Mungu hana dini na hazijui dini zenu

Mtapenda

JF-Expert Member
Sep 20, 2011
1,115
2,055
Habari zenu

Kumekuwepo na Dini nyingu na madhehebu Mengi juu ya dunia lakini Dini kubwa kuu mbili
1. Ukristo
2. Uislam

Katika hizo Dini mbili kuna mchuano mkali sanaa ila wanashare waanzilishi wa hizo Dini

Maana wote wanadai baadhi ya manabii au watangulizi wa hizo Dini walikua wafuasi wao

Mfano Ibrahim, Daudi, Suleiman, Yacobo na wengine wengi muislam anadai hao jamaa walikua waislam na wakristo wanadai hao jamaa walikua wakristo.

Lakini mkristo haamini katika mtume mohamed ila muislam anaamini katika Nabii Issa ambao wakristo wanamuita Yesu, ila tuu waislam hawaamini kama Yesu alitundikwa msalabani na kuvuliwa nguo.

Lakini katika uwepo wa Mungu kila Dini na kila dhehebu ambazo zipo Duniani wana utaratibu wao wa kuabudu na kwa mujibu wa Maombi yao wanadai wanajibiwa.

Na kila Dini inaamini kuna maisha mapya baada ya kufa ambapo kutakua na raha na starehe ambayo haina mwisho.

Kulingana na Ulimwengu ulivyo naamini kwamba huyo Mungu hana Dini na humjibu yoyote atakaye muomba na wengine hawajibu wanakufa na matatizo yao kwenye Dini zote.

WENGINE WANAFIKA MBALI ZAIDI WANADAI MUNGU NI NADHALI AMBAYO HAIPO POPOTE NI HADITHI TUU NA NGONJERA AMBAZO WATU WALITUNGA KUTUGAWA NA WATUTAWALE KIRAHISI KIFIKRA

kwahiyo makusudi makubwa yalikua kutoa umoja na kuleta utengano kusiwepo na maelewano..

JE, Mdau unaamini Mungu huyu anadini kwamba yeye ni muislam au mkristo!?
 
Back
Top Bottom