Dada yake MBOWE aikacha CHADEMA ajiunga na CCM!!

Dada yake MBOWE aikacha CHADEMA ajiunga na CCM!!

11:57 AM No comments

[h=3] [/h]
DADA wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Grace Mbowe, amejiunga na Chama Cha Mapinduzi ( CCM) akitokea Chadema, kwa kile alichodai haoni jambo jipya katika chama hicho.

“Freeman Mbowe ni mdogo wangu wa kuzaliwa kabisa, hakunishawishi kuingia CHADEMA, hivyo sioni haja ya kuendelea kubaki huku wakati sioni jambo jipya, mimi tangu naifahamu CCM iko vile vile, bali propaganda za upinzani ndizo zinawalaghai wananchi,” alisema.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, Hassan Mtenga kushoto akimkabidhi yadi ya CCM, Grace Mbowe, baada ya kutoka CHADEMA kwa kile alichodai hakuna jambo jipya.

Aliviasa vyama vya siasa, kuwa sasa umefika wakati wa kuacha malumbano na maandamano ya itikadi, yasiyokuwa na faida yoyote, badala yake huu ni muda wa kujenga nchi kwa ushirikiano.

Awali, akipokea kadi ya CHADEMA, Katibu wa CCM Wilaya ya Hai, Hassan Mtenga alisema alichokifanya Grace ni uamuzi wa busara, baada ya kutazama Chadema ilipo na inapokwenda.

Alisema wimbi la wanachama wa Chadema kurudisha kadi na kujiunga na CCM, limekuwa kubwa wilayani Hai. Alisema tangu Januari hadi sasa amepokea wanachama 530.

Mtenga aliwataka wananchi kutambua kwamba Jimbo la Hai, siyo kitovu cha upinzani bali CHADEMA ni chama kilichotoa upinzani kwa CCM katika uchaguzi mkuu wa 2010. Alisema hali hiyo, ilitokana na makundi ya CCM.

Alisema kwa sasa watu asitarajie tena suala hilo kutokea. --- via HabariLeo

mletauzi akiliyako haina akili hebu jiulize na ujijibu hiliswali dogo sana mbona mtoto wa nyerere yuko upinzani,ilihali babayake alikua mwenyekiti na mwasisi wa ccm ?

Aende tu kwa hao magamba alidhani akiwa chadema mbowe atampacheo kwasababu ni dadayake kama wanavyofanya magamba?
 
Mtapeli alieshindikana huyo,madeni chungu nzima anaishi kama digidigi. Kwanza arudishe hela za NGO aliyokuwa anasimamia upanga jengo la EMAU. MBOWE kamlipia madeni mpaka kamchoka. Anaishi kinyumba na tapeli aliemharibia maisha anatafuta pa kujishikiza. Njaaaaa hiyo
 
Du waafrica cku zote wanafiki tu yani haoni jipya akiwa CDM na CCM ni ileile sidhani kama wewe ni kijana wa enzi za Mwalimu.unaeona CCM ya Nyerere ni kama hii ya leo? kweli Dada uko seliously? Hizi pesa tutaziacha jamani hii c kama kutaka kuwambia watu kuwa Rangi ya damu ni nyeupe?
 
Mwache aende sisi ndio kwanza tunajiandaa na mpepetano wa mwaka 2014 na 2015 tupokee ushindi
 
mletauzi akiliyako haina akili hebu jiulize na ujijibu hiliswali dogo sana mbona mtoto wa nyerere yuko upinzani,ilihali babayake alikua mwenyekiti na mwasisi wa ccm ?

Aende tu kwa hao magamba alidhani akiwa chadema mbowe atampacheo kwasababu ni dadayake kama wanavyofanya magamba?

Hapo sasa. Hata Ulaya iko hiyo. But ansjuaje hiyo ni mpango wa seven buk per day.
 
mletauzi akiliyako haina akili hebu jiulize na ujijibu hiliswali dogo sana mbona mtoto wa nyerere yuko upinzani,ilihali babayake alikua mwenyekiti na mwasisi wa ccm ?

Aende tu kwa hao magamba alidhani akiwa chadema mbowe atampacheo kwasababu ni dadayake kama wanavyofanya magamba?
Hakuna mtoto wa Mwl. Nyerere ambaye yuko kwenye chama cha upinzani Tanzania. Validate your fact properly.
 
Tatizo wala huhitaji kufungua macho kuona kama undugu ndani ya CHADEMA ni mtaji kisiasa na kiuchumi kama vielelezo vinavyoonyesha hapa.
attachment.php
attachment.php

attachment.php
attachment.php
 
Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    34.7 KB · Views: 219
  • image.jpg
    image.jpg
    36.3 KB · Views: 219
  • image.jpg
    image.jpg
    29.7 KB · Views: 219
  • image.jpg
    image.jpg
    33.5 KB · Views: 219
Namkumbuka mdogo wangu Nakaaya alipojiunga na CCM akiikacha CHADEMA. Leo hataki kuzungumzia siasa.

Ndio, Grace Mbowe ana haki ya kujiunga na chama chochote kiile cha siasa, hata CUF akitaka. Kuondoka CHADEMA kwenda CCM sio hoja. Kama haoni jipya, nadhani atayaona mengi mapya huko CCM, ambayo imeshindwa kuiendesha nchi, licha ya kuwa na UZOEFU MKUBWA wa miaka 50!

Bado watu wanaishi kwenye nyumba za tembe; hayo ni maendeleo?
 
Hakuna mtoto wa Mwl. Nyerere ambaye yuko kwenye chama cha upinzani Tanzania. Validate your fact properly.

Mheshimiwa Letcia Nyerere, Joseph Nyerere, Makongoro Nyerere na watoto wa Mzee Wasira je?
 
Asije akawa kama Shibuda kwa CCM. Atawavuruga CCM ili wafe.haraka kuliko hata walivyotegemewa.
 
Mwigulu nadhani ni wakati muafaka uache kumtumia yule mhanga wa tindikali. Unaweza kumtumia huyu mgeni wenu mpya
 
Mwigulu nadhani ni wakati muafaka uache kumtumia yule mhanga wa tindikali. Unaweza kumtumia huyu mgeni wenu mpya

Mkuu yule mhanga wa tindikali mbona expired....walishamtumia kama condoms na kumtupa.
 
Umepotea sana humu jamvini tangu Taarifa za Dawa za kulevya zipambe moto tutazianzisha tena ili ukimbie jumla kumbe hii ndio dawa yako
Hahaha hahaha hahaha hahaha umenikumbusha dawa ya mwigulu mchemba ni jesca kishoa hahaha hahaha hahaha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom