CWT yapinga walimu kusafiri bure

CWT yapinga walimu kusafiri bure

Limekaa kisiasa zaidi..walimu wanapiga kura ndo mana bure..wanafunzi hawapigi kura inabdi walipe.kwaio maisha baada ya uchaguzi ni maigizo
 
Tanzania bana ukileta akili chanya lazima wataleta akili hasi kwa ajili ya kupata ufahali tu.
MTANZANIA ndivyo tulivyo mkuu. Asilimia kubwa ni majitu ya hovyo sana. Angalia comments ya baadhi ya majitu humu ndio utapata takwimu halisi ya madubwana yalivyo na hila nafiki....kwa kuwa tu Hilo suala limeletwa na DC Paul Makonda.
 
Tanzania bana ukileta akili chanya lazima wataleta akili hasi kwa ajili ya kupata ufahali tu.
Ni watu wachache sana wenye tabia hizo mi ni mwalimu nasema lazima nichukue kitambulisho siwasikilizi cwt
 
mm sijasomea uwalimu ili kuonewa huruma hata kidogo....huku ni kuwaona walimu ni wanyonge kiasi cha kulipiwa nauli za daladala.....kimsingi mm sitamwambia konda eti mm ni mwl.....mm na degree yangu kabisa nilioisotea kwa halali nianze kusumbuana na konda!hata kama mshahara hautoshi siwezi bora nikope...wanasiasa watuache na maisha yetu kabisaa
 
Sawa na mtoto je? JPM kaamua kuwapa watoto elimu bure hivo ingekuwa jambo jema kusafiri bure pia!

hoja ya msingi ni kuongeza maslahi ya walimu ili kila mwalimu, aende kwa usafiri anaopenda kazin, mbna wao hawapandi daladala ina maana mwalim hastahiri kuwa na private car au nao watumia magari ya umma kama watumishi wengine wa serikali,
 
Lkn mkuu cyo lazima kupanda hiyo bure
kama siyo lazima ni nn maslahi yake kwa umma, maana kiongozi anapotoa huduma lazima aangalie mantiki yake kwa wananchi, unanikata mikono ili unipe msaada kwakua nitashindwa kutafuta hhahhaa
 
Ukiitafakari kwa kina amri hii ni muendelezo wa sarakasi za "danganya toto" za kutafuta umaarufu na kutafuta maslahi ya mtu mmoja na si kwa manufaa ya walimu!
Haiingii akilini wanafunzi walipe nusu ya nauli walimu wasafiri bure!
Halafu ni nani atakayewafidia wenye magari ya biashara kwa kutoa huduma hiyo bure wakati wanalipa leseni, kodi, mishahara na matengenezo ya gari kwa gharama? Hakuna sheria inayomlazimisha mfanyabiashara kutoa huduma bure, kwa hiyo amri ile ilikuwa ya kuuza sura, aliyeitoa alikurupuka na kuropoka mithili ya mtu aliyetoka usingizini! Ndiyo maana wenye akili zetu tunasema ni amri hewa isiyo na mashiko.
 
DC yupo sahihi kufanya hivo na wala sio kuwazalilisha waalimu kama wengine mnavozani mbona polisi wanajeshi wanasafiri buree akati nao wanalipwa mshaharaa inamana nao wanazalilishwa makonda amefanya analoliweza yeye kwa waalimu wa dar huezi mlazimisha eti sisi hatutaki kusafiri bure tunataka nyumba na mishahara mikubwa ili tulipe wenyewe nauli yeye amefanya anachoweza wewe kama hutaki bure toa nauli
 
Toka lini mtu anayepiga wakubwa/wazee (Warioba) akawa na akili nzuri kwenye jamii?
 
DC yupo sahihi kufanya hivo na wala sio kuwazalilisha waalimu kama wengine mnavozani mbona polisi wanajeshi wanasafiri buree akati nao wanalipwa mshaharaa inamana nao wanazalilishwa makonda amefanya analoliweza yeye kwa waalimu wa dar huezi mlazimisha eti sisi hatutaki kusafiri bure tunataka nyumba na mishahara mikubwa ili tulipe wenyewe nauli yeye amefanya anachoweza wewe kama hutaki bure toa nauli
Walimu nao mtawanunulia sare kama za Polisi na Jeshi, halafu kwa nini iwe ni walimu tu wa kusafirishwa bure na isiwe madaktari, wauguzi, wataalam wa kilimo n.k.?
Wanajeshi na Polisi wanapokuwa kwenye magari ya abiria tunawachukulia kama watu wanaotupa ulinzi, na kwa kweli hadi sasa wameonyesha ustaarabu mkubwa kwa kupanda magari wakiwa wachache wachache kiasi kwamba hata wenye magari hawaoni bughudha yoyote, na hao walimu watatusaidia nini wakiwa garini?
Acheni kutafuta umaarufu kwa gharama za wenzenu, kama kweli serikali iko serious inunue mabasi maalum kwa kazi hiyo!
 
Ni mambo ya ajabu sana haya, kwa foleni za DAR hao walimu wala hawawezi kuwahi. Lakini wapo watumishi watoa huduma wengi kama wale wa Afya, Maji nk mbona hatusikii lolote. Bado Makonda aeleze dhumuni hasa ni lipi.
 
Kwa akili yako mwalimu wa Manyovu anapanda daladala? Je, wazo hili ni la serikali kuu au ni initiative ya sehemu husika? Poleni sana
Pole wape walimu mnaowatumia kisiasa zaidi badala ya kutengeneza mfumo endelevu,mwanae alipe mia mbili and at the same time yeye anapanda bure! Mnawatengenezea aibu jibu ni kuwakopesha vyombo vya usafiri au muwaongezee hela ya nauli kwenye mishahara yao
 
Si wawanunulie mabasi, serikali bana, inataka kuwadhalilisha kwa matingo tu
 
Back
Top Bottom