CWT cha sasa ni mchwa unaotafuna faida iliyotengenezwa na CWT ya Gratian Mkoba. Walimu waamke na kupiga kelele juu ya unyonyaji huu mkubwa

Mbogi

JF-Expert Member
Oct 10, 2021
681
825
Chama cha walimu kilianza miaka ya 2000 kikiongozwa na baadhi ya viongozi akiwemo Magreth Sitta aliyepokelewa kijiti hicho na ndugu Gratian Mkoba.

Ni katika kipindi cha miaka ya 2010's ndipo chama kilianza kuweka mipango na dira ya maendeleo ya chama kwa kutumia michango ya walimu kama ilivyo kisheria.

Uongozi wa G. Mkoba ulifanikiwa kutekeleza mpango wa kujenga vitega uchumi karibu kila wilaya na kila makao makuu ya mkoa, kikiwemo kitega uchumi cha jengo la mwalimu house ambalo hadi kufikia mwaka 2014 lilikuwa linaingiza faida ya bilioni moja kwa mwaka.

Lengo likiwa ni kujiandaa kuwapunguzia mzigo wa makato ya 2% ya mshahara wa walimu. Hata hivyo waliweza kuratibu mipango mingi ya maendeleo ikiwemo mchakato wa uanzishwaji wa benki ya mwalimu japo hili lilivurugwa na uongozi uliokuja baada yake.

(1) CWT ya sasa tangu alivyoondoka Mkoba hakuna jambo jipya la maendeleo lilofanyika la kuongeza kipato chochote,

(2) Mpango makhsusi wa kupunguza 2% ya makato ya mishahara ya walimu ilitupwa "kapuni" na sasa hata faida inayopatikana kupitia vitega uchumi ndiyo inayotafunwa pamoja na michango hiyo ya 2%.

(3) CWT ya sasa haioneshi wala kuwasomea wawakilishi wa walimu mpango wake wa maendeleo, bajeti wala mapato na matumizi. Ukiwauliza walimu hata wawakilishi wa ngazi za shule wakwambie dira, mipango, mapato na matumizi ya chama wanakwambia hawajui.

Kwa hali iyopo sasa viongozi wote wa CWT ya sasa ni wabadhilifu na watakatishaji wa fedha wakishirikiana na baadhi ya maafisa wachafu wa serikali.

CHONDE CHONDE WALIMU AMKENI MPAZE SAUTI KULINDA JASHO LENU NA MAFANIKIO YA CHAMA CHENU.
 
Back
Top Bottom