Kwa siku Mwalimu analipa shilingi 1200 kwenda na kurudi kazini, kwa wiki analipa 1,200 X 5 = 6,000, kwa mwezi analipa shilingi 6,000 X 4 = 24,000 (usafiri wa daladala)
Kama Mwalimu huyo anatoka mbali na kilipo kituo cha daladala basi atalipia bodaboda si chini ya shilingi 2,000 kwa siku (kwenda na kurudi) = shilingi 10,000 kwa wiki, = shilingi 40,000 kwa mwezi
Ukijumlisha na nauli ya daladala kwa mwezi unakuta mwalimu huyo analipa nauli ya shilingi (24,000 + 40,000) = shilingi 64,000
Ukiangalia mshahara wake kwa mwezi ni shilingi 400,000
Ukitoa kodi na makato mengine anabaki na take home ya kama shilingi 336,000
akilipa kodi ya nyumba, umeme, maji chakula nk Mwalimu huyo anakuwa na negative income, ndiyo maana wameamua kumpunguzia maumivu kwa ku subsidize nauli