Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

battawi koran yenu ni matokeo ya kitu kinachoitwa UPINGAJI.
Koran inapinga mafundisho ya Biblia karibu ya agano jipya karibu yote yani imefanya kinyume chake.

Mfano Nabii aliye mkuu kuliko manabii wote ulimwenguni Yohana mbatizaji anasema Yesu ni mwana wa Mungu na alikuja kuukomboa ulimwengu kwa kufa kwake tumepata ondoleo la dhambi (kiroho) Koran inasema Yesu si mwana wa Mungu ila inakubali ni Masihi seriously?

Biblia inatuambia Yesu alizaliwa horini koran inasema alizaliwa chini ya mtende seriously?
Kuwa mwana wa Mungu,kunahitaji maelezo,kwa kuwa Yesu alizaliwa Na Maria,Mwanadamu, Lakini Mungu alipulizia Pumzi yake ili apate Mimba yule Mariam. Sasa tunasemaje kuhusu Adam ,Babu yetu yeye hakuwa na baba wala mama ,si yeye angelistahiki zaidi kuwa mwana kamili wa Mungu?
Eva yeye kaumbwa bila ya Mama ,hata yeye angelistahiki kuitwa mwana wa mungu.
Kuwa Mwana wa mungu hapa umsikilize yesu mwenyewe ,amejiitaje?
Mbona yeye alijiita 'MWANA WA ADAM''?

ama kuhusu kule Horini hakuwezi kuwa na Mtende?.
Qur-an haijakataa ,kuzaliwa yesu bila ya baba,ila imekuongezea information ambayo kwenye biblia haikuwemo.Huo mtende ulitajwa hapa kwa malengo mahususi,aliutikisa na kumletea tende kama chakula baada ya kujifungua.
Hatukuona kwenye biblia habari ya kunywa maziwa eti kwa vile kajifungukia Horini(zizi la ngombe) labda hii nayo ingelifanana
 
Kwa waamini wa Biblia,yawafaa wajisomee kidogo haya
 

Attachments

  • en_Christian_Scholars_Recognize_Contradictions_in_the_Bible.pdf
    306.5 KB · Views: 3
Napenda kumalizia kwa kusema kuwa Mungu yupo,na
Alituma wajumbe wake wengi tuu ili kuwatambulisha wanadamu.
Huu ulikuwa ndio mpango aliojiwekea yeye mwenyewe.
Manabii na mitume walikuja wengi sana duniani.
Lakini waliokuwa maarufu na wa mwisho wao ni Muhammad (saw), akifutiwa na Yesu (Issamwana wa Mariam),Mussa, na wote hao Babu yao ni Ibrahim( baba wa manabii wengiwa nyumba ya israil na Waarabu.)
Siku ya Kiama ipo
Na binadamu wote tutawekwa kitimoto kuhukumiwa kwa mujibu wa matendo yetu.
Hivi vitabu tulivyonavyo leo vikuu vya dinivinatupa mafunzo yanayo fanana sana.
Usizini,Uwa
Usiibe,Fanya kazi towa sadaka na zakka,
Kuwa Muadilifu na mwema,
Usiiuwe bila ya haki.
Usilewe,na usiseme uongo.
Usimshirikishe Mungu na iungu mingine.
Usifanye ushirikina.
nk....
 
Mkuu najua unatumia akilizako kutafuta fact katika imani za watu.

Lakini to be honest kila binadamu mwenye akili timamu kunakitu anacho kiamini kwenye maishayake ambacho hajakiona.
Ni vichaa na mataahiratu ndio unaweza kusema hawaamini chochote mana akilizao hazifanyikazi vizuri.

Leo ukienda kulala angalia saayako wakati unaingia kitandani alafu ukiamka angalia saatena alafu jiulize hayo masaa yaliyopita wakati umelala ulikuwa hujui chochote kinacho endelea popote, jiulize tena nini kilikuwa kina endelea kwenye maisha yako katika mudahuo.
Ukikosa jibu ndio ujue kuna vitu invisible vinaendelea kwenye maisha yako ambayo wewe huvijui na ndio MUNGU.

Hoja kwamba MUNGU hayupo ama hatupendi kwa sababu kwanini anaacha majanga yana ikumba duniani na kusababisha vifo sio sawa.

MUNGU ameumba watu hapa duniani kaziyao ni kumtumikia kumuabudu na kutendeana mema na sio kuishi milele hapa.

Hapa ni sehemu ya kupita na MUNGU hajali umekufa kwa njia gani, anajali umetenda jambogani la kumpendeza hapa duniani ili uweze kuishi milele mbinguni.

Binadamu kama ametenda mema ataishi milele baada ya kufa.

Majangayote yanayo tokea na kutoa uhai wa binadamu haina mana kwamba MUNGU hatupendi ama hayupo, MUNGU yupo na anaona kilakinachoendelea kwa binadamu.

Anaweza kuepusha na anaweza kuacha kwa sababu zake mwenyewe.

Matatizo mbalimbali yanayo mkuta binadamu haya manishi kwamba MUNGU hatupendi ama hayupo.

Binadamu mbali na matatizo yanayo mkuta amefanikiwa sana katika maisha yake kwa mambo mbalimbali aliyojaliwa uwezo wa kuyafanya na MUNGU, sitayataja nimengi na kila mtu mwenye akili anajua.

Mbali na majanga binadamu amefanikiwa kuishi kwa raha na anasanyingi zisizo hesabika.

Kumbuka hata wewe unawachapa watoto wako na haina mana kwamba hauwapendi.

Bina damu kupata tabu na kufa sio tatizo kwa MUNGU.

MUNGU haumii tunapo kufa miiliyetu, anaumia tukifa rohozetu.

Kitabu cha mwanzo 3 - 23 kuna sehemu kinasema baada ya Adam kuhasi maagizo ya MUNGU, kwa kula tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya, MUNGU akaamuru aondolewe katika bustani iliasile tunda katika mti wa uzima alafu akaishi milele hapa duniani.

Hapo utaelewa kwamba MUNGU anajali maisha ya milele mbinguni hapa duniani jambo la mana kwa MUNGU ni kumpenda na kufuata maagizoyake, kifo kipotu hata pasipokuwa na majanga kama HIV , Covid-19, Ebola nk.

MUNGU yupo, anatupenda wakati wote.
Lakini pia hutujalia neema na anatoa adhabupia.
Poleni na majukumu ya hapa na pale sasa na kale yanayowafanya msilale, niende moja kwa moja kwenye mada husika.

Kama kweli maombi yanafanya kazi kwa namna ambayo tunaaminishwa, kwanini viongozi wa dini wameungana kutekeleza agizo la kuvunja mirundamano ikiwemo mijumuiko ya kiibada ili kuikwepa korona?

Kama walifanya maombi kwa lengo la kuizuia corona isiingie nchini, lakini tunaona corona imeingia, nini kinachokufanya uwaamini kua maombi ya sasa wanayojipanga kuyafanya yataitokomeza corona mazima?

Haya mambo probably si magumu ila ugumu tunauweka sisi kwa kuweka mizaha kwa kutumia kivuli cha dini.

Hivi mfano hawa madaktari wetu na sekta ya afya kiujumla wangejumuika kwenye maombi kwa kuamini kwamba maombi ni njia madhubuti ya kutatua matatizo kama haya katika kila janga la ugonjwa. Kama ambavyo watu wa dini wamekua wakituhimiza kufanya, je tungefanikisha kutibu gonjwa lipi kwa maombi?

Ngoma inaingia tanzania wabongo tulijitia wachamungu sana kua tumepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na n'ge hivyo ukimwi kwetu sio tishio.

Lakini tunachokiona mpaka saizi mapasta na masheikh wanachukua vidonge kwa siri sana. Lakini pamoja na hayo hatuwaoni wakijisalimisha kua wameshindwa kudhibiti ukimwi kwa maombi yao.

Mungu ambaye tunamtolea sadaka kila siku halafu katika matatizo kama haya kajichimbia tu wala hatuoni juhudi zake, huyu si mungu wakuabudiwa. Ni sawa na rafiki mnafki ambaye kwenye matanuzi mkiwa viwanja mnakua naye karibu sana halafu ikatokea siku umeishiwa anakukimbia.

Wahubiri wanahubiri huku wamevaa face mask at the same time wanasema damu ya yesu ni tiba ya kila kitu. What a joke but i ain't laughing?

Tunaambiwa ukiwa na imani waweza kuamisha hadi milima lakini sikutegemea kuona vatican, mekka ziwe kipaumbele kukataza watu wasiende kwao kwa hofu ya korona.

Mungu muweza wa yote yuko wapi mbona kawasusia msala madaktari wetu halafu yeye amesizi tu eti mpaka aamshwe kwa maombi?

Kwanini mungu mjuzi wa yote na muweza wa yote ahitaji maombi?

Mbona kwenye zile hadithi za gharika na sodoma na gomora huyu mungu ali-respond haraka sana kwanini asifanye hivyo kwenye janga hili linalomaliza ndugu zetu na kudhoofisha hali ya uchumi wetu?

Hivi kweli mungu huyu yupo kweli? Maana viongozi wetu wa dini nao wanaathirika mpaka inafikia hatua italy makanisa yameshehena maiti inamaana yeye haoni?

Kwanini Mungu ahitaji maombi yetu ili aweze ku-solve matatizo yetu, ilihali anaelewa hitaji la moyo wetu hata kabla hatujasema?

====

Chukua tahadhari kwa kufuata angalizo lililotolewa na mamlaka ya afya Corona haidhibitiwi kwa maombi bali kwa kuepuka makatazo ambayo yameainishwa na shirika la afya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna popote ndani ya biblia ilipokataa kuoa zaidi ya mke mmoja. bali Kuna pendekezo tuu lilopendekeza kuwa kuto kuoa ni bors kwa kiongozi wa dini,na atakae owa aowe 1 tena hiyo ni kwenye agano jipya.
Lile la kale Unaowa upendao.
Kwa hiyo Qur-an na Biblia kwa hili viko sambamba.
Nyogeza
Hata lile la Mungu mmoja na Utatu mtakatifu, Qur-an imewakataza wakristo juu ya imani hiyo kwa kuwa ni ya kupangwa na wanadamu si ya Mungu.

Kwanza kabisa ukiikubali biblia kua ni kitabu cha kweli hupaswi kutoa dosari ambazo ziko ndani yake

Kutoa dosari katika biblia kwa kuilinganisha na kuran kunaonesha kua hukubaliani na biblia, bali unaangalia maneno gani ambayo kwenye biblia yana match na maneno ya kuran

Mkristo anaweza kusema kwa kutumia akili yake anakubaliana kua biblia ni kitabu cha kweli kilicholetwa na mungu, nawewe ukisema kitabu hicho cha kuran ni cha kweli kutoka kwa mungu halafu wote mkakubaliana kua mungu ni mmoja, hiyo ni "contradiction"

Mungu wa biblia ambaye kawasetia pepo ya kuimba na kuabudu milele na mungu wa kuran ambaye kawasetia pepo ya mabikra 72 wanaume. Mungu hao hawawezi kua mmoja

Mpaka hapo tunaona kua akili ya mtu kukubaliana na jambo fulani sio kipimo thabiti kujua ukweli wa hilo jambo ambalo yeye kalikubali

It's Scars
 
Simply juu ni kule Nywele zako zilikoelekea.
Scientifically juu ni 'out of earth's surface' both directions' as you like' tunakuita juu.
Kwa upande wa Mungu anaposema juu ni kwa sababu yeye yupo nje ya hii dunia na nje ya space.
Yeye ni mkuu na ana kiti cha enzi hukko aliko.
Ukubwa wa kistuli cha hicho kiti kina enea mbingu na nchi, sikuambii ukubwa wa hicho kiti chenyewe.
Mungu katika kuumba kwake ,Kiti chake cha enzi ndio kiumbe kikubwa kuliko vyote, nacho kiko nje ya space, nje ya Galaxy

"Kiti cha enzi"

Huyo mungu anakaa kwenye hicho kiti inamaana ana makalio kama sisi?

Habari hii umeipatia wapi?

It's Scars
 
Kwanza kabisa ukiikubali biblia kua ni kitabu cha kweli hupaswi kutoa dosari ambazo ziko ndani yake

Kutoa dosari katika biblia kwa kuilinganisha na kuran kunaonesha kua hukubaliani na biblia, bali unaangalia maneno gani ambayo kwenye biblia yana match na maneno ya kuran

Mkristo anaweza kusema kwa kutumia akili yake anakubaliana kua biblia ni kitabu cha kweli kilicholetwa na mungu, nawewe ukisema kitabu hicho cha kuran ni cha kweli kutoka kwa mungu halafu wote mkakubaliana kua mungu ni mmoja, hiyo ni "contradiction"

Mungu wa biblia ambaye kawasetia pepo ya kuimba na kuabudu milele na mungu wa kuran ambaye kawasetia pepo ya mabikra 72 wanaume. Mungu hao hawawezi kua mmoja

Mpaka hapo tunaona kua akili ya mtu kukubaliana na jambo fulani sio kipimo thabiti kujua ukweli wa hilo jambo ambalo yeye kalikubali

It's Scars
UNATAKIWA KULINGANISHA NA KUBAINI HITILAFU, MAFUNDISHO YA MSINGI
Kimsingi vitabu hivi vyote vinazubgumzia Mungu mmoja,lakini mapokezi na mikono ya watu imereport tofauti
Ndo maana Qur-a akajaribu kusahihisha pale palipokuwa na hitilafu,
huu ni ushahidi kuwa Chanzo ni kimoja,
 
"Kiti cha enzi"

Huyo mungu anakaa kwenye hicho kiti inamaana ana makalio kama sisi?

Habari hii umeipatia wapi?

It's Scars
Jiongeze kujisomea, Najuwa wewe akili yakoiko kwenye makalio tuu,unafikiria kujisaidia ,lakini hayo ni Muhali Kwa Mungu,wala hahitaji hayo.
Kile kiti ni Sovereign tuu, kuonesha ukuu kwa viumbe kama alivyotuumbia sisi kuwa wafalme wetu huwa na viti vya vya kiutawala,Hii ni methali tuu,Lakini Mungu hafananishwi na kitu chochote ukijuacho kuwa ni kitu,lakini yupo na anona na kusikia
 
Mkristo anaweza kusema kwa kutumia akili yake anakubaliana kua biblia ni kitabu cha kweli kilicholetwa na mungu, nawewe ukisema kitabu hicho cha kuran ni cha kweli kutoka kwa mungu halafu wote mkakubaliana kua mungu ni mmoja, hiyo ni "contradiction"
Sasa inaonesha unaanza Kuamini Uwepo wa Mungu, lakini unaelekea kwenye Ukiristo,
Ok ,hatua si ndogo,
Pia mimi nakualika kujisomea Qur-an pia ili akili yako ijuwe pande zote mbili naiwez kuwa huru,
ukikwama ,tunaweza kushauriana katika hilo.
Imani si kiti cha urahisi rahisi
Mungu ni Imani ya Hakika yenye Fcts za kutosha.
 
We jamaa vina vyako vimekaa pouwa Ila Napingana kwa hoja zako zilizojaa tafiti changa

Twende

Scars nakufananisha na slay queen/... Hoja zako ziko weak.. Zama za Covid19/ Unapinga uwepo Wa Mungu/ unaendelea na drama za wazungu/ na majungu/ hauko smart nime prove/ we zuzu/
Nigga u better stay cool/ Am a graduate from school.....

Note:
Corona virus is real ,we need to take extra cares,

One love

Mwanaharakati nisiye na dini, nawakunja waumini kila mkao utadhani john sin.../

Nawapagawisha mi ndo wenu teacher, kwa vina adimu natoa funzo zaidi ya hao ma-preacher.../

Leteni sadaka masta nihubiri juu ya kinasa, yule pasta mliyemtolea yuko kuzifanyia anasa.../

Fikra za muafrika zimepotoshwa kwa juzuu, wajanja tusha sanuka wamebaki mazuzu.../



It's Scars
 
Kuwa mwana wa Mungu,kunahitaji maelezo,kwa kuwa Yesu alizaliwa Na Maria,Mwanadamu, Lakini Mungu alipulizia Pumzi yake ili apate Mimba yule Mariam. Sasa tunasemaje kuhusu Adam ,Babu yetu yeye hakuwa na baba wala mama ,si yeye angelistahiki zaidi kuwa mwana kamili wa Mungu?
Eva yeye kaumbwa bila ya Mama ,hata yeye angelistahiki kuitwa mwana wa mungu.
Kuwa Mwana wa mungu hapa umsikilize yesu mwenyewe ,amejiitaje?
Mbona yeye alijiita 'MWANA WA ADAM''?
Tatizo lako unaandika maneno mengi sana alafu haujibu maswali yangu.
Hizo habari za Adam na Hawa Koran ilizipata wapi kama si kwenye Biblia?

ama kuhusu kule Horini hakuwezi kuwa na Mtende?.
Hakuwezi na mimi nimeshafika Bethlehem alipozaliwa Yesu tumeelezwa yote.
Hiyo haitoshi si wote tunaweza kufika Israel, Biblia haijaandika alizaliwa chini ya mtende.

Qur-an haijakataa ,kuzaliwa yesu bila ya baba,ila imekuongezea information ambayo kwenye biblia haikuwemo.
Kama haikuwemo wewe umeitoa wapi? Yani Koran iisemee Biblia like seriously?

Huo mtende ulitajwa hapa kwa malengo mahususi,aliutikisa na kumletea tende kama chakula baada ya kujifungua.
Uwiii nasekaga!
Biblia inasema Kristo alipozaliwa ilipnekana nyota ya jaa ambayo iliwaongoza mama jusi wa mashariki mpaka horini na walimpelekea mtoto Yesu zawadi.
Ndio maana kipindi cha Christmas huwa unaona kitu kinaitwa Boxing day.
Hizo story unatoa wapi wewe?

Hatukuona kwenye biblia habari ya kunywa maziwa eti kwa vile kajifungukia Horini(zizi la ngombe) labda hii nayo ingelifanana
Biblia inazungumza habari za kupelekewa zawadi tu na mama jusi haisemi alikula tende wala kuzaliwa chini ya mtende.

Naomba uniambie Muhammad alijuaje kama Biblia imepotoshwa, alijuaje kama Yesu alizaliwa chini ya mtende, alimjuaje mama yake na kujua manabii wakale wote waliopita walifanya nini na kwa ajili gani?
 
Misingi ya Kikristo ni hiyi hapa kwa mujibu wa Yesu mwenyewe.
1.Uzima wa milele ni kumjuwa Mungu kuwa Ni mmoja wa kweli na wa pekee.( One God)
2. Yesu Ametumwa na Mungu ,na kwa hiyo ni mtumishi wake.
3.Yesu kaleta Ujumbe ,na wanafunzi waliupokea.
4.Wanafunzi wa Yesu wao wamejuwa kuwa Yesu katoka kwa Mungu ,na ujumbe umetoka kwa Huyo Mungu.
Hii ni misingi yako tu hakuna Mkristo mwenye hii misingi.
Msingi wa Ukristo ulio mkuu ni UPENDO na msingi wa pili ni kufuata mafundisho ya Kristo OVER!

5.Wakati Yeu anaondoka ,anawasisitiza watu wake kushika Mafundisho na kuyafanyia kazi.
Soma Injili ya
Yohana 17:-
1 Yesu alipokwisha sema hayo, alitazama juu mbinguni, akasema, “Baba, saa imefika! Mtukuze Mwanao ili naye Mwana apate kukutukuza. 2 Maana ulimpa Mwanao mamlaka juu ya watu wote ili awape uzima wa milele wote hao uliompa. 3 Na uzima wa milele ndio huu: kukujua wewe uliye peke yako Mungu wa kweli, na kumjua Yesu Kristo uliyemtuma. 4 Mimi nimekutukuza hapa duniani; nimeikamilisha ile kazi uliyonipa nifanye. 5 Sasa, Baba, nitukuze mbele yako kwa ule utukufu niliokuwa nao kabla ya kuumbwa ulimwengu. 6 “Nimekufanya ujulikane kwa watu wale ulionipa kutoka duniani. Walikuwa watu wako, nawe ukanipa wawe wangu; nao wamelishika neno lako. 7 Sasa wanajua kwamba kila ulichonipa kimetoka kwako. 8 Mimi nimewapa ule ujumbe ulionipa nao wameupokea; wanajua kwamba kweli nimetoka kwako, na wanaamini kwamba wewe ulinituma.

Hii verse uliyoiweka hapa unaiamini?
 
The Jehovah’s Witnesses in their “AWAKE” Magazine dated 8th September 1957 published the following headline:
“50,000 Errors in the Bible” wherein they say “..there are probably 50,000 errors in the Bible...errors which have crept into the Bible text...50,000 such serious errors...” After all of this, however, they go on to say: “...as a whole the Bible is accurate.”
I don't believe them do you got anything else?
 
Wote wako chaka wanaskilizia madaktari watoe jibu la hitimisho maana wao tayari wamejipanga na majibu yao mfukoni mwao

Ikitokea madaktari wametoa dawa, tutawaskia wakisema maombi yao ndio yamewezesha wanasayansi kupata dawa.

Na ikitokea hakuna dawa iliyotengenezwa na wanasayansi watasema kua mungu katupa corona ili kutujaribu na kutupima imani au watasema mungu hujibu maombi kwa wakati wake
Nikienda kanisan nikasikia maubiri ya padri huwa nacheka kimoyomoyo na kusema hapa niwe na kuja ilimradi tuu nisitengwe na wanajamii.
 
Wewe jamaa bhana
Kama hii ndio hoja yako basi unaweza kusema kila jambo limekuja kuumbua uongo wa dini.

Kwa nini hukusema kutafuta riziki kumekuja kuumbua uongo wa dini,maana ingetosha tu mtu kukaandani na kuomba dua halafu chakula kikamshukia.
Au kwanini hukusema kusoma kumekuja kuumbua uongo wa dini,maana ingetosha tu mtu kwenda msikitini kuomba dua kisha tayari akawa professor. Na hivyo hivyo mambo mengine.

We jamaa mwenyezimungu aliweka nidhamu/kanuni katika ulimwengu na mambo hayaendi vile unavyo fikiri wewe.
Hiyo paragraph ya mwisho sio kweli, mwenyezi Mungu mnambebesha misalaba ambayo sio. Hii haina tofauti kama unavyowaona wananchi kwa kilakitu kumlaumu Rais wa nchi.
 
HOW COVID-19 KILLS--I'm a Surgeon--And Why We Can't Save You



Source : Duc C. Vuong MD

N.B
Gonjwa la Covid-19 lipo hivyo tuzingatie maelekezo tunayopewa na Wizara ya Afya jinsi ya kujikinga na corona kwa kufuata hatua hizi rahisi : epuka misongamano, kukumbatiana, kusogeleana , epuka kuwa abiria wa bodaboda, nawa mikono mara kwa mara kwa maji yanayotiririka n.k
 
Nenda na chain hii nani alimza mzazi wako nk nk nk nk mpaka ukomo wake

Sent using Jamii Forums mobile app
Chain hiyo ukiifata bila kuipindisha itakuletea swali kua hata mungu naye atahitaji chanzo

Mzazi wa mungu ni nani? Baba na mama wa mungu nao watahitaji chanzo

Mpaka hapo bado kuna mungu tena?
 
Hii ni misingi yako tu hakuna Mkristo mwenye hii misingi.
Msingi wa Ukristo ulio mkuu ni UPENDO na msingi wa pili ni kufuata mafundisho ya Kristo OVER!



Hii verse uliyoiweka hapa unaiamini?
Sikiliza ,Uzi huu ulikuwa ni wa Mtu asiyeamini dini ,wala Mungu,
Nadhani wewe unapokuja na hoja za kulinganisha Uislamu na Ukiristo,itabidi tuanzishe uzi wingine.
Lakini,kwa ufupi,Miminaamini kuwa Muungu wa Yesu ndiye Muungu wa Muhammad ,na ndiye Muumba wa kila kitu.
Habari ya kuamini aya aukutoiamini,ni suala jingine,kwani nisingeliicote kama siiamini na kuikubali.
Yesu hapa anatufunza kuwa yeye mwenyewe anaomba kwa Mungu,hivyo nasisi tufuate nyayo zake.
Yohana 17:
24 Baba, shauku yangu ni kwamba, hawa watu ulionipa wawepo mahali nilipo ili waweze kuona utukufu wangu; utukufu ambao umenipa kwa kuwa ulinipenda hata kabla ulimwengu haujaumbwa. 25 Baba Mtakatifu, ijapokuwa ulimwengu haukufahamu wewe, mimi ninakufahamu, na hawa wanajua ya kuwa umenituma. 26 Nimekutambulisha wewe kwao, na nitaendelea kulitambulisha jina lako kwao ili upendo ulio nao kwangu uwe upendo wao pia; nami niwe ndani yao.”
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom