Cris Mauki anapenda sana kwa Wanawake

Muite

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
2,342
4,801
Jamaa anapenda sana SIFA kwa wanawake. Jamaa hakuna post yake au video clip
itakayoeleza mema ya mwanaume. Yeye clip zake zote ni kumponda mwanaume dhidi ya Mwanamke. Yaani utafikiri hiyo taaluma yake ya Saikolojia ni kwaajili ya Mapungufu ya Wanaume dhidi ya wanawake. Kumbe hajui pia saikojia inaeleza kuwa tabia za mtu hutambulisha kundi lake. Mauki post/clips zake zinamuonyesha kana kwamba yupo kundi la waathirika na tabia za wanaume(!!!!!!!!).

Mauki kama mwl wa saikolojia katika mahusiano alitakiwa kuielimisha jamii bila kubagua.

Ila jamaa kafanikiwa sana kujipatia umaarufu kwa WANAWAKE
 
Soko ni kubwa upande wa ke kuliko upande wa Me. Ukiwa mfanyabiashara lazima uangalie bidhaa gani inatoka zaidi.
Sawa kabisa. Anaangalia biashara yake kwa sababu wanawake wengi wapo emotional na wana maumivu ya mahusiano kiasi cha kujiona wao ni victims na wanaume ni watesaji au mbwa 😁😁.. Kwa hiyo akitokea mwanaume "good guy" Wa kusimama upande wao tofauti na hali ya kawaida lazma wamkubali.
 
Eti juzi katoa picha na mkewe akasema Eti anaona kama mwenye bahati sababu mkewe alimpenda alivyo sijui nini na nini amemvumilia n.k.

Kuna mtu akamuuliza;

Kwani wakati huo hukuwa na kazi ya kukupa kipato walau cha kujikimu na familia?

Akajibu alikuwa nayo.

Sasa hapo cha ziada ni kitu gani?

Angesema hakuwa na kazi wala kipato chochote lakini mwanamke akampenda na kuishi nae na kumpa heshima yake siku zote hapo ndipo kungekuwa na ziada na utofauti maana wanawake wengi wako kimaslahi ukiwa huna kipato hakutaki,

Na kama ulikuwa nacho kikakata atakutafutia sababu muachane kumbe kakuchoka siku nyingi alikuwa anatafuta sababu tu.
 
Back
Top Bottom