Bado naona kuna irreguralities nyingi sana zilitokea ktk process nzima ya contracting,na uhamishaji wa contract.Hakika deni hili linaweza epukika kama wanasheria private watalivalia njuga.
Lakini kama itabidi lilipwe,basi ni serikali nasi Tanesco wa kulipa.Hakika naanza kurudisha imani kwa watendaji wa Tanesco kwa kuwa walifuata taratibu sawasawa,na kila walichofanya waliplay safe,waliyafanya yote hayo under DURACE,siwalaumu kabisa.Serikali wabebe zigo lao, lakini no one should go unpurnished,waadhibiwe wote walioacha mambo haya yatokee,waliosign mawasiliano ya wizara kwa Tanesco.
Halafu mheshiwa invisible, sisi wananchi sasa tuanze upya ku-overhaul system, tuhakikishe wote waliokua serikalini kipindi hicho wametoka, hili ni kama tutashindwa kuiondoa serikali nzima madarakani. Tuweke serikari mpya kabisa, tuanze upya.
Walikotufikisha hawa ni aibu kwa kizazi kijacho na kizazi kijacho kitatuhukumu kwa kutochukua hatua. Afadhali tuchukue hatua, watoto wetu wataona kuwa tulichukua hatua kwa kadiri tulivyoweza.