Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 3,734
- 6,292
Nimejaribu kutafakari uchambuzi wa CNN kuhusu kushikiliwa kwa Freeman Mbowe, kuna kitu wanaongelea sana pale "timing of arrest". Nadhani exposure yao ni kubwa sana kwa siasa za mataifa mbalimbali ikiwemo siasa za bara la Africa. Tunafahamu katika tools za kupatia taarifa kwa mashirika ya kijasusi kama CIA ni kuptia vyombo hivi vilivyoenea duniani kote, mfano BBC inatumika na MI6, kuna Aljazeera huko Asia na kadhalika.
Kiuhalisia CNN inaichambua hali yetu ya kisiasa kama ya mwaka mmoja uliopita na ikimnasibisha Mama yetu na Hayati Magufuli. Inasema kuwa yeye alikuwa msaidizi wake so inawezekana ameamua kuendeleza mfumo ule. Kimataifa hii inaturudisha kule tulipotoka, kule kwenye matamko ya jumuiya ya kimataifa, kule kwenye kuanza kututenga na kumuandama Rais wetu.
Tanzania siyo kisiwa hivyo tunapaswa kujenga taswira nzuri kimataifa. Simaanishi Sheria zisifuatwe la hasha lakini hizi sheria zinazoleta makosa yanayomnyima mtu Dhamana hata Samia alishazuia kutumika hovyo. Tunakumbuka kesi ya kina Mbowe ambayo walishinda kwa rufaa na kurudishiwa fedha zao, ikumbuke Mbowe alishakaa ndani miezi mi4 kama Sugu na Lema na wengineo.
CNN wanahoji je kudai katiba mpya, kukusanyika, kufanya kusanyiko wa kisiasa ni "Constitutional Rights" (Wao wameziona wapi hizi haki?) means wamesoma katiba yetu.
Kwa jicho la tatu maana yake wao wanaona kama Serikali yetu inatunyima haki zetu za kikatiba. Hii ina maana mbaya sana kwa 6th Regime ya JMTkimataifa hasa kipindi hiki ambacho Mama anataka kuifungua nchi kuongeza wawekezaji na kuleta Maendeleo ya kiuchumi.
Serikali ipambane na wavunja Sheria,iendelee kupambana na ugaidi lakini isiwabambikie kesi hasa kwa makosa yanayonyima dhamana.
Kazi na iendelee!