Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

Kwa hiyo huamini katika maombi?
Magonjwa mengi yanaondoshwa kwa maombi
Kwa sisi tz tungeanza kwanza na Toba maana Ni Kama tulizembea kuchukua tahadhari mapema
Mungu anaweza jibu moja kwa moja au kwa kupitia kwa wataalam wetu wa afya.
Hayo Mambo unayosema tax reduction si suluhisho la ugonjwa

Sent using Jamii Forums mobile app
sawa umesikika!!

haya jibu hoja ya mtoa mada
 
Scars, Ndiyo ,Mimi Naamini katika maombi kwa asilimia zote.
Wewe unaamini katika Nini?

Kumjengea ama kutokumjengea mchungaji ni maamuzi ya mtu..kuna baraka katika kuwatunza Watumishi wa Mungu (japo si lazima ufanye hivyo)
Kama roho yako inakusukuma kutoa sadaka kwa ajili yake Wewe toa tu.
Kama unasukumwa kutoa sehemu nyingine Katoe..
Usikariri ,sadaka si lazima utoe kanisani tu.

Maombi ya mtu huanzia ndani mwa mtu,kanisa Ni moyo wako.
Kanisani huwa tunakwenda kukusanyika kama ilivyo desturi yetu lakini mahali popote pale waweza kujenga madhabahu na ukasali..si lazima kanisani

Labda nikwambie boss wangu,Imani yangu SI ya kutegemea kuombewa na mtu.
Nasimama kuomba mwenyewe.

Mchungaji ana nafasi yake Kama kuhani wa Mungu,Mimi pia Nina nafasi yangu kubwa sana kujiombea.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya corona kuisha nitaomba tusabahiane humu ili kujua nani kapona na ni nani kafa. Penye wengi tutaoana mengi. Kila mtu aamini kwa anachokiamini. Kama wewe unamwamini daktari sawa, kama unamwamini mchungaji sawa, kama unamwamini allah sawa, kama unamwamini Yesu Kristu sawa, kama unaamini miti shamba sawa,

kama unaamini ushirikina sawa, kama unaamini milima sawa, kila mtu na imani yake. Corona ipo kazini na haina tiba. Tiba ni how you protect yourself. Na ni kwa jinsi gani unatii sheria bila shuruti. Gnyt guys.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Saint Anne,
Mimi siamini katika maombi na sioni sababu yakufanya utani katika afya yangu kuamini maombi yanaweza kuniepusha na hili janga

Kwanini mchungaji asiombe kwa mungu ili mungu amjengee kama ambavyo yeye amekua akiwaambia nyie mumuombe mungu pindi mtakapopata tatizo kama kweli maombi yanafanya kazi?

Kwaiyo nawe ni miongoni mwa watu ambao wanaamini wataishinda hii corona kwa maombi?

Aisee we're fighting two pandemics diseases coronavirus and religious
 
Kiukweli nianze kwa kuwapongeza watanzania wote kwa kujitahidi kuzingatia mambo yote tulioelekezwa na viongozi wetu juu ya kujikinga na covid 19. Mwanzo wengi tulikuwa tunachukulia utani lakini mda unavyoenda tunagundua kuwa mauti IPO sufuriani tuwe makini, Ndugu zangu Mimi na kaelimu kangu ka darasa La saba naomba nitoe maoni ili nchi yetu isijefikia hatua ya kuokota maiti kama nchi nyingine zinavyopata tabu:

-Kwanza serikali isipaniki na kuwaweka watu wanachi wrote karantini kwa mini nasema hivyo hii ni kwa sababu baaadhi ya mikoa kama daresalam ugonjwa umetapakaaa mitaani sasa ikiwaweka karantini watu watakuwa wanaenda huko wakiwa na vijidudu mwisho kutakuwa na wimbi LA vifo vingi.

-Pili serikali ifunge baadhi ya mipaka ya mikoa kwa mfano daresalam ugonjwa umeonekana kuwapata wengi watu kutoka daresalaamu na Zanzibar wakiendelea kwenda mikoa mingine maambukizi yatatawanyika kama tulivyoanza kuona baadhi ya mikoa ikipata maambukizi kwa Mara ya kwanza.

-Tatu Serikali kuanza kupima mikoa ile ambayo kuna maambukizi mengi na kuwapeleka hospitali kwa wale ambao watapatikana na maambukizi na kuwatibu.

-Nne Serikali kuanza kupiga dawa ya kuua vijidudu(virus) kwenye maeneo yote yaliokuwa na watu wengi has a mikoa niliyoitaja hapo juu.

Mwisho wananchi wasisitizwe kumuomba mungu na kuchukua tahadhari zote ikiwemo kuepuka mikusanyiko hata ikiwezekana ya ibada.

NB: Adui yetu mkuu kwa sasa ni covid19 tuwewazalendo kwa taifa letu.
 
Sasa hivi kila mtu anafungua uzi lakini maudhui yale yale hakuna jipya!kuna thread km 8 humu wazo ni hili hili moja! Ah "kolona" tupixhe xie😅
 
Scars, Kama huamini Ni wewe boss
Mimi Naamini kabisa na Mungu ana njia nyingi za kuponya watu kama nilivyosema pale juu kwamba anaweza achilia uponyaji kupitia madaktari na namna nyingine nyingi Kama mafunuo au kupona Moja kwa moja.

Nimekuuliza wewe unaamini katika Nini?
Unaamini punguzo la Kodi na Riba za mikopo zitamaliza Corona??

Kuhusu mchungaji mbona nimekwambia kwamba Kama Roho mtakatifu anakusukuma ukatoe kwa mchungaji Basi nenda katoe..Kama husukumwi kutoa huko basi usitoe
Wapi wamekulazimisha kutoa sadaka?

Sadaka wa wahitaji(yatima &Watumishi wa Mungu) Ni somo Pana nitakufundisha Kama utahitaji.

Mungu huwalisha na kuwavisha Hawa watu kwa kupitia wanadamu ambao Ni Mimi na wewe...

Amhurumiaye mhitaji humkopesha Mungu..wanaofanya hivyo wanamkopesha Mungu maana hiyo kazi ni yake mwenyewe..Yeye mwenyewe atawalipa. Sijasema Kama Ni lazima utoe..toa unapojisikia wewe.

Lakini Neno pia linasema leteni chakula ghalani mwangu ili kiwepo chakula..pia hazina yako ilipo ndipo na Roho yako ilipo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom