Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
44,314
105,143
Poleni na majukumu ya hapa na pale sasa na kale yanayowafanya msilale, niende moja kwa moja kwenye mada husika.

Kama kweli maombi yanafanya kazi kwa namna ambayo tunaaminishwa, kwanini viongozi wa dini wameungana kutekeleza agizo la kuvunja mirundikano ikiwemo mijumuiko ya kiibada ili kuikwepa korona?

Kama walifanya maombi kwa lengo la kuizuia corona isiingie nchini, lakini tunaona corona imeingia, nini kinachokufanya uwaamini kuwa maombi ya sasa wanayojipanga kuyafanya yataitokomeza corona mazima?

Haya mambo probably si magumu ila ugumu tunauweka sisi kwa kuweka mizaha kwa kutumia kivuli cha dini.

Hivi mfano hawa madaktari wetu na sekta ya afya kiujumla wangejumuika kwenye maombi kwa kuamini kwamba maombi ni njia madhubuti ya kutatua matatizo kama haya katika kila janga la ugonjwa. Kama ambavyo watu wa dini wamekua wakituhimiza kufanya, je tungefanikisha kutibu gonjwa lipi kwa maombi?

Ngoma inaingia Tanzania wabongo tulijitia wachamungu sana kuwa tumepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na n'ge hivyo ukimwi kwetu sio tishio.

Lakini tunachokiona mpaka saa hizi mapasta na masheikh wanachukua vidonge kwa siri sana. Lakini pamoja na hayo hatuwaoni wakijisalimisha kua wameshindwa kudhibiti ukimwi kwa maombi yao.

Mungu ambaye tunamtolea sadaka kila siku halafu katika matatizo kama haya kajichimbia tu wala hatuoni juhudi zake, huyu si mungu wakuabudiwa. Ni sawa na rafiki mnafki ambaye kwenye matanuzi mkiwa viwanja mnakua naye karibu sana halafu ikatokea siku umeishiwa anakukimbia.

Wahubiri wanahubiri huku wamevaa face mask at the same time wanasema damu ya Yesu ni tiba ya kila kitu. What a joke but I ain't laughing?

Tunaambiwa ukiwa na imani waweza kuhamisha hadi milima lakini sikutegemea kuona Vatican, Mekka ziwe kipaumbele kukataza watu wasiende kwao kwa hofu ya korona.

Mungu muweza wa yote yuko wapi mbona kawasusia msala madaktari wetu halafu yeye amesizi tu eti mpaka aamshwe kwa maombi?

Kwanini Mungu mjuzi wa yote na muweza wa yote ahitaji maombi?

Mbona kwenye zile hadithi za gharika na sodoma na gomora huyu mungu ali-respond haraka sana kwanini asifanye hivyo kwenye janga hili linalomaliza ndugu zetu na kudhoofisha hali ya uchumi wetu?

Hivi kweli Mungu huyu yupo kweli? Maana viongozi wetu wa dini nao wanaathirika mpaka inafikia hatua Italy makanisa yameshehena maiti inamaana yeye haoni?

Kwanini Mungu ahitaji maombi yetu ili aweze ku-solve matatizo yetu, ilihali anaelewa hitaji la moyo wetu hata kabla hatujasema?

====

Chukua tahadhari kwa kufuata angalizo lililotolewa na mamlaka ya afya Corona haidhibitiwi kwa maombi bali kwa kuepuka makatazo ambayo yameainishwa na shirika la afya
 
Hata mimi nilikuwa nasubiria kweli kweli hao wanaojiita mitume wasambaritishe huu mzigo

Sent using Jamii Forums mobile app
Wote wako chaka wanaskilizia madaktari watoe jibu la hitimisho maana wao tayari wamejipanga na majibu yao mfukoni mwao.

Ikitokea madaktari wametoa dawa, tutawaskia wakisema maombi yao ndio yamewezesha wanasayansi kupata dawa.

Na ikitokea hakuna dawa iliyotengenezwa na wanasayansi watasema kua mungu katupa corona ili kutujaribu na kutupima imani au watasema mungu hujibu maombi kwa wakati wake.
 
Mungu muweza wa yote yuko wapi mbona kawasusia msala madaktari wetu halafu yeye amesizi tu eti mpaka aamshwe kwa maombi?

Sasa nani amekwambia amewaachia Madaktari,wakati yeye ndio ameruhusu ugonjwa huo uwepo na uwadhuru watu.

Yeye ndio ameuleta na yeye ndio wakuuondoa,hakuna mwanadamu mwenye kuweza kuuondoa ugonjwa wala kuleta ugonjwa.

Maelezo yako yote yanaonyesha ni kwa namna gani humjui Mola muumba wa mbingu na ardhi.
 
Poleni na majukumu ya hapa na pale sasa na kale yanayowafanya msilale, niende moja kwa moja kwenye mada husika.

Kama kweli maombi yanafanya kazi kwa namna ambayo tunaaminishwa, kwanini viongozi wa dini wameungana kutekeleza agizo la kuvunja mirundamano ikiwemo mijumuiko ya kiibada ili kuikwepa korona?

Kama walifanya maombi kwa lengo la kuizuia corona isiingie nchini, lakini tunaona corona imeingia, nini kinachokufanya uwaamini kua maombi ya sasa wanayojipanga kuyafanya yataitokomeza corona mazima?

Haya mambo probably si magumu ila ugumu tunauweka sisi kwa kuweka mizaha kwa kutumia kivuli cha dini.

Hivi mfano hawa madaktari wetu na sekta ya afya kiujumla wangejumuika kwenye maombi kwa kuamini kwamba maombi ni njia madhubuti ya kutatua matatizo kama haya katika kila janga la ugonjwa. Kama ambavyo watu wa dini wamekua wakituhimiza kufanya, je tungefanikisha kutibu gonjwa lipi kwa maombi?

Ngoma inaingia tanzania wabongo tulijitia wachamungu sana kua tumepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na n'ge hivyo ukimwi kwetu sio tishio.

Lakini tunachokiona mpaka saizi mapasta na masheikh wanachukua vidonge kwa siri sana. Lakini pamoja na hayo hatuwaoni wakijisalimisha kua wameshindwa kudhibiti ukimwi kwa maombi yao.

Mungu ambaye tunamtolea sadaka kila siku halafu katika matatizo kama haya kajichimbia tu wala hatuoni juhudi zake, huyu si mungu wakuabudiwa. Ni sawa na rafiki mnafki ambaye kwenye matanuzi mkiwa viwanja mnakua naye karibu sana halafu ikatokea siku umeishiwa anakukimbia.

Wahubiri wanahubiri huku wamevaa face mask at the same time wanasema damu ya yesu ni tiba ya kila kitu. What a joke but i ain't laughing?

Tunaambiwa ukiwa na imani waweza kuamisha hadi milima lakini sikutegemea kuona vatican, mekka ziwe kipaumbele kukataza watu wasiende kwao kwa hofu ya korona.

Mungu muweza wa yote yuko wapi mbona kawasusia msala madaktari wetu halafu yeye amesizi tu eti mpaka aamshwe kwa maombi?

Kwanini mungu mjuzi wa yote na muweza wa yote ahitaji maombi?

Mbona kwenye zile hadithi za gharika na sodoma na gomora huyu mungu ali-respond haraka sana kwanini asifanye hivyo kwenye janga hili linalomaliza ndugu zetu na kudhoofisha hali ya uchumi wetu?

Hivi kweli mungu huyu yupo kweli? Maana viongozi wetu wa dini nao wanaathirika mpaka inafikia hatua italy makanisa yameshehena maiti inamaana yeye haoni?

Kwanini Mungu ahitaji maombi yetu ili aweze ku-solve matatizo yetu, ilihali anaelewa hitaji la moyo wetu hata kabla hatujasema?
=============================

Chukua tahadhari kwa kufuata angalizo lililotolewa na mamlaka ya afya Corona haidhibitiwi kwa maombi bali kwa kuepuka makatazo ambayo yameainishwa na shirika la afya
Usimjaribu Mungu wako
 
Wote wako chaka wanaskilizia madaktari watoe jibu la hitimisho maana wao tayari wamejipanga na majibu yao mfukoni mwao

Ikitokea madaktari wametoa dawa, tutawaskia wakisema maombi yao ndio yamewezesha wanasayansi kupata dawa.

Na ikitokea hakuna dawa iliyotengenezwa na wanasayansi watasema kua mungu katupa corona ili kutujaribu na kutupima imani au watasema mungu hujibu maombi kwa wakati wake
Kuna mmoja alisema corona ni laana ya Mungu kwa wachina, juzijuzi naye akaupata, sasa sijui akipona atawaambia nini wafuasi wake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom