA ajiunga na CCM!!

Dada yake MBOWE aikacha CHADEMA ajiunga na CCM!!

Dada yake Mbowe kajitambua, ameona haiwezekani akili ndogo iongoze akili kubwa.

Hongera sana Grace Mbowe.

Kama nyumbani wanamkataa Mbowe, kulikoni.

akili za ccm siku zinawaza utawala wa kifamilia. Baba Mwenyekiti Taifa(Jk), Mtoto uvccm pwani(ritz moko), mama sijui nini tena malizia mwenyewe family member wengine chipukizi ..
CDm mpira tofauti kabisa njoomba ...
 
Amejitambua kuwa yeye hawezikuwa msukule.

Inawezekana Mbowe alitaka ampeleke kwenye vurugu akaona upuuzi.

soon vijana wengi watajitambua pia
Bado tu ugonjwa wako wa akili hujapona tu? Dawa yake ni ndogo tu, rudi kwenu kalenga kamtafute mzee Kidegembasi akutengenezee mchanganyiko wamavi ya kuku na mafuta ya kenge unywe mara tatu kutwa kwa mwezi mmoja, utapata nafuu!
 
Siwezi kushangaa, sababu Mbowe na Chadema ni brand kubwa sana hivi sasa Tanznaia, kwa hiyo kitu chochote chenye uhusiano na chadema bongo ccm wanaweza kulipia fedha yoyote kukipata wakizani kuwa wanaidhoifisha chadema, kumbe wanajikomoa. Sawa na huyo dada, amesha chukua fedha ya ccm ili atangaze hiyo propaganda, lakini haisaidii kitu.
 
Bado tu ugonjwa wako wa akili hujapona tu? Dawa yake ni ndogo tu, rudi kwenu kalenga kamtafute mzee Kidegembasi akutengenezee mchanganyiko wamavi ya kuku na mafuta ya kenge unywe mara tatu kutwa kwa mwezi mmoja, utapata nafuu!

Kweli wew dawa unazifahamu! Yaani huo mchanganyiko atapona magonjwa yote!
 
Yani unamaana Makongoro Nyerere alipojiunga na NCCR na kupata ubunge, Mwenye heri Julius Nyerere alikuwa hana ushawishi kwa level ya familia?
Au coincidence ya Mary Nagu na Jitu Son au Anna Tibaijuka na Kikwete ni ushawishi wa kifamilia?


ndio nyerere hakuwa na ushawishi wowote
 
Safi sana, sasa anasubiriwa mbowe mwenyewe

Mnamtamani? Kila siku mnamsema kuwa ni akili ndogo, fomu 6 failure, na maneno mabaya yote myajuayo, leo mnatamani aje ccm? Kweli? Hapana, huo ni umalaya wa mdomo!! Hiyo propaganda ya Grace mliyotengeneza ni butu, ingekuwa kweli vyombo vya ccm na serikali vingelionyesha kwa mbwemwe, kama mlivyofanya kwa Shonza na Mwampamba. Na kwa kuwa vikao vilikuwa Dom mngelifanya sherehe huko na kupamba sana kubomoa upinzani. Vinginevyo hilo ni changa la macho.
 
Huku jf kuna watu wa ajabu kuna kitu gani cha maana cha kubishana hapo dah wadanganyika bwana!
 
ahaha RITZ1 umeludi tena mwambie baba yako akukamte wewe ni muuza madawa ya kulevya
 
Ni bora huyu mama kaamua kuweka huru mawazo yake amekacha chama cha familia kajiunga na chama cha watanzania shime grace.
 
Huyu dada/mama amegusia pale pale wengi wetu tunapopaona kua katika sera CCM bado ni safi na CDM ni wanaharakati tu wasio na uzoefu wowote wa kuongoza dola huku wakipita huku na huko kudanganya tui watz...

CDM imekua ghafla na bila ya kujitayarisha kisawa sawa kwenye demokrasia ya ndani na maslahi binafsi ya kiuongozi.. ni chama kidogo lakini kutokana na kukua kwa umaarufu wake maradufu ndani ya miaka kama mi5 hivi kimejikuta overwhelmed with its own success na kuonyesha nyufa zote za chama kikongwe...

katika uchambuzi yakinifu, CDM ina hatari ya kuzorota na kufa kabisa kama itashindwa uchaguzi wa 2015 kwa % nyingi na CCM. kama nilivyoonyesha hapo juu licha ya umaarufu kushindwa kwa kishindo kutaifanya CDM na safu yake ya uongozi "kuangalia wapi walikosea na nani anahusika na makosa hayo" yaliyosababisha kushindwa vibaya wakati wakiwa na imani ya kua umma mkubwa wa watz upo nao (nikimaanisha umma mkubwa not necessarily wapiga kura), kutokana na hulka ya ubinafsi ya wanasiasa waliopata mafanikio makubwa ndani ya muda mfupi "wafanya makosa watakataa kuwajibika" na hapo mgogoro mkubwa wa kiuongozi utauikumba CDM na kutishia uhai wake.

ukitilia maanani kua umoja miongoni mwa viongozi muhimu wa kitaifa wa CDM umeshikiliwa na imani 2 ya kua 2015 kuna uwezekano mkubwa wa kushika dola. kushindwa kwa CDM kutakua mwisho wa umoja na mshikamano baridi huu wa hawa viongozi na wengi wao kuanza kujiuliza maswali ya kubadilisha dira yote, mipango na taswira ya chama kupata nguvu mpya ya kisiasa. Mabadiliko mara nyingi hutishia watu wenye maslahi yao na hapo hali haitokua shwari kwa CDM.

CDM lazima washinde uchaguzi wa 2015 ili iendelee kuwepo, au watone down ambitions zao na waelekeze nguvu kwenye kujenga sustainable opposition kwa kuongeza namba ya wabunge, wavutie zaidi viongozi na vijana toka vyama vingine hususan toka CCM, otherwise mwisho wa CDM kama chama kikubwa cha upinzani ni 2015.

Hayo ni mawazo ya kizamani!
 
Grace Mbowe ninamfahamu na ni kweli ni dada yake Freeman..
Kuweka historia vizuri ni kwamba huyu Grace alikuwa bosi wa kitengo kimoja pale CSSC Upanga.. Kabla ya hapo alikuwa na ofisi yake ya consultancy pale Billicanas.. Na alikuwa registered Quantity Surveyor na alikuwa yuko safi.. Baadae akapata matatizo baada ya kupata mwanaume mmoja mwenye jina la kitanga.. Akaja kuachishwa kazi pale CSSC na baadae ikawa mbaya maana alikuwa anaongea na watu na kuwaazima pesa (alikuwa na credibility kubwa tu mbele za watu).. Tatizo akawa akipata anamkabidhi huyo jamaa na hela zinapelekwa pwani.. Maisha yakaendelea hivyo mpaka akawa amechokwa sio na watu baki tu.. bali hata ndugu zake maana waligundua huyo mwanaume ndo anaembugisha Grace na walishamuambia mara kibao aachane nae lakini ikashindikana.. Ikafikia wakati akawa anakimbiwa hata na wale waliokuwa juniors kwake.. Wale ambao mwanzoni walimheshimu na kumu-admire.. Last time jina lake lilitolewa na AQRB (bodi ya wasanifu majengo) kwamba atafutwa kwenye usajili wa bodi..
Kama kweli amekuja na uamuzi huu mie siwezi kushangaa..
Muwe mnashangilia huku mkijua mmelamba galasa..
 
Amejitambua kuwa yeye hawezikuwa msukule.

Inawezekana Mbowe alitaka ampeleke kwenye vurugu akaona upuuzi.

soon vijana wengi watajitambua pia

Msukule si tu kuchukuliwa kwa faida ya mwenyeshamba bali ni pamoja na kutetea ujinga pia cz msukule wengi CCM ni wazee na hawanajipya ukilinganisha na vijana wenye uelewa na utashi kwani hii sio 1947 hakuna hata kijana mmja hufuatwa kwao bali hujitolea kutokana na kuguswa kwao. usipoangalia yawezekna kuwa wewe ni msukule pia.
 
Amejitambua kuwa yeye hawezikuwa msukule.

Inawezekana Mbowe alitaka ampeleke kwenye vurugu akaona upuuzi.

soon vijana wengi watajitambua pia


Kama kweli wewe ni Mwanasiasa Unayependa AMANI na UPENDO wa NCHI yako; Kweli unaweza kunieleza VURUGU Mwenyekiti wa CHADEMA -- MBOWE alitaka kumpeleka Dada yake Ndani ya CHADEMA?

Wewe upo nchi yenye Demokrasia ya Ukweli na ni Matarajio yangu kuwa WEWE utakuwa MKWELI na kutoa ni VIPI alitaka kumpeleka Dada yake kwenye VURUGU akiwa CHADEMA?

Honestly na Usiwe MSUKULE na Unajua tafsiri ya MSUKULE... [
Mtu aliyechukuliwa na NGUVU za GIZA; Saidia ili na wewe Usiitwe MSUKULE]


"Dare to be honest and fear no labor."
 
Mwigulu kazi hiyo ya kuzurula nae mikoani tafadhari usile mzigo.
 
Angalau amepata nafasi ya jina lake kuandikwa kwenye gazeti na kujadiliwa JF... Amshukuru Mbowe kuwa mwenyekiti wa CDM maana vinginevyo tusingekuwa tunalijua jina Grace Mbowe...
 
Hongera sana na tunamtakia heri na fanaka , salamu nyingi sana kwa Juliana Shonza .
 
Jasusi.

Naona povu linatoka tu au na wewe una maslahi katika familia ya Mbowe.

Ritz,
Nimetulia kama maji ya mtungi. Hamna cha povu wala cha nini. Ndiyo, ninayo maslahi katika familia ya Mbowe kama nilivyo na maslahi katika familia ya Nyerere. Umefurahi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom