Vigogo CWT wakomba Billion 7.2 ndani ya wiki moja

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,583
11,659
Walimu Walimu Walimu

20231118_163851.jpg

Vigogo CWT wakomba Sh. 7.2 bilioni ndani ya wiki moja

Na Faki Sosi
ZIMWI la migogoro limeendelea kukitafuna Chama cha Walimu nchini (CWT), wiki mbili baada ya kupelelewa kitita cha Sh. 9.4 bilioni kutoka Hazina, imefahamika.

Taarifa kutoka makao makuu ya CWT mjini Dodoma zinasema, mabilioni hayo ya shilingi, yalitawanywa ndani ya wiki moja, baada ya kuingizwa kupitia benki.

Fedha hizo, ni michango ya wanachama wanaokatwa kupitishia mishahara yao, ili kuendesha chama chao.

Mtoa taarifa wa gazeti hili anasema, kila mwezi, serikali inapeleka
CWT kiasi cha Sh. 4.8 bilioni, kutoka kwenye makato ya wanachama wake nchini kote.

Anasema, kiasi cha Sh. 9.6 bilioni, ni michango ya miezi miwili ya Septemba na Oktoba 2023. Anasema, fedha za Septemba zilichelewa kutolewa kufuatia baadhi ya waliokuwa viongozi kuiandikia barua benki ya NMB, kuzuia fedha hizo.

Viongozi waliozuia fedha kutolewa benki, waliongozwa na Joseph Misalaba, aliyekuwa naibu katibu mkuu. Misalaba anadai kuwa bado kiongozi halali wa chama hicho na anatambulika benki kama mmoja wa watia saini katika baadhi ya akaunti.

Akaunti za CWT zilizopo NMB, zimetajwa kuwa ni Na. 20103500343, 20101300312 na 20106600576, na kwamba fedha ziliruhusiwa kutolewa baada ya viongozi wa sasa kwenda mahakamani.

Katika uamuzi wake wa 25 Oktoba 2023, Mahakama Kuu, ilikubaliana na ombi la CWT la kuruhusu kutumiwa kwa fedha hizo. Siku saba baada ya kupita na mahakama kuidhinisha kutumika kwa fedha hizo, haraka viongozi wakaandaa malipo ya zaidi ya Sh. 7.2 bilioni.

Aidha, CWT wanamiliki akaunti nyingine kupitia benki ya Walimu (MCB) yenye Na. 0351083201 MCB na CRDB, ambako ndiko mabilioni ya shilingi yaliyotokea Hazina kama michango ya walimu kwa mwezi Oktoba, waliamua kuyapitishia.

Uamuzi wa kupitishia fedha CRDB, ulitokana na wanachoita, “mizengwe ya NMB na Benki ya Walimu,” ambako wanawatuhumu kuzuia fedha zao bila sababu za msingi.

Katika hatua nyingine, kuna madai ya kutoelewa kwa viongozi wa chama hicho kutokana na kuwapo matumizi mabaya ya madaraka na ubadhirifu wa fedha za wanachama.

Viongozi wanaotuhumiana ni pamoja na Rais wa CWT, Leah Ulaya; Makamu wake, Dinna Mathamani; Katibu mkuu, Maganga Japhet, Misalaba pamoja na viongozi wengine wa ngazi za juu ndani ya chama hicho.

Uchunguzi uliofanywa na MwanaHALISI na kuthibitishwa na wajumbe 18 wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) waliofutwa uanachama na Baraza Kuu la chama hicho, unaonyesha namna fedha zinavyotafunwa.

Mgogoro unaoutafuna CWT unachangia kwa kiwango kikubwa kuharibu utulivu wa walimu na kujenga taharuki ndani yao, jambo linalochangia kuharibu ufanisi wa elimu nchini.

“Tunaiomba serikali na vyombo vyote vya kimamlaka kuuangalia mgogoro huu kwa jicho la tatu na la kipekee, ili haki ipatikane na CWT iendelee kuwepo kwa maslahi ya walimu waliowengi, badala ya kikundi cha watu wachache,” ameeleza Misalaba akidai kuwa serikali isipoingilia kati CWT itakufa na maslahi ya walimu yatapotea.

Aliongeza: “CWT imekuwa na mgogoro toka mwaka 2017 jambo linalowafanya walimu kutumia muda mwingi kukaa ofisini kujadili juu ya mgogoro huu badala ya kufundisha hivyo kuhatarisha maendeleo ya elimu nchini.”

Naye Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CWT aliyefutwa uanachama na Baraza Kuu, Mwalimu Thobias Sanga, ameomba serikali kuunda tume ya kuchunguza mgogoro, ikiwamo matumizi mabaya ya michango ya wanachama.

“Tunaiomba serikali na wenye mamlaka wajitokeze na kutoa maamuzi juu ya jambo hili, walimu wanaathirika kisaikolojia, wanakosa umoja na wanashindwa kufanya shughuli nyingine za uchumi kwa kutumia muda mrefu kujadili jambo hili,” alisisitiza.

Hata hivyo, madai hayo yaliwahi kukanushwa na Leah katika mahojiano yake na gazeti hili, wiki tatu zilizopita.

Wanatuhuamiana nini?
Viongozi hao ambao wametia fora kwa migogoro, wametuhumiana katika maeneo mbalimbali ikiwamo kukiuka Katiba, Kanuni na Miongozo.

Kwa mfano, Maganga anadaiwa kuvunja kanuni za CWT toleo la nne la mwaka 2015, kifungu cha 32 juu ya ‘utatuzi wa migogoro na nidhamu kwa viongozi,’ kwa kukikimbia kikao cha KUT na kuliita baraza batili.

Anatuhumiwa kuvunja katiba ya CWT ibara ya III, kifungu Cha 22.3 (f) kwa yeye kuandaa ajenda ya baraza la Taifa badala ya KUT na hapa ametumia madaraka vibaya.

Pia anatuhumiwa kukaidi melekezo kutoka ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ya tarehe 15/06/2023 yenye Kumb Na. DA 27/380/12/94 yenye kichwa ‘Utekelezaji wa Majukumu ya Chama kwa Kuzingatia Katiba na Kanuni za CWT’.

Barua hiyo ilibatilisha baraza la tarehe 18/06/2023 kwa kuwa liliitishwa bila kupangwa na KUT na kimepangwa kinyume cha utaratibu.

Aidha, barua hiyo iliwataka watendaji wakuu wa CWT na wajumbe wa KUT (waliofikisha malalamiko kwa niaba ya wenzao), kukutana katika ukumbi wa OSHA mnamo tarehe 16 Juni 2023 saa tano kamili asubuhi, katika kikao kilichoitishwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, bado Maganga, aligoma kuhudhuria.

Akizungumzia tuhuma hizo, Rais wa Leah Ulaya alikemea kitendo cha Misalaba, Mwalimu Magesa na baadhi ya viongozi wakuu wa kitaifa, wakiwamo wajumbe wa Kamati tendaji kusimamisha majukumu ya kazi ya katibu mkuu Maganga.

Leah alisema, viongozi hao wamevunja katiba na kanuni za CWT kwa maslahi yao binafsi na kuchafua taswira na heshima ya chama na wanachama.

Alisema ili kuondoa sintofamu iliyotokana na kikao batili cha Kamati tendaji Taifa cha tarehe 6 Juni 2023, pamoja na maazimio yake Msajili wa vyama vya wafanyakazi na waajiri kupitia Kumbukumbu namba. DA 27/380/12/21 alithibitisha maazimio ya kikao hicho na utekekezaji wake hakikuwa halali na kilifanya maamuzi batili ambayo hayakuzingatia katiba na kanuni za CWT.
 
Majambazi ya walimu

Atoto njoo mpenzi uone mijizi inayowaibia walimu kama ambavyo wewe umeiba moyo wangu, shubaamiti.
Ama kweli mapenzi upofu, hawa waliowaibia walimu wananikera, ila we uliyekwiba moyo wangu nakuchekea na tunajifunika shuka moja. 😍😍

😂🤣
 
Wapigaji kila kona Nchi hii shida.
 
Wana Mtandao mkubwa sana Takukuru wapo tu kukamata vikesi vya kijinga ila wahuni wanatoa Billion za kutosha wiki moja Bank na wapo kimya hao BOT wenye sheria zao kuhusu mambo ya Fedha nchini wapo kimya unakuta gazeti linatoa taarifa za Fedha harafu eti BOT hawajui kitu Nchi ngumu sana hii...
 
Back
Top Bottom