Hivi Watanzania tukiacha Ushabiki wa Siasa na Kuangalia Utendaji wa kazi na Uwajibikaji.. Pinda ana nini cha kujivunia katika miaka yake yoote alio kua waziri mkuu??
Ukiniuliza kumhusu Lowassa pamoja na ubaya wake lakini alituletea shule za kata, watoto wa wakulima tunasoma, aliwatimua ma DC na Wakandarasi wazembe, Mfano mkandarasi wa barabara ya Shekilango.. Sasa haya machache yana jirudia kwenye kichwa changu... Lakin kila nikijaribu kusaka Jitihada za Pinda sizipati..
Emu wadau Nisaidieni lipi jema Pinda kafanya kumzidi Lowassa kwenye Kazi??
N.B
Ukiondoa issue ya tuhuma ya wizi!!
Pinda ana uwezo mkubwa wakulialia
Pinda hana alicho fanya... Kilimo kwanza kampeni ya Kitaifa ilianzishwa kwa suport Kikwete!
Labda KILIMO KWANZA...nadhani ame-initiate ila sijui kama kinapumua.
Nakuunga mkono Marytina.
Hata hizi shule za kata wanazojivunia CCM, na ambazo mamia ya maelfu ya wanetu wanasoma huko pamoja na mapungufu yake, ni 101% kazi ya Lowassa.
Katika kuchagua mashetani wawili kwa kweli nitamchagua Lowassa...
pinda ni coward, hana jipya zaidi ya unafikinafiki tu
Wote takataka tu. Chombo kichafu hakitoi chakula safi. Lowassa kwa aliyoyafanya hasafishiki kupitia JAMII FORUM.munamuonaje PINDA-si mchapa kazi, anajiliza, analalamika maofisa kununua magari ya bei juu,hapingii rushwa kivitendo,ni ndumila kuwili (leo A kesho Z),anajifanya mtu wa kanisa,mtoto wa mkulima (bora angekuwa mtoto wa bilionea) anayechekelea nchii ikiangamia,
LOWASA-ni mchapa kazi anayeogopwa na maofisa wenzake serikalini (sifa muhimu),ana ujasiri na kujua maana ya cheo chake ni fisadi kivitendo (hana tofauti na PINDA asiyeupinga ufisadi).
hapa ni bora nchi kuwa na lowasa fisadi mchapakazi, kuliko PINDA mpalilia ufisadi asiyechapa kazi?