Rais wa CWT Leah Ulaya atumika na genge la maadui wa walimu

HaMachiach

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
3,399
6,077
CWT ilizaliwa tarehe 1/11/1993 na mwaka huu Chama kimepanga kufanya kumbukizi ya miaka 30 ya umri wake jijini Mwanza. Kwa kawaida maandalizi ya shughuli kama hii hupangwa na Sekretarieti yaani rais, makamu wa rais, katibu mkuu, naibu katibu mkuu, na mwekahazina wa chama. Kisha mpango huo husimamiwa na wajumbe wa kamati ya utendaji ya taifa yenye muwakilishi mmoja kutoka kila mkoa; mwakilishi wa walimu wanawake, mwakilishi wa vijana na mwakilishi wa walimu wenye ulemavu. Kilichojitokeza ni hiki;

Bi Leah Ulaya ambaye ni rais wa chama alishirikiana na wenzake wa sekretarieti kwenye maandalizi ya sherehe hizo zilizopangwa kufanyika tarehe 16 disemba 2023 jijini Mwanza huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan. Cha kushangaza ni kwamba tarehe 12 disemba 2023 Bi Leah Ulaya akiwa Dodoma huku viongozi wenzake wa chama wakiwa Mwanza alitangaza kuahirishwa kwa shughuli hizo eti kwa sababu
  1. Mgeni Rasmi hatopatikana
  2. Wamekosa uwanja wa CCM Kirumba kwa ajili ya kufanyia sherehe.
Hapa kuna mambo machache ya kujiuliza. Kwa nini Bi leah Ulaya anafikia maamuzi ya kuahirisha sherehe peke yake bila ya kuwahusisha viongozi wenzake? Pia kwa kawaida kama mgeni rasmi hatapata nafasi kwa tunavyomfahamu Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania na namna anavyowapenda walimu, ni kweli kwamba ameshindwa kupata mtu wa kumuwakilisha? Kwa nini barua ya kukosa uwanja na ya Mgeni rasmi kuahirisha hawaonyeshi viongozi wenzake ambao wako Mwanza?

Ile clip inayosambaa ikimuonesha Mwalimu Leah akitangaza kuahirisha sherehe inaonesha kuwa anatoa taarifa ile kwa shinikizo. Ni kwa kuwa anaonekana anatetemeka na hata maneno yake ni ya kukosea kosea. Na hakutolea taarifa hiyo kwenye ofisi za chama zilizoko Dodoma.

Kwenye kikao cha kamati ya utendaji kilichopita kilichofanyika Mwanza, Bi Leah Ulaya alidai kwamba anayo barua ya katibu mkuu kiongozi ikimuelekeza kuwa Bwana Japhet Maganga katibu mkuu wa CWT ajiuzulu nafasi yake kwa kuwa Serikali haiko tayari kufanya kazi na yeye kwa hiyo chama kinaathirika kwa uwepo wake. Aliposhinikizwa na wajumbe aioneshe barua hiyo alikataa na hadi leo zaidi ya yeye mwenyewe hakuna mtu aliyekiri kuiona barua hiyo. Huu ni uongo mtupu na kuisingizia Serikali. Kwani kinachotafutwa hapa ni nafasi ya Ukatibu mkuu ambayo kama umekuwa ukifuatilia sarakasi za sakata hili tangu mwazo utagundua kuwa genge lile lile linaloongozwa na Deus Seif aliyekuwa Katibu Mkuu wa CWT, Joseph Misalaba aliyekuwa naibu katibu mkuu, Protas Magessa aliyewahi kuwa mwekahazina wa muda na Mohammed Utaly aliyewahi kuwa mwekahazina wa taifa wa CWT ndio wakandarasi wa vurugu zote ndani ya CWT. Baada ya sarakasi za muda mrefu hatimaye genge hili limefanikiwa kumghilibu Leah Ulaya na kwamba kama asingeshirki kutekeleza mpango huu eti wangefichua siri zake nyeti walizonazo.

Wasiwasi uliokuwepo ni kwamba kama Mhe. Rais angehudhuria kwenye sherehe angeelezwa kinaga ubaga kile kinachoendelea CWT ambapo baadhi ya viongozi waandamizi ndani ya serikali ndio wanaofadhili vurugu hizI na lengo lao ni kwamba Maganga akiondolewa wataweka mtu wao kwenye nafasi hiyo na wanatarajia atawasaidia sana mwaka 2025 kwa kufuja mali za chama. HUO NDIO UKWELI HALISI na Mhe. Rais akiamua kutumia vyombo vyake atabaini ukweli huu. Bi. Leah amewahi kwenda idara kuu ya utumishi kuomba barua ya kumuondoa Maganga, aliponyimwa alikwenda kwa msajili wa vyama vya wafanyakazi naye akamtolea nje. Sasa anamsingizia Katibu mkuu kiongozi na Serikali. Katika Sakata hili, picha potofu wanayoweza kuipata walimu ni kwamha Serikali haiwapendi na mbaya zaidi watamhusisha na Mhe. Rais. PICHA HIYO SI YA KWELI. Hii ni kazi ya genge la wahuni waliotajwa hapo juu ambao kama umekua mfuatiliaji wa sakata hili tangu mwanzo utakua umeona mtiririko wa matukio na mipango yao miovu juu ya walimu na mali zao.

Genge hili liliigawa kamati ya utendaji kukafanyika kikao cha mapinduzi. Msajili aliyepita Bi. Pendo akasimamia katiba ya CWT hili likaisha, genge hili likaongoza na baadhi ya wafanyakazi wa CWT makao makuu wakaenda kwa Katibu mkuu wizara ya Kazi eti kulalamikia uonevu. Katibu wa WIzara hili akalimaza. Na leo hii likazuka hili jipya.

Maamuzi ya Bi. Leah Ulaya yamesababisha mambo yafuatayo.
  1. Wajumbe wa kamati ya Utendaji na wengine waliopaswa kuhudhuria sherehe hizo tayari wapo Mwanza itabidi walipwe fedha za usafiri na kujikimu
  2. Wageni kutoka vyama na mashirika ya nje ya nchi tayari wako Mwanza, lazima baadhi ya gharama Chama zitaingia na watarudi kwao bila kukamilisha lengo walilojia na hii ni aibu kwa Taifa.
  3. Baadhi ya kumbi za mikutano ukiwemo ukumbi wa Tunza zimeshalipiwa na malipo ya awali ya vyakula tayari yameshafanyika.

Bi Leah Ulaya ameitisha kikao cha wenyeviti wote wa mikoa na kamati ya utendaji ya taifa ili kifanyike Kesho tarehe 16 disemba 2023 jijini Dodoma. Lengo lake ni kuendeleza propaganda ile ile kwamba serikali haitaki kufanya kazi na Maganga. Kikao hicho kitashindikana kwa kuwa wengi wa wajumbe tajwa hapo juu wako Mwanza.

CWT kufikisha umri wa miaka 30 pamoja na mambo mengine imetokana na viongozi waadilifu na wenye busara na kufanya kazi na serikali kwa amani na maelewano. Wanasiasa hawakuwa wanaingilia shughuli za chama. Hivi sasa wanasiasa ndio wanaokivuruga chama kwa kutumia genge tajwa hapo juu ambalo wanalifadhili kwa fedha na umashuhuri wao. Ushauri wa Mhe. Mizengo Pinda kule Geita ulikuwa wa maana sana na ulionesha kwamba mzee huyu anaelewa kiini cha migogoro ya chama cha walimu. Tunaendelea kuwaomba walimu kusimama imara na chama chao na wasikubali kuona kinarudi kilipokuwa enzi za wabadhirifu ambao kwa bahati nzuri tumeshawabainisha. Ni muhimu walimu wasiyumbishwe wawajue adui zao
 
Huku town nasikia tu CHAKUHAWATA na siyo CWT Ina maana ninyi walimu mna vyama viwili tofauti?
 
Mwakilishi wa walimu wanawake, ana jukumu gani?

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
WALIMU WOTE NCHI NZIMA KILA MMOJA KWA IMANI YAKE WAINGIE MAKANISANI NA MISIKITINI KULAANI WOTE WANAOGOMBANIA MICHANGO YAO HUKU WAKIWAACHA WALIMU WAKINYIMWA HAKI ZAO NYINGI.LAANA NA MIKOSI YOTE IWAANDAME WATU HAWA AMEN.
 
Back
Top Bottom