Dini zinafundisha uongo kumhusu Mungu

Clever505

JF-Expert Member
Jul 27, 2020
1,099
2,032
Mods, nilishawahi kuweka hapa threads mbili zinazohusiana na mambo ya dini ila sijui huwa mnazifuta au mnazihamishia kwingine maana baada ya muda kidogo nikipost huwa sizioni. Ikiwa mada hizi hazitakiwi humu niambieni sio mnaziondoa bila taarifa.

Kwenye mada sasa,
Dini zetu hizi kubwa mbili zinafundisha mambo ambayo ukiyaangalia na kuchunguza kwa makini utagundua ni uongo wa waziwazi kabisa na ni wachache tunalitambua hilo. Haya ni baadhi ya Mambo hayo ambayo ukituliza akili kuyaelewa utagundua kwamba ni uongo.

I. MUNGU ANAJIBU MAOMBI.
Hebu fikiria kuna mtu anaamini biashara yake ikifanyiwa maombi atapata faida nyingi. Mtu anaamini akienda kuchukua udongo ulioombewa na mwamposa akaumwaga shambani atapata mazao ya kutosha. Mtu anaamini akifanyiwa maombi anapona ugonjwa alionao. Hii ni imani ya uongo sana, yaani mi nilime kwa juhudi na kufata kanuni zote za kilimo nikose mavuno kisha we upate mavuno bora kwa sababu ya maombi tu? Mi naweka bidhaa bora dukani na nahudumia kwa ukarimu kisha biashara iwe mbovu lakini we ufanikiwe kisa maombi? Hii haiwezekani hata kidogo. Tunaambiwa kifo ni mpango wa Mungu, na sasa unaumwa eti watu wanakuombea upone usife, maombi ya nini sasa wakati mnatuambia siku ya kufa ameipanga Mungu? Au ni kwamba Mungu anaweza kubadili siku yako ya kufa kwa sababu watu wamemuomba akuponye au mtu anaweza kufa siku ambayo Mungu hajapanga! Maombi hayasaidii chochote.

II. MUNGU ANAWAPENDA WANADAMU
Hebu soma mfano huu.
Kuna watu wawili wanakuja na zawadi kwa ajili ya watoto. Zawadi zipo 10 na watoto wapo 10, mmoja anaamua kugawa tu kwa kila mmoja kisha anaondoka zake ila mwingine anaamua kutoa mtihani kwanza na atakayefaulu ndo anapewa zawadi. Mwisho wa mtihani wanafaulu watoto wanne kisha wanapewa zawadi hao wanne jamaa anaondoka na zawadi zikizobaki anaenda kuzitupa. Kati ya hao ni Nani ana upendo? Bila kupepesa macho huyo wa kwanza ndo mwenye upendo.
Sasa ikiwa Mungu anatupenda kulikuwa na ulazima wa kutuleta duniani tuyashinde majaribu aliyoyaweka mbele yetu ndo atupeleke peponi? Kama peponi ni kukubwa na hakujai ni aina ipi ya upendo aliyonayo ambayo yupo tayari kuwapeleka watu motoni eti kisa wameshindwa majaribu wakati nafasi ya kuwaweka peponi ipo? Mtu anayekupenda hayupo tayari kukuona unatumbukia kwenye matatizo ikiwa anao uwezo wa kukusaidia, why Mungu hana upendo huu? Kama Mungu atawapeleka watu motoni hana upendo hata kidogo.

III. AMETUUMBA TUMUABUDU
Yaani katuleta duniani lengo kubwa la kutuleta ni kumuabudu na hataki kabisa na ni kosa kubwa kumuabudu kiumbe mwingine.
Ukiziuliza hizi dini, Mungu anapata nini tunapomuabudu? Jibu utakalopewa ni kwamba hafaidiki na chochote. Sasa utajiuliza, inamaana Mungu ametuumba tumfamyie kitu kisichokuwa na faida kwake? Utagundua kwamba huu ni uongo na hilo sio kusudio la kutuumba. Ikiwa mtu anaweza kuzaliwa leo na kufa kesho huyu atakuwa ametimiza kusudi la kuumbwa(kumuabudu muumbaji)? Ni wazi kusudio halijatimia, sasa hapo ni kwamba mipango mingine ya Mungu huwa inafeli. Kama hakuna mpango wa Mungu unaofeli, sio kweli kwamba tumeumbwa ili tumuabudu.

IV. ALITUMA MITUME KUTULETEA NENO LAKE
Sisi wanadamu tunaambiwa tumetoka kwake na kwake tunarejea. Sasa kulikuwa na ugumu gani wa yeye kutupa hayo maagizo wakati anatuumba ili tukifika duniani tuwe tayari tunajua cha kufanya kuliko anatuleta tukiwa empty ndo amtume mtu atuletee ujumbe wake! Hapo hapo amempa shetani uwezo wa kupenyeza ujumbe wake, maanaake hapo ni kwamba tuchanganyikiwe tusijue tufate lipi ili mwisho wa siku akatuadhibu kwa kutokufata maagizo yake ilihali yeye mwenyewe ndo ameyapa nguvu maagizo ya shetani yawe sambamba na yake.
Ukitafakari hilo kwa makini utagundua kwamba Mungu hajatuma mitume, hawa wanaojiita mitume akina mwamposa, Muhammad wamejituma wenyewe tu. Kuna uwezekano mkubwa Mungu hajataka kabisa tujue kuhusu yeye.

V. ANATAKA TUMTOLEE SADAKA
Huu ni uongo kabisaaaaa, yani hapo ni sawa mi nikupe milioni 1 kisha nakuomba laki 1. Mungu hawezi kufanya utoto huo. Eti miaka ya mwanzo ilikuwa Mungu anataka sadaka za kuteketezwa kabisa, yaani ukitoa sadaka ya mavuno au mnyama ni kwamba unavichoma vinateketea hivo vitu. Hii inamsaidia nini! Nadhani anasingiziwa, Mungu hawezi kufanya hivi. Niende kanisani nikatoe elfu50 kwa ajili ya Mungu kisha mwamposa azichange akajenge hotel, hivyo ndo Mungu anavyotaka? Habari ya kutoa sadaka sio ya Mungu msimsingizie.

VI. USIZINI
Yaani mi nimemtongoza mke wa jirani nikamla hii nayo iwe dhambi? Si amekubali mwenyewe kunipa mbususu why liwe kosa? Ingekuwa nimembaka hapo kweli ni kosa. Ni sawa na wewe nikuombe buku10 ukanipa halafu ionekane mi na wewe tuna makosa, ikiwa nimeichukua bila ridhaa yako hapo ndo itafsiriwe kosa.
Kwa nini kitendo ambacho watu wamekubaliana iwe dhambi? Mi nadhani watu waliona hili jambo la kulala na mke ambaye si wako halipendezi wakaona ili watu waogope na wasilifanye inabidi tuseme Mungu kakataza. Mungu angekuwa anakwazwa sana na hii kitu nadhani kusingekuwa hata na baraka za kupata mtoto watu wakizini. Msimsingizie Mungu, kuzini sio dhambi ila kubaka ndo dhambi.

VII. MSILE NGURUWE
Huu ni uongo wa waziwazi kinoma. Sasa nguruwe akiliwa kuna ubaya gani kwa Mungu hadi aamue kukataza? Hebu niambieni nguruwe ana kazi gani sasa kama asipoliwa? Mungu anapata hasara gani tukimla huyu mnyama hadi akataze? Acheni kumsingizia Mungu, hajakataza nguruwe kuliwa.

VIII. MUNGU HANA UPENDELEO
Ikiwa Mungu anamuacha mtu mwingine aishi miaka zaidi ya 80 na mwingine anaishi miaka haifiki hata 10 anakufa utasemaje Mungu hana upendeleo? Ikiwa Mungu alimuumba Yesu akampa nguvu ya kumshinda shetani na akashindwa kuwapa watu wote nguvu kama ya Yesu bado huamini kwamba ana upendeleo? Mtu unaishi maisha ya tabu tangu utoto hadi uzee na kuna mwingine anaishi maisha mazuri hadi anakufa ni kwa vipi mseme hana upendeleo? Mungu ana upendeleo.

IX. AMETUPANGIA SIKU YA KUFA
Ukifa leo watu wanasema siku yako imefika, ukifa kesho, mwakani au baada ya miaka kadhaa bado watu watasema hiyo ndo siku Mungu amekupangia ufe. Ikitokea ajali, mtu akifa tunasema Mungu amempenda zaidi, na mwingine akipona tunashukuru sana na kusema Mungu amemuokoa. Tuna akili kweli? Ukifa tu Mungu anasingiziwa kwamba ndo amepanga ufe.
Ingekuwa siku ya kifo ameipanga shetani kisha ukapata ajali mbaya na ukapona hapo tunaweza kusema Mungu amekuokoa, sasa kifo anapanga yeye na sasa hujafa ni kwa vipi tuseme amekuokoa? Kuokoa inabidi iwe hivi, ilibidi ufe leo ila utakufa mwakani, hapo ndo tutaita kuokoa. Sasa amepanga ufe mwakani itakuwaje wakati huu ambao hujafa ionekane umekuokoa?
 
Hizi changamoto zako zote zina majibu kwenye Maandiko ya Biblia, yani majibu very logical.

Mungu ni Mwaminifu, na anayosema yote hutimiza, shida ni watu si wakamilifu kwa Mungu.

Kila kitu kina input, then output, Biblia inasema maombi ya mwenye haki hujibiwa, kama huna haki?

Reference :


Yakobo 5:13-18
Neno: Bibilia Takatifu

13 Je, kuna mtu ye yote miongoni mwenu aliye na shida? Basi na aombe. Je, yuko mwenye furaha? Basi na aimbe nyimbo za sifa.

14 Je, kuna mtu miongoni mwenu aliye mgonjwa? Basi awaite wazee wa kanisa wamwombee na kumpaka mafuta katika jina la Bwana.

15 Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa huyo na Bwana atamwinua. Kama ametenda dhambi, atasamehewa.

16 Kwa hiyo ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana ili mpate kuponywa. Maombi ya mtu mwenye haki yana nguvu na huleta matokeo"


Tatizo la watu wanaojiita wa Mungu hawayafanyi Mungu anayotaka, hence no results.
 
Back
Top Bottom