Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Yumkini hali si nzuri. Rais kafunguka.

=====

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe magufuli ameandika:

"Ndugu zangu Watanzania, kutokana na ugonjwa wa Corona, nawaomba tutumie siku 3 za kuanzia tarehe 17- 19 Aprili, 2020 {Ijumaa, Jumamosi na Jumapili} KUMUOMBA MWENYEZI MUNGU aliye muweza wa yote atuepushe na janga la ugonjwa huu. Tusali kwa kila mmoja kwa imani yake, atatusikia."

Rais.JPG
 
Thats the bold and strong move, huku tukizingatia tahadhari zitolewazo ndio njia pekee itakayoyuvusha katika hili. Tukisema tunapambana we are doomed!

Naimani wote watu 50+mill tutakutana 31 dec kusherehekea mwaka mpya tukiwa wazima wa afya tele. Tupambane na hofu ndio mbaya zaidi
 
Katika tweet ya jioni hii, Rais Magufuli ameandika yafuatayo "Ndugu zangu Watanzania, kutokana na ugonjwa wa Corona, nawaomba tutumie siku 3 za kuanzia tarehe 17- 19 Aprili, 2020 {Ijumaa, Jumamosi na Jumapili} KUMUOMBA MWENYEZI MUNGU aliye muweza wa yote atuepushe na janga la ugonjwa huu. Tusali kwa kila mmoja kwa imani yake, atatusikia."

 
Rais John Magufuli wa Tanzania amewataka watanzania watumie siku za ibada za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kuiombea nchi iepukane na corona

Source,EATV update
My take :hofu inaua hivyo kila moja ajaribu kufanya anachoweza
 
Back
Top Bottom